Ufaransa ilijitoa NATO kwa amani, Urusi anashambulia nchi zinazotaka kujiunga

Ufaransa ilijitoa NATO kwa amani, Urusi anashambulia nchi zinazotaka kujiunga

Mbona ueleweki, France ni mwanachama wa NATO, wapi wamesema kajitoa?. NATO ina members 30. UK, US ,Canada, Ureno , Spain, Luxemburg, Italy, Germany , Slovenia, Zcheck, Hungary, Romenia,Birgalia, Lithiania, Estonia, Latvia, Norway, Sweden, Neither land, Belgium, Greece, Turkey, North Macedonia,Denmark, Poland, Romania,Albania, Croatia, Montenegro na Ireland. Kuna nchi 2 tu katika Ulaya ya magharibi neutral ambazo hazipo Nato lakini zimeomba kwa sasa ni Finland na Switzer land. Mashariki mwa Ulaya ambazo zimeomba ni (Ukrein, Moldava na Georgia) hizi zinasumbuliwa na Urusi. France ndie NATO Ulaya hawezi toka.
Ukiwafatilia hawa mkuu, utachanganyikiwa....
 
Daaah,we jamaa hata sisi Tanzania tuko Karibu zaidi na Urusi kuliko USA na Urusi!
Ninachosema,itakuwaje kama Russia ataunda umoja na mexico au Cuba ambao wamepakana na USA na kwenda kuweka huko Kambi za kijeshi na nyuklia weapons?Unadhani USA atakubali?
Hilo siwezi kulijibu manake halijatokea na hata likitokea linaweza kufikiwa muafaka kwa Round table discussion kuliko kwenda kuua Raia wasio na hatia wamama na watoto its like leo uwaulize Ukraine wapige kura wachague Block yao kati ya Soviet an Ulaya
Nahisi jibu unalo.
Mbona Poland ipo karibu na Mrusi na hakuna shida japo Mrusi anajitapa zamu yao inafwata.
 
Soma vizuri kaka nimesema Ufaransa ni Neutral state tunaita nchi zisizofungamana na upande wowote
Kwahyo Ukraine nae alitaka Kuwa neutral au?? Maana unazilinganisha Ukraine Na ufaransa
 
We una maswali ya kijinga sana, Je, wakati Marekani anazichagulia nchi za kiarabu marais na hata kuwaua hadharani akina Sadam, Gadafi na kushambulia kwa nia ya kumuondoa Assad wa Syria alipata baraka za nani? na kwa nini hulisemi hilo? au kwako Mmarekani kushambulia nchi huru na kuziharibu yeye ndio ana haki sana? wacheni mrusi atetee maslahi yake na mkae kimya kama mlivyokaa kimya siku Marekani wanamchomoa rais wa nchi huru ya Iraq kwenye shimo na kwenda kumnyonga hadharani bila hatia, tena nyamaza kabisa nyambaaf!!
thread closed
 
My friend wrong is wrong even if every body is wrong na kosa moja sio kosa la kuhalalisha uovu mwingine mwishoni nimesema sipendi vita yes Marekani alikua wrong je naye Putin afanye kisa Marekani alifanya tujifunze kuiga mazuri.

Leo anafanya Russia, Kesho anafanya China, kesho kutwa Korea kaskazini unadhani dunia itakua sehemu salama.

Wakati nchi za kiarabu zinavamiwa na viongozi wao kuuawa mbona mlikaa kimya!!! Au kwakuwa ni waarabu/waislamu!! Eti sasaiv ndio unasema hata marekani alikua wrong,,hapo nyuma ulikua wapi kutamka hili neno!!! baada ya mrusi kumvamia ukrein ndio mnatupigia kelele humu!! Tena kaa kimya kijana.
 
Hilo siwezi kulijibu manake halijatokea na hata likitokea linaweza kufikiwa muafaka kwa Round table discussion kuliko kwenda kuua Raia wasio na hatia wamama na watoto its like leo uwaulize Ukraine wapige kura wachague Block yao kati ya Soviet an Ulaya
Nahisi jibu unalo.
Mbona Poland ipo karibu na Mrusi na hakuna shida japo Mrusi anajitapa zamu yao inafwata.
Kaangalie ramani upya,Poland amepakana na Ukraine,Halafu Ukraine ndio kapakana na Russia!Russia ambacho hataki ni nchi NATO kujitanua Kwa kuingiza nchi wanazopakana by land,Russia anaona Hilo jambo kama hatari Kwa usalama wake!
Nimesema iliwahi kutokea huko nyuma na USA akawa tayari Kwa world war 3 iwapo meli za Kivita za Russia zingevuka line kuelekea Cuba!
Muwe mnaelewa,anachofanya Russia Kwa Ukraine kisingetokea kama Russia angesikilizwa Toka awali!Kwa miaka mingi amekuwa akiongea na Ukraine na nchi za NATO,amewaambia NATO wasiendelee kujitanua kuelekea East maana itakuwa kama maadui zake wanatengeneza umoja Kwa kumzunguka!
Hivi Leo Taiwan atake kujiunga NATO,China atakubali?
USA ni wakulaumiwa Moja Kwa Moja Kwa kinachatokea Ukraine!
 
Unakumbuka kuwa Mmarekani hataki Russia waweke vifaa vyake pale cuba
 
Ufaransa ilikuwa mwanachama wa NATO mpaka mwaka 1966 ilipoamua kujitoa na kubaki Neutral state huku wanachama wote wakibariki maamuzi hayo hatukuona Makombora ya Iskander yakivurumishwa Paris.

Kwa upande wa pili mambo ni kinyume kabisa nikimaanisha nchi zilizokua za Kisoviet ukitaka kutoka huko na kujiunga na NATO unakumbana na makombora ya Iksander ya kutosha tu.
Swali jepesi,
makubaliano yanasema ukitaka kujiunga NATO lazima Mrusi akushambulie? wamekubaliana hivyo?

Sweden na Finland ni neutral state ila wameanza tetesi za kutaka kujiunga NATO ila tiyari Mrusi keshawapa vitisho and good enough siku Sweden anatangaza mpango wake huo kuna ndege za Urusi kama sio mbili zilivunja sheria na kuruka anga la Sweden.

Swali Jepesi.
Kwanini Mrusi anawachagulia nchi huru maisha yao ya kuishi?

Kuna nchi baada ya kuonyesha mrengo wa kujiunga NATO au kinyume na Sera za Urusi zimekula makombora ya Iskander ya kutosha japo nyingine zilijiunga kibabe ref Georgia, Poland, Latvia, Chenchya, Romania, Hungary, etc zote hizo zina makovu ya makombora ya Iskander kutoka kwa Mrusi

Na leo hii wote ni mashuhuda angalia kinachoendelea Ukraine kila aina ya makombora yanatumika kutoka angani, baharini, nchi kavu kote huko zinatoka Iskander, Hypersonic, Vacuum, thermoballic Bomu...nk.

Swali jepesi.

Je Mrusi anaamini sana katika vita ndio njia ya kutafuta muafaka au ni Ubabe wake na kauli ya hakuna wa kunifanya kitu.

Vita niya kupingwa ni wapenda amani wote wanakufa watu wasio na hatia baada ya Vita ya Vietnam/Vietcong baada ya watu kushuhudima matokeo ya vita walikuja na kauli hii " VITA NI SULUHISHO LA MWISHO KABISA ENDAPO NJIA ZOTE ZA MAZUNGUMZO ZIMESHINDIKANA"

Kataa vita penda Amani.
Ufaransa siyo neutral state bali ni mwanachama hai wa NATO
 
Ndugu mleta mada, France ni active member wa NATO tangu kuanzishwa kwake. Iliwahi kujitoa mwaka 1966 katika masuala ya jeshi la pamoja pekee, ila ilirejea mwaka 2009.
 
Binafsi sioni mantiki ya kuhalalisha Uvamizi Wa Urusi kule Ukraine eti kwa vile Marekani walivamia nchi nyingine..

Ina maana Misri naye akiamua kuvurumisha mabomu Tanzania kwa madai ya kulinda maslahi yao tutakaa kimya pia?

Je Vita ndiyo njia sahihi ya kutafuta suluhu pindi tukikwazana?
Kama ukimfuatilia kwa makini, hii vita ina mkono usioonekana wa Mmarekani! Jaribu kutulia. Na pengine kabla hatujafika mbali, hapa hapa Africa tunazo nchi zilizovamiwa na vikundi vya wahuni kwa msaada wa mataifa ya Marekani na washirika wake ili tu watuibie malighafi zetu!!, unaonaje kama ungeanza kuyatetea mataifa yanayoonewa hapa Africa kama kweli una moyo wa huruma kihivyo!
 
utakuja kuelewa pale mke wako atapolala na panga na visuu
 
We una maswali ya kijinga sana, Je, wakati Marekani anazichagulia nchi za kiarabu marais na hata kuwaua hadharani akina Sadam, Gadafi na kushambulia kwa nia ya kumuondoa Assad wa Syria alipata baraka za nani? na kwa nini hulisemi hilo? au kwako Mmarekani kushambulia nchi huru na kuziharibu yeye ndio ana haki sana? wacheni mrusi atetee maslahi yake na mkae kimya kama mlivyokaa kimya siku Marekani wanamchomoa rais wa nchi huru ya Iraq kwenye shimo na kwenda kumnyonga hadharani bila hatia, tena nyamaza kabisa nyambaaf!!

Tahadhari, picha za kutisha!!

Nionyeshe wamarekani wakiwaua hadharani Gadaffi na Sadam
 
Ufaransa ilikuwa mwanachama wa NATO mpaka mwaka 1966 ilipoamua kujitoa na kubaki Neutral state huku wanachama wote wakibariki maamuzi hayo hatukuona Makombora ya Iskander yakivurumishwa Paris.

Kwa upande wa pili mambo ni kinyume kabisa nikimaanisha nchi zilizokua za Kisoviet ukitaka kutoka huko na kujiunga na NATO unakumbana na makombora ya Iksander ya kutosha tu.
Swali jepesi,
makubaliano yanasema ukitaka kujiunga NATO lazima Mrusi akushambulie? wamekubaliana hivyo?

Sweden na Finland ni neutral state ila wameanza tetesi za kutaka kujiunga NATO ila tiyari Mrusi keshawapa vitisho and good enough siku Sweden anatangaza mpango wake huo kuna ndege za Urusi kama sio mbili zilivunja sheria na kuruka anga la Sweden.

Swali Jepesi.
Kwanini Mrusi anawachagulia nchi huru maisha yao ya kuishi?

Kuna nchi baada ya kuonyesha mrengo wa kujiunga NATO au kinyume na Sera za Urusi zimekula makombora ya Iskander ya kutosha japo nyingine zilijiunga kibabe ref Georgia, Poland, Latvia, Chenchya, Romania, Hungary, etc zote hizo zina makovu ya makombora ya Iskander kutoka kwa Mrusi

Na leo hii wote ni mashuhuda angalia kinachoendelea Ukraine kila aina ya makombora yanatumika kutoka angani, baharini, nchi kavu kote huko zinatoka Iskander, Hypersonic, Vacuum, thermoballic Bomu...nk.

Swali jepesi.

Je Mrusi anaamini sana katika vita ndio njia ya kutafuta muafaka au ni Ubabe wake na kauli ya hakuna wa kunifanya kitu.

Vita niya kupingwa ni wapenda amani wote wanakufa watu wasio na hatia baada ya Vita ya Vietnam/Vietcong baada ya watu kushuhudima matokeo ya vita walikuja na kauli hii " VITA NI SULUHISHO LA MWISHO KABISA ENDAPO NJIA ZOTE ZA MAZUNGUMZO ZIMESHINDIKANA"

Kataa vita penda Amani.
mkuu sioni muunganiko wa hoja yako

Ufaransa kajitoa ulitakaje sasa ili iwe sawa na Ukraine kutaka kujiunga na NATO

Watu wanapaswa kujua hii ni vita baridi ya miaka nenda rudi kati ya USA na iliokua Urusi na baadae Russia ikarithi vita hiyo

Ndani ya makabrasha hatari ya CIA na FBI ni kutaka kuhakikisha Russia inapotea au kupoteza kabisa nguvu zake, ilifanikiwa kwa Gorbachev na sasa wanataka kuimaliza Russia ya Puttin

Russia nayo kwenye makabrasha yao ni kuhakikisha USA hawafanikiwi tena this time wanafanya kila linalo wezekana kuhakikisha halitokei

Usa wana nguvu na ushawishi mkubwa sana na wameishikilia UN na NATO na ndio maana ujinga wao mwingi wa kuvamia nchi yoyote inayo hatarisha maslahi yao inapata uungwajj mkono kimataifa kwa uongo mwingi kama kumvamia Sadam eti ana silaha hatarishi wakati hakua nazo
Russia alitaka kupeleka makombora yake cuba lakini usa walifanya kila njia kuhakikisha hilo halifanikiwi the same na anachofanya Russia kwa ukraine na nchi alizo zipiga mkwara

Ukiangalia kwa jicho la HAKI utabaki unajiuliza hayo maswali yako lakini ukiangalia kwa jicho la UHALISIA uliouliza sio maswali sababu yana majibu
 
Tahadhari, picha za kutisha!!

Nionyeshe wamarekani wakiwaua hadharani Gadaffi na Sadam

Mkuu kwa mantiki hii haya mambo ni makubwa sana kuliko upeo wa uwezo wa fikra zako
 
Ufaransa France ndo muasisi wa NATO alijitoaga kwenye mambo ya kijeshi tu hata hivo alirud 2009 sjui Kama niko sawa akarud kuwa active kwenye aspects zote so nazan n NATO
 
Kilaza huyo
Unayoyasema assume yangekua yanafanyika ndani ya nchi yako yani wewe na familia yako wote mfe kisa Taifa linatafuta ukubwa,, u can't be serious bro unasema hivyo kisa unashuhudia kwenye Tv omba yasikukute waulize wale Watz walikua Ukraine vita inafananaje watakwambia.
 
Ufaransa ipo ndani ya NATO, wewe mleta mada vipi?
Umesahau kuwa hata kumtoa Ghadafi NATO ilihusika na ufaransa alikuwa kimbelembele?
 
Back
Top Bottom