Ufahamu mfuko wa uwekezaji UTT

Ukikokotoa mlingano huo uliouweka ninafikiri unataka kuangalia Returns vs inflation. Inategemea na rate ya inflation. Mfano 20yr treasury bond yetu (Tz) inayield 15.49% per year. Sijui inflation rate ni % ngapi- ikiwa kubwa kuliko 15.49% ni wazi kuna kupoteza. Iwapo inlfation ni ndogo kuliko 15.49%, then kuna gain.

Lakini iwapo fedha imekaa tu, au iko benki, inflation ndio italeta hasara zaidi sana.


Asante. Nilitamani nifahamishwe kuhusu mlinganyo huu:

Returns za mfuko+Pesa zilizowekwa vs Pesa zilizowekwa+Inflation.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau huko juu wameeleza sababu ya kutoelewa masuala ya hisa/utt/bonds. Ni sababu ya msingi.

Sababu nyingine ya watu kutokuchangamkia fursa hizo ni kutokuwa na utamaduni wa kuweka akiba. Wengi wetu hutumia kila kinachopatikana mara kinapopatikana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu?

I hope mko salama na Kama siyo poleni. Najuwa tupo ktk kipindi Cha ugonjwa wa Corona ila no way out. Tujikinge kwa Kila mtu kwa nafasi yake.

Lengo la uzi huu ni kuweza kupata ABC kutoka kwa wadau wanaowekeza ktk UTT AMIS kwani nimekuwa nikisikia hii kitu Ina faida Sana. Yaan unaweka pesa zako huko then unasubiri faida.

Wakuu, Mimi Nina tshs 100000/= naomba kujuzwa Hatua kwa Hatua Juu ya namna ya kuwekeza humo

AHSANTE.
--------
Mchango wa mdau:
 
Soko la hisa Dar ni bovu. Hisa hazipandi, zaidi zinashuka.
Wawekezaji hakuna
 
Mwanzilishi wa thread hii ungeeleza japo kwa kifupi kuhusu hiyo UTT AMIS ungefanya la maana sana, kwa sababu inaonekana ni kifupi cha maneno fulani.
 
kaifanyie bisahara, achana na huo upumbavu was wizi wa kileo
Hahahaa....dunia inaenda kasi sana mkuu.,biashara zimeshabadilika namna ya kuendeshwa...ndiyo maana Leo unaona kuna Watu wanaingiza pesa ndefu tu kupitia YouTube channel,Instagram n.k.

Tukubali mabadiliko Watanzania hasa kwenye kufanya biashara na uwekezaji kwa mbinu za kisasa,sayansi na technolojia tuitumie vyema itupe manufaa.

Leo mmiliki Wa Facebook,amazon,alibaba,n.k biashara zao sio za kubeba magunia yakaonekana kuwa hayo hapo yanauzwa,..ila.ndo matajiri wa dunia ya leo.(Mimi na wewe tunayekomaa na kubeba gunia mia za mahindi mpanda hadi.kahama tuko wapi? Mwaka wa kumi Leo...hahahaa...utani bhana)

Kinachowafanya wazidi kupaa juu kiuchumi hao matajiri ni kumiliki hisa tu za makapuni mbalimbali duniani,pia kupitia biashara zao nao wanauza hisa za makapuni yao ili kuongeza mitaji...hatimaye wanazidi kuwa matajiri.

Unaweza ukalima,ukawa mfugaji,mchimba madini,sijui msanii maarufu,nk.ila.usipojitahidi kuwekeza kwenye biashara mbalimbali hasa hizi mnazosema za kileo...(ingawa zipo tangu enzi) usitawi wako kimafanikio unaweza ukawa na changamoto zaidi kuliko wale Watu wanaoenda na mabadiliko ya kibiashara.

Hivyo basi UTT,ipo ni uwekezaji mzuri kwa Watu wenye malengo ya muda mrefu,na malengo ya kati,pia badala ya UTT,kuna hisa, hatifungani.

Pia biashara online zipo nyingi ambazo unaweza kuzitafuta mwenyewe na ukawekeza muda na akili yako huko na utapiga.pesa.

Hivi unadhani Millard ayo anapokuomba u subscribe YouTube yake,au u follow pages zake za kijamii unafiri hapati chochote?wee... thubutu yako. Lazima wa Tanzania tuamkie,tubadilike tuwe wa kisasa hasa Kwenye biashara za kisasa hizi nasi tunufaike.
Tuache ukale.
 
Mkuu huu ni uwekezaji mzuri ila elimu ndo changamoto, ukichukua kundi la vijana na watu walio na umri wa kati idadi ipatayo watu 100 inawezekana watu wanaofahamu DSE na vile inafanya kazi ni watu 10 tuu so elimu ndo tija kubwa.

Pia na walio na elimu hiyo wengi wanaogopa zile hasara ukizingatia watu wanajione ya ACACI, TOL,NIKO,PAL kwahiyo watu hofu inawaingia watu wanaona bora kunusuru kidogo chao.

Ila elimu ikitolewa yakutosha hasa kwa kampuni husika ambazo zinataka nguvu ya pamoja inaweza inua elimu na nguvu ya uwekezaji, mfano mzuri ni ka vodacom Tanzania walivyofanya, niwapongeze VODACOM TANZANIA maana walifanya kazi kubwa sana na watu walipata elimu ya uwekezaji katika hisa.
 
Umetisha bro!!🤝🤝🤝
 
Ndugu wapendwa naomba kufahamu kama kuna muelewa wa mfuko wa UTT unavyo fanya kazi, faida na changamoto zake.
 
UTT AMIS ilianzishwa mwaka 2013 kuchukua majukumu ya usimamizi wa Mifuko ya Uwekezaji wa pamoja kutoka kwa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) kufuatia maamuzi ya wamiliki kubadilisha muundo.

UTT AMIS, hapo awali ilijulikana kama Dhamana ya uwekezaji Tanzania (UTT) ambayo ilianzishwa chini ya Sheria ya Udhamini (Sheria yaDhamana Na. 318) na kupewa majukumu kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na Kuanzisha na kuendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja katika njia ambayo itaongeza thamani ya mifuko hiyo, kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba kupitia ushiriki mpana katika umiliki wa vipande.

JINSI UTT AMIS WANAVYOFANYA KAZI

Hawa jamaa wanapiga kazi kwa mfumo wa Mutual Funds, yaani wao wanakusanya pesa kutoka kwa wananchi au yeyote anayetaka kwa mfumo wa kuwauzia vipande, Kisha mjumuisho wa hela itakayokuwa imepatikana ndio UTT huitumia kwa kunua dhamana kwenye masoko ya Pesa, dhamana zinaweza kuwa hisa, hati fungani, zamana za serikali au mengineyo yanayo patikana kwenye soko la pesa.

Hii ina maana kwamba, anayenunua vipande UTT AMIS yeye husubiria gawio lake wakati wenye mfuko wao ndio huhangaika kujua ni sehemu ipi nzuri kuwekeza ili mwenye vipande aweze kupata faida baada ya muda waliokubaliana.

Uwekezaji wa aina huu unafanyika kama mtu anakuwa hapendi kuingia kwenye kashikashi za biashara za soko la fedha.

Ziko baadhi ya threads humu zikiwataja watu wakilalama kuhusu kushuka kwa bei ya hisa walizonunua kwenye IPO nk. Haya ni mambo ambayo mtu aliyewekeza kwenye mfuko wa UTT AMIS anaweza kuepukana nayo

Mutual Funds ni kati ya masoko ya pesa na anayeshiriki(mwekezaji/mwenye vipande) anatarajia gawio baada ya muda waliokubaliana wakati ananunua vipande.

NB: Unapotaka kufanya uwekezaji wowote waone wataalamu wa biashara pia jitahidi kujielimisha kbala haujajiingiza katika suala husika, masoko ya pesa ni kama masoko ya bidhaa nyingine unaweza angukia pua pia.



Signed

Oedipus
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…