fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 2,977
- 3,798
Ni jioni sasa,nimesima hapa sebuleni kwangu,naangalia nje,mvua inanyesha.Naangalia miti na maua inavyopeperushwa na upepo, ni shwaaaaaaaaa, sauti ya majinya vua, na fyuuuuuuuuuuuuuuuu, sauti ya upepo,nani kwangu ni kimyaaaa kabisa,narudisha macho ndani,nakutana na vitu vya nyumbani, meza, viti, makochi, majokofu, majiko, vyombo na tumashine mbalimbali twa upishi,kusafisha nyumba na mapambo.
Nawaza huku naaangalia huo umbali niliotoka, ni mrefu sana, ila naangalia huo umbali naoenda ni mfupi, basi namsujudia Mola wangu na ufalme wake.
Nafurahia amani kwenye moyo wangu,amani ambayo haipimwi na mali nikiyonayo,au ambayo sina,haipimwi na furaha au shida za naoishi nao,ni amani bayo Mungu kanipa kumjua kila aliyekaribu nami na aliye mbali nami. Asante MOLA wangu