HONGERENI SANA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA.
Wapendwa wana JF habarini za asubuhi?,Kama kichwa kinavyojieleza,Wiki iliyopita nilikwenda Hospitali ya Rufaa ya nyanda za juu kusini-Mbeya kwa lengo la kufanya Check up ya mwili mzima kutokana na kutojisikia vizuri,Ikumbukwe kuwa hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kwenda ktk hospitali hiyo.
Baada ya kuwasili hospitalini hapo nilipokelewa vizuri sana nikawa naelekezwa vizuri sehemu ambazo napaswa kupita,baada ya vipimo niligundulika na tatizo ambalo ilikuwa lazima kufanyiwa Upasuaji.Basi Daktari alinipa maelekezo kuhusu tatizo nililonalo, kisha akaniuliza ikiwa nipo tayari kufanyiwa operation siku ya pili asubuhi,nami nikakubali.
Baada ya kukubali kufanyiwa operation,nikalazwa;Nami nikaomba kuwekwa Wodi ya Private Usiku wote wakati Nasubiria kufanyiwa operation Madaktari walinitembelea na kunichukua vipimo mbalimbali na kunifariji kuwa nisiwe na wasiwasi kuhusu operation hiyoe.Ilipofika saa kumi na moja Alfajiri niliamshwa na kuambiwa kuwa nijiandae kwaajili ya operation,nikajiandaa kwaajili ya operation nikaenda Theater.Madaktari walinifanyia Operation kwa upendo mwingi huku Manesi wakinibembeleza kwa sauti nyororo, baada ya operation nikaanza kusikia maumivu makali lkn nilifarijiwa sana kwa huduma nzuri za Wataalamu wetu wa Afya.Nilipoanza kijisikia vizuri niliruhisiwa kurudi nyumbani,hivi sasa naendelea vema,bado natumia dozi ya dawa nilizopewa.
Hitimisho.
Binafsi nimevutiwa na kufurahishwa sana na huduma za Hospitali hii,kuna wakati nilimuuliza mke wangu aliyekuwa ananiuguza,"Hivi hii ni hospitali ya Private au ya Serikali?",Jibu likawa ni ya Serikali,niliuliza hivyo kutokana na kushangazwa na huduma zao bora sana.Hebu fikiria Daktari aliuenifanyia operation alinipigia simu saa nne usiku kuniuliza ninaendeleaje? Na akasema kupitia Namba yake hiyo nimpigie simu muda wowote ikiwa Kuna shida inanipata.Kwa kweli sikuona mhudumu aliyenijibu Vibaya au kutonijali.Ilifika wakati nikawaza kuwa ningekuwa Rais wa nchi hii ningeamuru Mshahara wa Watumishi wa wizara ya Afya uongezwe.Hongereni sana Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya nyanda za juu kusini-Mbeya kwa Huduma yenu bora sana.Mwenyezi MUNGU awabariki sana.