Ufanisi wa madaktari wa Tanzania umeshuka, tatizo ni nini?

Hahaha hamna mzee ukisema uzembe maanake unataka kuishi duniani miaka 200 , sisi tunapambana kunusuru maisha ya wanadamu ila inapofika hatua tunamwachia alieko juu afanye yake
Labda nitumie neno mistakes

Mistakes zinafanyika sana hospitalini, katika kumtibu mgonjwa.

Daktari nae ni binadamu anafanya mistake kama watu wengine.
 
Dah!...pole sana boss.

Hii sekta ya afya inahitaji usimamizi making sana.
 
Sidhani kama Kuna daktari hamsikilizi mgonjwa,ni wachache mno madaktari wenye tabia hizo,Kila daktari anajitahidi kuhudumia mgonjwa wake apone vizuri,Tena wengine hata ukiwapigia simu ukamweleza tatizo lako la kiafya anakupatia maelezo mazuri kitu Cha kufanya,sema labda ulikutana na Mmoja ambaye naye anamatatizi yake,sio madaktari wote .
 

Pole sana Mkuu

Hii code kama naifaham hiv
 
Da! Nikama yalionikuta. Nilipewa za
ikashuka haswa, nikapewa za kuipandisha, ikapanda kuwa karibu na normal . Nikajiuluza mbona mimi sina historia ya kuwa ma BP.
Mother akaniambya "babu yako alizitumia muda mrefu hatimae mishipa ikabast akafa" Nikaogopa na ikawa ndio mwisho wa kuzitumia mpaka sas nipo kawaida, nimegundua kumbe maumivu yapo kwenye misuli ya nje na sio ya ndani moyo.
Ukweli mwili wa binadamu unawasumbua sana madokta.
Tatizo langu nimepimwa hispitali tano + na kila mmoja katoa jibu lake tofauti na mwenzie, ie hawajawahi toa majibu yanayofanana., hospitali mojawapo iliniambia kuwa hawajaona chochote nikabaki kushangaa na kujouliza huyu physician yupo serious kweli!
 
Which hospital? Tuanzie hapo kwanza! Halafu waheshimu sana madokta, sawa? Isijekuwa umeenda kwa waganga sangoma, then unaleta stori nyingii.
Ujamuelewa mtoa mada au uelewa wako ni mashaka sana.
 
Sio udaktari tu nadhani sekta zote mambo hayako kama zamani na hii inatokana na kuangalia pesa kuliko vigezo vinavyotakiwa nenda muhas pale kuna watu wanasoma pale ila ufaulu wao haujakidhi vigezo vya kusomea udokta pesa yako tu ila ukienda kichwa kichwa unaambiwa hauna vigezo nadhani tatizo limeanzia hapo.
 
HONGERENI SANA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA.



Wapendwa wana JF habarini za asubuhi?,Kama kichwa kinavyojieleza,Wiki iliyopita nilikwenda Hospitali ya Rufaa ya nyanda za juu kusini-Mbeya kwa lengo la kufanya Check up ya mwili mzima kutokana na kutojisikia vizuri,Ikumbukwe kuwa hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kwenda ktk hospitali hiyo.
Baada ya kuwasili hospitalini hapo nilipokelewa vizuri sana nikawa naelekezwa vizuri sehemu ambazo napaswa kupita,baada ya vipimo niligundulika na tatizo ambalo ilikuwa lazima kufanyiwa Upasuaji.Basi Daktari alinipa maelekezo kuhusu tatizo nililonalo, kisha akaniuliza ikiwa nipo tayari kufanyiwa operation siku ya pili asubuhi,nami nikakubali.
Baada ya kukubali kufanyiwa operation,nikalazwa;Nami nikaomba kuwekwa Wodi ya Private Usiku wote wakati Nasubiria kufanyiwa operation Madaktari walinitembelea na kunichukua vipimo mbalimbali na kunifariji kuwa nisiwe na wasiwasi kuhusu operation hiyoe.Ilipofika saa kumi na moja Alfajiri niliamshwa na kuambiwa kuwa nijiandae kwaajili ya operation,nikajiandaa kwaajili ya operation nikaenda Theater.Madaktari walinifanyia Operation kwa upendo mwingi huku Manesi wakinibembeleza kwa sauti nyororo, baada ya operation nikaanza kusikia maumivu makali lkn nilifarijiwa sana kwa huduma nzuri za Wataalamu wetu wa Afya.Nilipoanza kijisikia vizuri niliruhisiwa kurudi nyumbani,hivi sasa naendelea vema,bado natumia dozi ya dawa nilizopewa.

Hitimisho.
Binafsi nimevutiwa na kufurahishwa sana na huduma za Hospitali hii,kuna wakati nilimuuliza mke wangu aliyekuwa ananiuguza,"Hivi hii ni hospitali ya Private au ya Serikali?",Jibu likawa ni ya Serikali,niliuliza hivyo kutokana na kushangazwa na huduma zao bora sana.Hebu fikiria Daktari aliuenifanyia operation alinipigia simu saa nne usiku kuniuliza ninaendeleaje? Na akasema kupitia Namba yake hiyo nimpigie simu muda wowote ikiwa Kuna shida inanipata.Kwa kweli sikuona mhudumu aliyenijibu Vibaya au kutonijali.Ilifika wakati nikawaza kuwa ningekuwa Rais wa nchi hii ningeamuru Mshahara wa Watumishi wa wizara ya Afya uongezwe.Hongereni sana Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya nyanda za juu kusini-Mbeya kwa Huduma yenu bora sana.Mwenyezi MUNGU awabariki sana.
 
Mods mnakera sana,sasa habari yangu kuhusu kuipongeza Hospitali ya Rufaa ya nyanda za juu kusini-Mbeya,inahusiana nini na Kushuka ufanisi wa Madaktari??.Dah mnakera sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…