Ufahamu mchezo wa Chess: wataalamu wa mchezo huu tukutane hapa.

Ufahamu mchezo wa Chess: wataalamu wa mchezo huu tukutane hapa.

popomwitu

Senior Member
Joined
Aug 11, 2022
Posts
118
Reaction score
278
Habari ya wakati huu wanaJf, kama title ya uzi inavyojieleza shuka nao.

Chess ni moja ya michezo ya zamani zaidi na ya kimkakati duniani, yenye historia ndefu inayorudi nyuma zaidi hadi karne ya 6 huko India. Na ikasambaa Ulaya kupitia Waarabu na Wafarsi, hatimaye kuwa mchezo wa kisasa tunaoujua leo. Chess ilianza kuchezwa kwa sheria za kisasa mwishoni mwa karne ya 15.

Chess inachezwa na wachezaji wawili kila mmoja akiwa na vipande 16 Vikiwa na kete kama :– Mfalme, Malkia, Askofu, Farasi, Rukwaji, na Askari. Kila kipande kina mwendo wake maalum, na lengo ni kumzuia mfalme wa mpinzani katika hali ya "checkmate", ambapo hawezi kuepuka kukamatwa.

Chess inahitaji uwezo wa kufikiri hatua kadhaa mbele, jambo ambalo husaidia katika kutatua matatizo katika hali halisi ya maisha. Wachezaji wa chess wanahitaji kuwa na uvumilivu na umakinifu wa hali ya juu ili kuepuka makosa ya kiufundi wakati wa kuucheza mchezo huu.

Hawa ni wachezaji Maarufu wa Chess, ambao walisumbua Duniani kwenye mashindano Kadhaa ya chess :-

Magnus Carlsen: Bingwa wa Dunia wa Chess kutoka Norway, anayejulikana kwa uwezo wake wa hali ya juu wa kucheza na ubunifu wake kwenye ubao.

Garry Kasparov: Bingwa wa zamani wa dunia na mmoja wa wachezaji wakubwa wa chess katika historia.

Bobby Fischer: Mmarekani bingwa wa dunia, na anayejulikana kwa mchezo wake mzuri na upinzani wake kwa Warusi.

Pia soma vitabu hivi kujiimarisha zaidi kwenye mchezo huu:-

1. My System - by Aron Nimzowitsch
2. Think Like a Grandmaster - by Alexander Kotov
3. Silman's Complete Endgame Course - by Jeremy Silman

Wakali wa mchezo huu tupia mbinu, tuendelee kujifunza.
 
Back
Top Bottom