SerikaliUTT ni kampuni ya private au government?
Ivi mtu anaweza ishi kwakutumia hatifungani bila kufanya kazi yoyote ile?Habari wana Jf.
Hapa Tanzania Kuna fursa za uwekezaji katika Soko letu la hisa ( DSE) pamoja na UTT AMIS, lakini watanzani wengi hawajitokezi katika kufanya uwekezaji huo?
Je, unafikiri ni sababu zipi inapelekea hali hii? Na mambo gani yafanyike ili kuongeza wawekezaji katika Soko la hisa na UTT AMIS.
YOUNG INVESTORS FORUM- 3
Hamna shida hii project itawafikia wengi sana na kuwanufaisha Watanzania Wengi. Kufahamu zaidi unaweza kunicheki 0746617796
Ukizihitaji unazipata kwa utaratibu maalumu,,wa kujaza fomu na vipande vyako kuuzwa kwa mwingine,,Halafu ndani ya siku 5 za kazi unapewa mzigo wako..Iko hivyo kama sikosei
Jamaa kasema mwamko mdogo Sasa watamuuzia nani nafikiri utasubiri sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Mi nikawekeza kwenye mfuko wa DESI ikabaki week moja nivune serilkali ikafanya yake ndo basi tena kwa sasa siwezi kukuelewa mambo ya uwekezaji japo sina hela zenyewe
Ivi mtu anaweza ishi kwakutumia hatifungani bila kufanya kazi yoyote ile?
Sent using Jamii Forums mobile app
UTT wana, kwa mfano, mfuko wa Ukwasi au kimombo wanauita Liquid fund. Ukiujua huu walahi hutahangaika na fixed deposits za benki.
Sent using Jamii Forums mobile app
iseee mwendo wa kinyongaUTT unaweza wekeza kuanzia elfu 8 kwa mwezi. Kwenye uwekezaji muda ndio kitu muhimu kuliko ukubwa wa mtaji. Mwaka 2005 kipande kimoja cha mfuko wa UMOJA kilikuwa kinauzwa kwa 103.77 tzs lakini kwa rekodi za jana kipande hicho kina bei ya 623.79 tzs.
Hii inamaanisha kama ungewekeza milioni 1 mwaka 2005 kwa ajili ya mwanao wa miaka mitano kwenye mfuko wa UMOJA leo ungempatia mwanao huyo milioni 6 kama mtaji. Ikizingatiwa hapo kati ulikuwa huongezi uwekezaji.
UTT ipo chini ya wizara ya fedha Net Asset Value | UTTAMIS - Asset Management and Investor Services Plc
Slow but sure..Effortlessiseee mwendo wa kinyonga
kweliSlow but sure..Effortless
What about inflation?
What about it?
Kwa wanaoweza kufanya biashara mbalimbali kwa mafanikio, returns probably zitakuwa kubwa na kuzidi kabisa mapato ya hisa, utt, bonds nk. Inflation huko itashindwa. Lakini pia risk huko ni kubwa zaidi - hatari ya kupoteza mtaji ni kubwa zaidi.
Kwa tusioziweza biashara kwa sababu mbalimbali, au kwa wanaoogopa risk za biashara, kuweka akiba zao utt au katika hatifungani ni very logical. Very low risk.
Sent using Jamii Forums mobile app
Uwekezaji wa hisa kwenye hii awamu ya tano ni sawa na kuchoma pesa.
Awamu hii mauzo ya hisa yalishuka kwa kiwango ambacho hakija wahi onekana dokea DSE ianze.
Sent using Jamii Forums mobile app
UTT ni fursa kubwa kwa wenye mitaji midogo. Kuna mifuko unaweza kuanza na elfu 8000 kwa mwezi.
Mwenendo wa vipande vya UTT ni mzuri sana. Siku hizi unaweza kuweka pesa na kufuatulia account za utt kutumia simu.
Kwa uzoefu wangu kutoa pesa utt ni rahisi sana, hawajawahi kuchelewesha zaidi ya siku tatu za kazi(hii ni experience yangu)