Changer 22
Member
- Jul 29, 2022
- 11
- 5
Nini nikasome baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari..?
Inawezekana likawa swali ambalo linajirudia mara kwa mara kutoka kwa ndugu, marafiki hata wazazi wakitafuta kitu Bora Cha kusoma baada ya kuhitimu elimu ya sekondari.
Kukosekana kwa elimu sahihi au kukosa muongozo mzuri wa kitu Cha kusoma baada ya kuhitimu inawezekana ikawa ni sababu Moja wapo ya asilimia kubwa ya wahitimu wa elimu ya sekondari wakose dira ya maisha yao ya baadaye.
Bado asilimia kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa katika vyuo mbalimbali wanakiri kuwa kada walizochaguliwa hazikuwa sehemu ya vipaumbele vyao hivyo wanasoma kutoka na ndio chaguo waliochaguliwa wakajifunze. Wengine waliamua kwenda kusoma kozi ambazo Kuna uwezekano wa kupata mikopo chuo. Sababu ambayo hupelekea wanafunzi wengi kupoteza ndoto zao ambao zingewasaidia kufikia malengo Yao.
Vijana wa kijijini huadhirika zaidi kutokana na kukosa msaada wa ushauri juu ya kipi Cha kujifunza...?
Ongezeko la matumizi ya mitandao ya kijamii, matumizi ya smartphone kumeongezeka zaidi kote mjini na vijijini lakini hii haizuii kuwa Bado vijana wengi wanaotoka kijijini Bado wanapata changamoto zaidi kuhusiana na upatikanaji wa taarifa kamili na fursa zilizopo kwenye hicho wanachosomea ambapo hii hupelekea kukosekana kwa mwelekeo mzuri kwa asilimia kubwa kwa vijana.
Kipi kifanyike katika kuisaidia Idadi kubwa ya vijana wanaokosa mwelekeo wa kitu Cha kwenda kusoma vyuoni..?
Uanzishwaji wa seminar na warsha za kutoa elimu kwa vijana wa vijijini zinaweza kuwa sehemu sahihi ya kuwasaidia vijana kujua Nini Cha kwenda kujifunza wanaotarajia kujiunga na chuo.serikali inahitajika kuangalia njia sahihi ya kuwaidia vijana wengi wanaopoteza matumaini ya kupata kitu sahihi Cha kwenda kujifunza.

Upvote
0