Ufaransa yaipa Tanzania mkopo wa Tsh. Bilioni 361.7 kuzalisha umeme wa jua

Tunachukua mikopo mingine ambayo tija hata haionekani,,,,kuanza kutenga hela kwa ajili ya umeme wa jua kwa kweli ni suala la aibu achilia mbali kufikia hatua kuchukua mkopo kwa ajili ya hilo
 
Hizi pesa zitatafunwa tu,maana system ya wapigaji ndo imeshaanza kurudishwa kwenye system ,mdogomdogo.hakuna jipya tena.wazilete tu hizo wapigaji wakishagawana ,watawaajiri vijana wetu mtaani watakapoanza kujenga mijengo yao.
 
K
Tunachukua mikopo mingine ambayo tija hata haionekani,,,,kuanza kutenga hela kwa ajili ya umeme wa jua kwa kweli ni suala la aibu achilia mbali kufikia hatua kuchukua mkopo kwa ajili ya hilo
Kuna wanaofananisha mkopo wa SGR na mkopo wa kuzalisha umeme wa Jua. Hadi uchaguzi mkuu 2025 ndio ccm itatuletea tunayemuona anafaa Ila kwa sasa hali sio. Kila Kona mikopo mikopo mikopo mikopo.
 
Deni la Taifa linakwenda kufikia trilioni 100 by next week.
 
Waafrika tumelogwa na nani? Yaani mnakopa kwa ajili ya Umeme? Kwani hatuna Umeme? Viongozi kopeni kwa mambo serious unaona hata wakulima wanawashangaa mmechemka! Ningekuwa Mwenye mamlaka hiyo akieomba huo mkopo angekuwa Ndani na kulipa yeye mwenyewe binafsi siyo wananchi wa tz.
 
Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la Ufaransa (AFD), imeipatia Serikali ya Tanzania mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 361.7 kwa ajili ya kugharamia mradi wa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa jua.

Mkataba wa makubaliano ya msaada huo umesainiwa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Bw. Frederic Clavier Pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bi. Stepanie Mouen Essombe, kwa niaba ya Serikali ya Ufaransa.

Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa Mkataba huo, Bw. Tutuba alisema kuwa mkopo huo utatumika kujenga mitambo ya kuzalisha umeme-jua kiasi cha Megawatt 50 katika Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga.

“Ni matumiani yangu kwamba AFD wataridhia kutupatia fedha kwa ajili ya kutekeleza awamu ya pili ya mradi huo iliyopangwa kuzalisha Megawatt nyingine 100 ili kuweza kufikia kiwango cha uzalishaji kilichokusudiwa cha Megawatt 150”, alisisitiza Bw. Tutuba.

Alisema kuwa Shirika la Maendeleo la Ufaransa lilitoa pia msaada wa Euro milioni 7 kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa mradi ambao utatekelezwaji wake utaanza Mwezi Machi 2022 hadi Machi mwaka 2023.

Bw. Tutuba alisema kuwa faida za mradi huo utaongeza uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme na kuiwezesha TANESCO kutimiza malengo yake ya kuzalisha umeme kupitia vyanzo mbalimbali kupitia nishati jadidifu, utapunguza utegemezi wa umeme wa nguvu za maji na kuzalisha umeme wa ziada utakao tumika majira ya ukame.

“Sehemu ya mkopo uliosainiwa utatumika kufanya maboresha na kuimarisha Grid ya Taifa ili kuifanya ya kisasa ili kupunguza upotevu wa umeme” aliongeza Bw. Tutuba

Bw. Tutuba aliishukuru Serikali ya Ufaransa kwa kuipatia Serikali ya Tanzania mkopo huo kwani utasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika ambapo utachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Mkoa wa Shinyanga na maeneo mengine nchini.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Bw. Frederic Clavier, alisema kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuhakikisha Mpango wa Taifa wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26 unafikia malengo yake.

Mhe. Clavier alifafanua kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaifanya Tanzania kushika nafasi ya 2 kwa ukubwa Afrika Mashariki katika uzalishaji wa umeme wa nguvu ya jua na kuifanya TANESCO kuwa na umeme wa uhakika kutoka katika chanzo rafiki wa mazingira.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bi. Stephanie Mouen Essombe, alisema kuwa kati ya mwaka 2016 na 2020, Ufaransa imetoa zaidi ya Euro bilioni 6 kwa ajili ya Miradi ya Nishati sawa na shilingi za Tanzania trilioni 17 ambapo kati ya fedha hizo shilingi trilioni 2.8 zimetumika kwenye miradi ya umeme-jua.

Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo wa Umeme-Jua mkoani Shinyanga utaiwezesha TANESCO kuzuia zaidi ya tani 43,460 za hewa ya ukaa na kuchangia jitihada za Serikali ya Ufaransa za kuhifadhi mazingira duniani.

“Katika kipindi cha mwaka 2020, Ufaransa imetoa misaada na mikopo yenye thamani ya Euro milioni 330 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 932 na kwamba kusainiwa kwa kiasi kingine cha Euro milioni 130, kutaifanya jumla ya mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na Ufaransa kupitia shirika lake kufikia Euro 580 sawa na sh. Tril. 1.6.

Alisema kuwa mwaka huu, Shirika lake linaandaa mkakati ama mpango mpya wa namna ya kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo hifadhi ya mazingira na kilimo endelevu kwa upande wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, miradi ambayo imewasilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) Mhandisi Dkt. Titto Mwinuka, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, alisema kukamilika kwa mradi huo utachangia kufikia lengo la Taifa la upatikanaji wa umeme kufikia Megawatt 5,000 kufikia mwaka 2025.

Aliongeza kuwa mradi huo utasaidia kuwa na mchanganyiko wa vyanzo mbalimbali vya nishati kwa sababu lengo la Serikali ni kuwa na vyanzo vingi vya nishati ikiwemo maji, nyuklia na jua.

Dkt. Mwinuka aliahidi kusimamia kikamilifu mradi huo ili ikuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kufikia lengo lililokusudiwa.

View attachment 1815915
View attachment 1815916
Masharti ni yapi? Au free hiyo? Kweli?
 
Deni la Taifa limefikia trillion 71, Bado tunaenda kukopa fedha za kuzalisha umeme wa jua na kurekebidha grid ya Taifa? Hii awamu inaendeshwa na awamu ya nne.
Hatuwezi kuogopa kukopa kwaajili ya maendeleo kwa sababu tuna deni kubwa never..
 
good move. nishati ya uhakika ni chachu kwa maendeleo endelevu ya taifa letu
 
Sijaelewa huo mkopo unamashiko gani kwa taifa hivi hii serikali ya hawamu hii inatutakia mema kweli mbona mnatuuza kwa Bei ya jumla
 
Huo mkopo uchukueni, na kwakuwa tutaulipa basi wasitupangie cha kuufanyia, uende wote kwenye Rufiji hydropower.
 
Waafrika tumelogwa na nani? Yaani mnakopa kwa ajili ya Umeme? Kwani hatuna Umeme? Viongozi kopeni kwa mambo serious unaona hata wakulima wanawashangaa mmechemka! Ningekuwa Mwenye mamlaka hiyo akieomba huo mkopo angekuwa Ndani na kulipa yeye mwenyewe binafsi siyo wananchi wa tz.
Sindiyo hapo mkuu, yaani nchi ya pili kutoka chini tunafikiria maumeme
Ikibidi hizo hela zijenge kiwanda cha juisi ya mananasi watu tupate ujira
 
Back
Top Bottom