Ufanisi wa madaktari wa Tanzania umeshuka, tatizo ni nini?

Siyo wa sasa. Hadi wa zamani, tena hao ndiyo mabomu kabisa. Kilichopo ni wagonjwa wanajielimisha na wana uelewa sana siku hizi. Madaktari wa zamani wengi ni hovyo kabisa.
 
Ndugu hamna kinachoshndikana kwenye nchi hii sawa mtoa mada kaeleza aliyo kutana nayo wewe unabisha
Ni kweli hakuna kinachoshindika ila form failure waliopata alama D wanaishia uku uku level ya zahanati hawana nafasi zaidi ya hapo na ndio hao hao wanaozalisha matatizo sugu,,utakuta clinical officer au assistant clinical officer anatoa dawa kwa mtu ambaye hana history ya hypertension wala dalali za hypertension ghafla tu pressure ipo juu moja kwa moja anakurupuka anampa dawa za pressure hajacheck renal function test,liver,ecg,eco nk

Serikali/wizara ya afya inabidi iliangalie ili swala kwa makini sana afya za watu zipo hatarini
 
Hivi madaktari wa siku hizi wana shida gani! mbona kama ni hawajui kitu tena!? Yaani siku hizi ukienda hospitali utapata tiba ya haraka kama unaumwa magonjwa yaliozoeleka kama malaria,typhoid, u.t.i nk lakini kama unaumwa kitu ambacho hakijazoeleka unaweza ukafia hapo wanakuangalia.

Yaani imefika mahala mtu ukiumwa unaona hakuna umuhimu wa kwenda hospitali kwasababu unajua kabisa utakavyoambiwa na dawa utakazopewa.

Na wamekuwa wabishi sana hata ukijaribu kuwaelezea ni jinsi gani unaumwa na unavyojisikia wao wanaconclude mambo yao fasta fasta bila kujali hali ya mgonjwa.

NIliwahi kupata tatizo linaitwa Acute Pancreatitis miaka ya nyuma, nikashauriwa kuwa atleast kila mwaka nifanye check-up ya kongosho ili nijue utendaji kazi wake kama upo sawa au la...ili nisije kupata complications za kufeli kwa kongosho kama kupata ugonjwa wa kisukari ambao tayari nishaupata, nilijaribu kila mara kwenda kwenye hosp tofauti tofauti mikoani hadi kwenye hosp za rufaa za baadhi ya mikoa lakini cha ajibu utakuta umemuelezea daktari aina ya tatizo ulilopata inakuwa ni kama unamfundisha na yeye hajui chochote, yaaani uwe na historia ya acute pancreatits halafu daktari anakuandika ukapimwe u.t.i!!

Are these doctors serious! maana hata afya yangu ilipofikia madaktari pia wamechangia kunifikisha cos ningefahamika mapema kuwa kogosho yangu haijakaa sawa basi ningeanza mapema matibabu huwenda nisingepata kisukari.

JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala TANZANIAN DOCTORS
Mimi niliwahi kutoa maoni hum kwenye uzi wa aina hii watu wakapuuza kumbe ni watu wengi wanakutana na mambo haya!!

Miaka miwil iliyopita dengue ilivoingia nchini me nilikua miongoni mwa wale wagonjwa wa mwanzo kabisa waliokumbana na huo ugonjwa, mwanzo huu ugonjwa hata vipimo vilikua vinapatikana ktk hosptal chache kubwa za serikal na binafs yaan dalili zake kama malaria.

Sasa me niliumwa sana nikazdiwa nikaenda hosptal fulan nilikua sijelewi kabsa hali niliyokua nayo ni mbaya, kufika pale niakalazwa kwanza wakafanya vipimo nikaambiwa na malaria na UTI kali nilipata nafuu usku wakaniruhusu ila nilitakiwa kurud asubui kuanza dozi ya sindano za UTI.

Siku ya kwanza nikachoma , siku ya pili nikachoma nilizidiwa zaid ya mwanzo tukaenda hosptal fulan ya waarabu kufika pale tukatoa lile kadi la hosptal ya mwanzo wale walivonipima walisema naumwa dengue tu hivo vingine walivoadnika hao siumwi.

Ugonjwa hauna dawa pale walichkua wanafanya wanakuwekea drip 2 asubui na jion 2 kwa sku 5 unakua fresh.sasa jiulize ile hospital ya kwanza si walitaka kuniua bila hatia kwa kuniandikia misindano ya UTI wakati siumwi UTI!! Yule dokta uchwara wa kile kihosptal nilimtaman sana bas tu
 
Yaani imefika mahala mtu ukiumwa unaona hakuna umuhimu wa kwenda hospitali kwasababu unajua kabisa utakavyoambiwa na dawa utakazopewa.
Ndugu yangu alikaa miezi kadhaa haponi mguu alioungwa Muhi2, baada ya kupelekwa hospital moja iko maeneo ya Temboni ikagundulika wataalamu waliegesha tu screws kwenye chuma
 
[emoji26]
 
Sitasahau dada yangu aliambiwa ana matatizo ya figoo na kuanza kutumia dawa Ila wapi bado anapata maumivu sana na anaumwa kweli imeenda zaidi ya miezi6 nikamwambia aje mkoa niliopo kwenda hospital ya rufaa apa pia wanasema ivyo ivyoo anapewa dawa Ila Hali Badoo haibadiliki nikasema ngoja niende private Kwanza akatushaurii tupige ultrasound tukaungwanishwa Kwa jamaa mmoja maana ya apo hospital ilikuwa mbovu jamaa akafanya majibu aliyoyatoa yalinishangaza sana kwamba figo hazina shida Ila ovari zimetokewa na viuvimbe vidogo ndyo vinasababisha aumwe ivyoo tukapewa dawa baada ya wiki mbili mtu kapona haumwii tena nikasema aisee mtu unaweza kufa au kutumia dawa ambazo haziusiani na ugonjwa ulionao sema sababu nyingine hospital za serikali wahudumu wachache wagonjwa wengi vifaa vichache kwaiyo mtu analipua tu
 
Labda nikuweke wazi kiongoz, sisi Ma Dr hatuna tatizo kwenye kuelekeza mgonjwa nini chakufanya,
Unachotakiwa kujua ni kwamba maelezo yako kwa lugha nyepesi utakavo jieleza vizur ndivo utakavo nisaidia kujua nini kinakusumbua .

Ila ukishindwa kujieleza ndipo hapo aslimia kubwa utakuta tunatumia lessons ya clinical feature.
 
Ndio maana veternary medicine ni watu na nusu.
 
Hivi madaktari wa siku hizi wana shida gani! mbona kama ni hawajui kitu tena!? Yaani siku hizi ukienda hospitali utapata tiba ya haraka kama unaumwa magonjwa yaliozoeleka kama malaria,typhoid, u.t.i nk lakini kama unaumwa kitu ambacho hakijazoeleka unaweza ukafia hapo wanakuangalia.

Yaani imefika mahala mtu ukiumwa unaona hakuna umuhimu wa kwenda hospitali kwasababu unajua kabisa utakavyoambiwa na dawa utakazopewa.

Na wamekuwa wabishi sana hata ukijaribu kuwaelezea ni jinsi gani unaumwa na unavyojisikia wao wanaconclude mambo yao fasta fasta bila kujali hali ya mgonjwa.

NIliwahi kupata tatizo linaitwa Acute Pancreatitis miaka ya nyuma, nikashauriwa kuwa atleast kila mwaka nifanye check-up ya kongosho ili nijue utendaji kazi wake kama upo sawa au la...ili nisije kupata complications za kufeli kwa kongosho kama kupata ugonjwa wa kisukari ambao tayari nishaupata.

Nilijaribu kila mara kwenda kwenye hosp tofauti tofauti mikoani hadi kwenye hosp za rufaa za baadhi ya mikoa lakini cha ajibu utakuta umemuelezea daktari aina ya tatizo ulilopata inakuwa ni kama unamfundisha na yeye hajui chochote, yaaani uwe na historia ya acute pancreatits halafu daktari anakuandika ukapimwe u.t.i.

Are these doctors serious! maana hata afya yangu ilipofikia madaktari pia wamechangia kunifikisha cos ningefahamika mapema kuwa kogosho yangu haijakaa sawa basi ningeanza mapema matibabu huwenda nisingepata kisukari.
Pengine ni stress za mishahara midogo na ugumu wa maisha, matokeo yake madktari na wauguzi wamekuwa wakitafuta fursa za kuongeza kipato badala ya kufanya kazi kwa utashi na moyo wa kujitoa kama watoa huduma.

Hii inchi ina kimbilia kuboresha miundombinu ila ina sahau ustawi wa watumishi, pili waajiri watoa huduma wa kutosha, maana kichwa kimoja kitibu watu 200 kwa siku si mchezo, akili ikichoka na hama wa kumpokea inabidi asukume tu muda uishe akapumzke. Watoe ajira kuwe na medical staff ya kukidhi mahitaji.

Tukikamilisha mazingira rafiki kwa wao kufanya kazi sasa tuwahukumu kwa kupuyanga.
Japo wapo wanaopuyanga hata kama wana kila mazingira rafiki katika kituo husika, hao wanaweza kuripotiwa kwenye mamlaka zao wakashughulikiwa, pengine ni tabia yake au ni incompetent, atolewe kunusuru maisha ya wananchi.
 
Labda nikuweke wazi kiongoz, sisi Ma Dr hatuna tatizo kwenye kuelekeza mgonjwa nini chakufanya,
Unachotakiwa kujua ni kwamba maelezo yako kwa lugha nyepesi utakavo jieleza vizur ndivo utakavo nisaidia kujua nini kinakusumbua .

Ila ukishindwa kujieleza ndipo hapo aslimia kubwa utakuta tunatumia lessons ya clinical feature.
Sio hivyo bana. Kubali tuu Uzembe upo. Na huwa unatokea.
 
Hivi madaktari wa siku hizi wana shida gani! mbona kama ni hawajui kitu tena!? Yaani siku hizi ukienda hospitali utapata tiba ya haraka kama unaumwa magonjwa yaliozoeleka kama malaria,typhoid, u.t.i nk lakini kama unaumwa kitu ambacho hakijazoeleka unaweza ukafia hapo wanakuangalia.

Yaani imefika mahala mtu ukiumwa unaona hakuna umuhimu wa kwenda hospitali kwasababu unajua kabisa utakavyoambiwa na dawa utakazopewa.

Na wamekuwa wabishi sana hata ukijaribu kuwaelezea ni jinsi gani unaumwa na unavyojisikia wao wanaconclude mambo yao fasta fasta bila kujali hali ya mgonjwa.

NIliwahi kupata tatizo linaitwa Acute Pancreatitis miaka ya nyuma, nikashauriwa kuwa atleast kila mwaka nifanye check-up ya kongosho ili nijue utendaji kazi wake kama upo sawa au la...ili nisije kupata complications za kufeli kwa kongosho kama kupata ugonjwa wa kisukari ambao tayari nishaupata.

Nilijaribu kila mara kwenda kwenye hosp tofauti tofauti mikoani hadi kwenye hosp za rufaa za baadhi ya mikoa lakini cha ajibu utakuta umemuelezea daktari aina ya tatizo ulilopata inakuwa ni kama unamfundisha na yeye hajui chochote, yaaani uwe na historia ya acute pancreatits halafu daktari anakuandika ukapimwe u.t.i.

Are these doctors serious! maana hata afya yangu ilipofikia madaktari pia wamechangia kunifikisha cos ningefahamika mapema kuwa kogosho yangu haijakaa sawa basi ningeanza mapema matibabu huwenda nisingepata kisukari.
Tamaa ya pesa mzee sikuhz wahonjwa wengi hufia hosptal siku si zao yani unyama kbsa utu haupo...
 
Labda nikuweke wazi kiongoz, sisi Ma Dr hatuna tatizo kwenye kuelekeza mgonjwa nini chakufanya,
Unachotakiwa kujua ni kwamba maelezo yako kwa lugha nyepesi utakavo jieleza vizur ndivo utakavo nisaidia kujua nini kinakusumbua .

Ila ukishindwa kujieleza ndipo hapo aslimia kubwa utakuta tunatumia lessons ya clinical feature.
Na hapa ndipo shida kubwa ilivyo.

History taking ni ishu ya msingi sana kwenu madaktari.

Unakuta daktari hashawishi kabis amgonjwa kufunguka,au mgonjwa mwenyewe anakuwa msirimsiri mwishowe anampa shida daktari kujua tatizo.

Mgonjwa anapojieleza vizuri anakuwa ndio daktari mwenyewe.
 
Sio hivyo bana. Kubali tuu Uzembe upo. Na huwa unatokea.
Hahaha hamna mzee ukisema uzembe maanake unataka kuishi duniani miaka 200 , sisi tunapambana kunusuru maisha ya wanadamu ila inapofika hatua tunamwachia alieko juu afanye yake
 
Mi nakubali kwenye hii Field uzembe upo sana, na ni kuanzia Hospital za Juu kabisa mpaka chini.

Halafu sio siku hizi hata zamani uzembe ulikuwepo.
Sema Siku hizi ile hali ya kuwaona madaktari wanajua kila kitu imepungua, kutokana na maendeleo ya teknologijia. Hii imefanya blunders za madktari na wauguzi zionekane kirahisi.

Vitu vinavyochangia uzembe mi ninavyoona.

Moja ni daktari kutokuwa na ufahamu wa kitu anachokiona kwa mgonjwa + kukosekana kwa vipimo husika.
Kwasababu mara nyingi features anazopresent mgonjwa zinarandana na magonjwa mengi. Sasa kama hakuna kipimo cha kutofautisha. Utaishia kupewa dawa Malaria. Au utaambuawa huna tatizo.

Pili kitu kinacholeta uzembe ni kazi nyingi, hasa hawa madaktari bingwa unakuta 24/7, Ratiba imejaa + Uchovu.

Inshu nyingine ni watu wanatanguliza masilai, hata kama anaona kwenye hospitali yao hawataweza kukusaidia, watakutafuatia ugonjwa, ili tuu waingize mapato.
 
Back
Top Bottom