Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa habari nilizopata jioni ya leo kutoka vision FM ni kwamba wafaransa wamegundua tuba ya VVU na tayari watu 14 waishapona. Habari hii isije hararisha ngono zembe.
pole kumbe mnaumwa!!Tutapona muda si mrefu
Hakuna ugonjwa usiokua na dawa!pepopunda iliua 1/3 ya watu duniani lakini dawa ilikuja patikana
Nikiwa nimepumzika kwangu baada ya kazi nzito ndo nikasikia hiyo habari njema
Tatizo ya Ukimwi ni kuwa hao siyo wadudu ila VIRUS. Kuwaondoa Virus mwilini ni kasheshe.
Inabidi waje wagundue Anti Virus ambao wataingizwa mwilini na kuwashambulia.
Mfano ni ugonjwa wa KANSA ambao na wenyewe ni VIRUS. Juzijuzi wametibu mtu kwa kumwingizia Virus waliokuwa modified wa Ukimwi na jamaa akapona. Kilichotokea hapo ni kuwa hao Virus wa Ukimwi walikuwa kama ANTI VIRUS na wakawashambulia Virus wa Kansa na mtu akapona.
Labda wawabadili Virus wa Kanza na waanze kuwatumia kuwala Virus wa ukimwi?!?!?! Ngoja wataalamu wa IT na Uganga waje hapa watupe mwanga zaidi kwa hili.
Ila msianze ngono nzembe sasa maana kuna magonjwa mengine mengi tu yanauwa na hujui bei ya hiyo dawa itakuwaje.