Ufanisi wa kazi kwa watumishi wa umma ni mdogo sana

Ufanisi wa kazi kwa watumishi wa umma ni mdogo sana

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Wanabodi, twende mbele, turudi nyuma, wafanya kazi wengi wa serikali (zaidi ya 70%) hawana ufanisi katika kazi zao. Ni kama serikali inawalipa mishahara ya bure kabisa.

Kada za ualimu, afya, ulinzi/usalama (Polisi, Magereza, Wanajeshi), sheria(mahakimu) zinajitahidi sana hata kuingia kazini mapema, kuchelewa kutoka kutokana na majukumu yao....

Watumishi wengi wa serikali kwenye hizi Halmashauri zetu hawafanyi kazi kabisa, wanaenda kazini kupiga stori tu. Mtu anaenda kazini saa 2 asubuhi, saa 4 anatoka kwenda kunywa chai lisaa lizima, saa 8 mchana mtu ananyanyuka huyoo anarudi nyumbani, halafu anaenda kumwambia mkewe/mumewe kuwa katoka kazini. Ni uongo mkubwa.

Usione mtu anaonekana smart serikalini, kavaa vizuri anawakaa....performance yake ni ndogo mno. Hawana outputs kabisa yaani. Watu wanavizia genji tu hasa kwenye shughuli kuu za kitaifa hasa uchaguzi, mitihani, sensa, ziara za viongozi wakuu wa kitaifa n.k!

Mshahara ambao serikali inawalipa watumishi wa umma unatosha sana. Tusidanganye umma.
 
Kweli kabisa,maana wengi ajira zao wamezipata kwa mchongo,

Huwa naangalia maofisa wa idara moja wakija kukagua mitambo yetu ya mawasiliano,yaani mpaka huwa najiuliza,Hawa walifakaje hapo,

Maana ukiacha usmart nakunukia unyunyu wa bei mbaya,hawana maajabu,

Kuna siku nimeenda ewura,kuulizia leseni,nawaambia Mimi nywira ya akaunti yangu nimeisahau,sasa wao wenye system waniangalizie kama leseni imetoka,na ipo wapi!!jasho tupu,wananiambia niende Kigoma kuuliza!!nitoke Dar mpaka Kigoma
 
Usione mtu anaonekana smart serikalini, kavaa vizuri anawakaa....performance yake ni ndogo mno. Hawana outputs kabisa yaani. Watu wanavizia genji tu hasa kwenye shughuli kuu za kitaifa hasa uchaguzi, mitihani, sensa, ziara za viongozi wakuu wa kitaifa n.k!

Mshahara ambao serikali inawalipa watumishi wa umma unatosha sana. Tusidanganye
SERIKALI sikivu ya CCM.....uitaje Kabisa
 
Kazi ziwe za mikataba mifupi mifupi zenye kuonesha mlengo au unaenda kifanyia nini. Sheria kali uwekwe ukisababisha hasara au upotevu
 
Huu ni ukweli kabisa bongo wafanyakazi hawatimizi kabisa majukumu yao kwa ufasaha ila siwalaumu sana kwa hili, ni kutokana na uongozi mbovu pia kuanzia juu. Huku ughaibuni wenzetu wanapiga kazi sana sio kwa sababu malipo ni mazuri sana la hasha. Wenzetu viongozi wenyewe wanafanya kazi kama vile ni ya kwake, sasa mtu wa chini ataanzaje kukwepa majukumu iwapo viongozi wanafanya kazi sana. Hata kipindi cha mwendazake nasikia wabongo walibadilika sana kiutendaji, sasa alipokuja huyu wa " kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake", basi hali ikarudi back to square 1.
 
Suala la kutopenda kuwajibika na kujituma ni janga la Kitaifa. Serikalini ukiwa mchapakazi na mtu wa kuhimiza watu wajitume na kutofuja mali za Serikali utapewa kila majina machafu na yenye kebehi. Mfano Mhe. Rais aliyepita wapigaji akina Nappe na Genge lake walisikika wakimuita MSHAMBA.
So aina hiii ya utamaduni imeota mizizi kwenye sekta zoooote za Umma na umekuwa ugonjwa suguuuu.
Tunahitaji Aje Rais mwenye maamuzi magumu sana na anayeujua Utumishi wa Umma kuondoa Ombwe hili la aibu.
 
Sasa kama maboss hawatupi kazi nyingi za kufanya sisi tufanyaje...sisi tunafanya kazi kutokana na anavyopanga supervisor and not otherwise
 
Ungetaja kada zembezi na siyo kutujumlisha sote...huku kwetu tupo watumishi kumi wanafunzi 700k ..unataka tufanye kazi kwa kiwango gani..halafu mnakofanyakazi Sana mna marupurupu kibao...naendelea kulimia shamba langu nikikuta kazi nitafanya jumatatu.
 
Back
Top Bottom