Ufanyike uchunguzi kwa Wanafunzi wanaoandika matusi kwenye mitihani ya taifa

Ufanyike uchunguzi kwa Wanafunzi wanaoandika matusi kwenye mitihani ya taifa

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara - 51:
Inaleta ukakasi kwa mwanafunzi mdogo (kiumri) anayefanya mitihani ya taifa ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi kuandika matusi kwenye karatasi la majibu (Answer sheets).

Napendekeza ufanyike uchunguzi kwa wanafunzi ambao wanaandika matusi, huenda nyuma ya hii tabia kuna watu wazima wanawashawishi watoto kufanya hivyo ili watimize maovu yao kiurahisi.

CONNECT THE DOTS
Zifuatazo ni Dots nne (4) ambazo zinaweza kuleta uhusiano kati ya matukio yanayotokea - na hii tabia ya wanafunzi kuandika matusi kwenye mitihani ya taifa.

DOT 1: Matukio ya wazazi na walezi ambao wanaozesha (wanafungisha ndoa) watoto wao ambao bado ni wanafunzi.

DOT 2: Matukio ya kubakwa kwa watoto ambayo yanatokea maeneo mbalimbali nchini.

DOT 3: Matukio ya wanafunzi wa kike kupewa mimba, au kutoroshwa na vijana wahuni.

DOT 4: Matukio ya wanafunzi wa kiume kuacha shule kwa sababu mbalimbali ambazo zinasababishwa na wazazi/walezi/majirani, au watu wengine.

Hizo ni Dots nne (4) ambazo tukiziunganisha zinaweza kuleta uhusiano wa wanafunzi kuandika matusi kwenye mitihani ya taifa. Hivyo haipaswi kupuuzia, bali ufanyike uchunguzi ili endapo kama kuna watu nyuma yao wanashawishi watoto wajifelishe makusudi - wachukuliwe hatua za kisheria.​

Right Marker
Dar es salaam
 
Unafikiri wana andikaga hata matusi ya kihivyo basi. Inakuwaga kama hivi:

SWALI : RAIS WA KWANZA WA TANZANIA MWALIMU JULIUS NYERERE ALIFARIKI MWAKA GANI?

MWANAFUNZI: 👇👇👇👇👇

KAMUULIZE MAMA AKO YEYE NDIO ALIKUWEPO WAKATI NYERERE ANAISHI. UNANIULIZA MIMI NITAJUAJE WAKATI SIKUWEPO.
 
Aisee basi mimi nilijua wanaporomosha mitusi kama ya yule member mwenzetu kutoka Bunda.
 
Back
Top Bottom