Ufaransa: Muswada unaozuia wazazi kuweka picha za watoto Mtandaoni wawasilishwa Bungeni

Ufaransa: Muswada unaozuia wazazi kuweka picha za watoto Mtandaoni wawasilishwa Bungeni

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
1,215
Reaction score
3,035
Wazazi nchini Ufaransa wanaweza kupigwa marufuku ku-post picha za Watoto wao kwenye mitandao ya kijamii iwapo muswada mpya uliowasilishwa wiki hii utapitishwa kuwa sheria.

Muswada huo utaipa Mahakama mamlaka ya kuwapiga marufuku Wazazi kuweka picha za Watoto wao mtandaoni ambapo wote wawili watawajibikia katika kusimamia haki za picha za Watoto wao huku uamuzi wowote wa kuzipost mtandaoni ukitakiwa kuzingatia umri wa Mtoto pamoja na kiwango cha ukomavu wake.

Sheria inayopendekezwa inakuja baada ya muamko wa wazazi wengi kupost picha za watoto wao mitandaoni jambo ambalo huitwa “sharenting” ikijumuisha moja ya jambo kuu linalo hatarisha haki za faragha za watoto, kulingana na taarifa ya maelezo ya mswada huo pia ilisema asilimia 50 ya picha zinazotumiwa kwenye majukwaa ya ponografia ya watoto hapo awali zilichukuliwa kupitia picha zilizopostiwa na wazazi wenyewe kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa Daily Mail, muswada huo bado unahitaji kupitishwa katika Bunge la Seneti ya Ufaransa kabla ya kusainiwa na kutangazwa na Rais kuwa sheria.
 
Sijawahi ona uungwana wa kuweka picha ya mtu mtandaoni bila ridhaa yake.

Mtoto naye ana haki, haki zake ziheshimiwe
 
Kutumia picha mitandaoni ni kosa, ila kuwafundisha watoto ushoga freshi tu.

Mabeberu wamevurugwa.
 
Back
Top Bottom