kaifanyie bisahara, achana na huo upumbavu was wizi wa kileo
Hahahaa....dunia inaenda kasi sana mkuu.,biashara zimeshabadilika namna ya kuendeshwa...ndiyo maana Leo unaona kuna Watu wanaingiza pesa ndefu tu kupitia YouTube channel,Instagram n.k.
Tukubali mabadiliko Watanzania hasa kwenye kufanya biashara na uwekezaji kwa mbinu za kisasa,sayansi na technolojia tuitumie vyema itupe manufaa.
Leo mmiliki Wa Facebook,amazon,alibaba,n.k biashara zao sio za kubeba magunia yakaonekana kuwa hayo hapo yanauzwa,..ila.ndo matajiri wa dunia ya leo.(Mimi na wewe tunayekomaa na kubeba gunia mia za mahindi mpanda hadi.kahama tuko wapi? Mwaka wa kumi Leo...hahahaa...utani bhana)
Kinachowafanya wazidi kupaa juu kiuchumi hao matajiri ni kumiliki hisa tu za makapuni mbalimbali duniani,pia kupitia biashara zao nao wanauza hisa za makapuni yao ili kuongeza mitaji...hatimaye wanazidi kuwa matajiri.
Unaweza ukalima,ukawa mfugaji,mchimba madini,sijui msanii maarufu,nk.ila.usipojitahidi kuwekeza kwenye biashara mbalimbali hasa hizi mnazosema za kileo...(ingawa zipo tangu enzi) usitawi wako kimafanikio unaweza ukawa na changamoto zaidi kuliko wale Watu wanaoenda na mabadiliko ya kibiashara.
Hivyo basi UTT,ipo ni uwekezaji mzuri kwa Watu wenye malengo ya muda mrefu,na malengo ya kati,pia badala ya UTT,kuna hisa, hatifungani.
Pia biashara online zipo nyingi ambazo unaweza kuzitafuta mwenyewe na ukawekeza muda na akili yako huko na utapiga.pesa.
Hivi unadhani Millard ayo anapokuomba u subscribe YouTube yake,au u follow pages zake za kijamii unafiri hapati chochote?wee... thubutu yako. Lazima wa Tanzania tuamkie,tubadilike tuwe wa kisasa hasa Kwenye biashara za kisasa hizi nasi tunufaike.
Tuache ukale.