Ufalme wa P Funky Majani ndani y East Africa!

Aman peaceful

Member
Joined
Mar 2, 2018
Posts
89
Reaction score
63
Wasaalamu WanaJf popote mlipo..!

Nimeona ni bora leo tukaukumbuka ufalme wa Prodyuza mkali bongo na East Africa kwa ujumla ndugu Paul Majani!
Ukiachilia mbali Kipaji chake cha kutengeneza midundo mikali ya wasanii mbalimbali, P majani anafahamika pia kwa Ukorofi wake hasa ukimzingua! rejea ..kipigo heavy alichomshushia Afande Sele!

Bila shaka kwa mziki wa Bongo hapa ulipofikia karibu Asilimia 85 zinamhusu Majani mwenyew na ninakiri wazi kuwa yeye ni legend wa Music Bongo!

Wasanii wengi wakubwa hasa wa hiphop wamepita ktk mkono wa Majani! achilia mbali vibao vikali sana vya kitambo unavoweza kudhani labda vimepikwa jana tu! Mfano; zali la mentali by Prof. Jay!

Hapa Bongo, P Majani amekumbana na visa vingi tu ikiwemo Beef lake na mzazi mwenzie, Kajala, Kumproduze kimwil rayc bila kusahau kitu cha jamaica!

Ninaomba tujikumbushe Mafanikio yake katk muziki, visa vyake mbalimbali na mastaa wa bongo, bila kusahau maisha yake kwa ujumla kama njia mojawapo ya kuendelea kufurahia uwepo wake katika industry ya muziki hapa bongo!

Ameifanyia makubwa sana Industry ya muziki Hapa Tz, He is a living Legend indeed!

Respect Sana P!
 
Kumproduze kimwili Ray C? Hebu fafanua.

Vinginvyo namkubali sana huyu jamaa kwa kazi zake. Ukorofi wake tumwachie maana kila mmoja antabia zake,kipaji ndicho muhimu kujadili maana kinawezankuwa nafaida hata kwa wengine wenye fikra sawa na zake
 
Kiufupi ilikuwa ni kutoka nae kimwil mkuu!
Hakika kipaji chake cha muziki ni kitu cha kujivunia sana mkuu
 
P funk alikuwa mkali enzi hzo cheki pin za kina jebby na wakal wengne huez fananisha na miondoko ya sasa,,,,,old skul ni mwanzo mwixho[emoji120]
Hakika mkuu! Produza wa sasa wana mengi ya kujifunza kutoka kwake coz yeye alikuwa ni full kipaji! naskia msanii kurekod bongo recorz enzi hizo lazima uwe umejipanga haswa! ukizngua tu ni mitusi toka kwa P!
 
Yani ktk Africa mashariki hasa ktk nchi kubwa kuliko zote Africa mashariki, yaani Tanzania, kuna miguu mitatu iliyoinua huu mziki hadi kufikia hapa ilipo heshima kwao mabraza, p funk, mikamwamba, na master j. Hakika Tanzania haitawasahau. Wameacha alama.
 
hakika Mkuu! Mungu awabariki sana kwa Alama muhimu walioiacha.
 
Yaan beat za majani unaweza sikiliza bila mtu kuimba bado ukaenjoy ..jamaa aliku genius wa beats moja ya ma producers wangu bora wa mziki bongo muda wote kwa nini tusirud enzi za old skul ata kidogo [emoji3] kule ndio mziki ulikuwa mziki acha tarabu na makanjanja ya mziki wa saivi
 
hakika mkuu ..wengine watasubir sanaaaaaa
 
P funk alikuwa mkali enzi hzo cheki pin za kina jebby na wakal wengne huez fananisha na miondoko ya sasa,,,,,old skul ni mwanzo mwixho[emoji120]
Jebbyb hajawah kufanya nyimbo kwa majani acha kupotosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…