Ufaransa yapiga marufuku matumizi ya simu kwa watoto katika shule

Ufaransa yapiga marufuku matumizi ya simu kwa watoto katika shule

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,143
Reaction score
6,560
Ufaransa yapiga marufuku matumizi ya simu janja ' Smart Phones ', tablet na saa janja ' Smart Watches kwa watoto chini ya miaka 15 katika shule.

Serikali ya taifa imekuwa ikitilia shaka uwezo wa wanafunzi kwa maana ya kutegemea vifaa hivi katika masomo yao pia ikionekana kama chagizo la mmomonyoko wa maadili.

Hatua hii inatambuliwa kama “Sheria kwa karne ya 21”, sheria inayolenga kumuwezesha mtoto na kijana kutumia uwezo wake wa asili. Kupitia sheria hii inamtaka na kumlazimu mtoto chini ya miaka 15 kufika shule pasi ya simu janja, saa janja, tablet na vifaa vyenye uwezo wa kuchata mfano wa PSP na Nintendo Switch (Vishkwambi).

Aidha kupitia sheria hii mpya mtoto huyu hapaswi kuonekana mita 100 katika viunga vya shule na vifaa hivyo.

Sheria na taratibu hizi zinakuja kipindi ambacho kwa nyakati tofauti taifa la Ufaransa lilishuhudia ukuaji mkubwa wa watoto wa kike kuvunja ukimya wa kihisia na mtazamo dhidi ya watoto wa kiume kwa kuwashiwi Kwa kutumia jumbe fupi wawapo darasani.

Moja ya tukio la kukata na shoka ni lile mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 17 alipomshawishi kwa upendo ' Kutongoza ' mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 14 na kukutwa akimfanyia faragha shawishi kitaalamu ' Romance ' katika choo cha kike katika shule moja jijini Strasbourg.

Kwa upande wa wazazi, walezi na wadau wa elimu wameipokea sheria hii kwa mitazamo tofauti, wengi wao wakiona sheria hii kama moja ya kipangamizi kwa maendeleo ya teknolojia kwa watoto na ukuaji wa taifa.

Wengine wakidai simu ni muhimu kwa mtoto kuwa nayo maana inaweza tokea hali ya hatari kwa mtoto kama utekwaji, ulawiti, kubughudhiwa au ubakaji na mtoto kuomba msaada mara moja.

Huku wengine wakifurahishwa na hatua hii kwa kusema, wao hawakusoma kwa simu shuleni na maisha yaliendelea na kuona hatua hii kuwa yenye viwango vya usawa na kutunza maadili.

Pia wazazi/walezi wengi wikidai simu zilichochea kutosikilizwa kwa waalimu na wazazi na watoto wengi kijiingiza katika vitendo vya ajabu na kuyaishi maisha ya kimtandao.
 
Hili ni la kuipongeza Ufaransa...!! Katika mambo tunayotakiwa ku'copy' na ku'paste' ni hili. Mtoto under 15 years smartphone ya nini?...
 
Hili ni la kuipongeza Ufaransa...!! Katika mambo tunayotakiwa ku'copy' na ku'paste' ni hili. Mtoto under 15 years smartphone ya nini?...
Tucopy ili iweje mkuu wakati simu hadi 18 Africa...mcheki mdau alivyonijibu hapo juu yuko sahihi...
 
Hili ni la kuipongeza Ufaransa...!! Katika mambo tunayotakiwa ku'copy' na ku'paste' ni hili. Mtoto under 15 years smartphone ya nini?...
Sasa umesha ambiwa ni watoto bado ' asilimia kubwa ya maamuzi yao huamuliwa na mlipuko wa hisia kuliko mantiki so wakisha achwa watumiwe hivyo vifaa majority yao kubwa ni lazima itatumbukia katika mlipuko wa tabia hasi
 
Back
Top Bottom