Ufaulu wa darasa la nne, kidato cha pili na nne umepaishwa ili kuwafurahisha wapiga kura; ushahidi huu hapa


Wazee mna tabu Sana! Kwani Hakuna aliyefeli?
 
Ulishawahi kusikia mbunge mwenye degree anashindwa kuapa kwa kuwa hajui KUSOMA VIZURI, only in Bongo, mpe mtoto wa Form two kipande Cha gazeti asome, hawa waliosoma Saint Kayumba, utapata hofu moyoni
 
Kuna mengi yamebadilishwa, Nakumbuka wakati fulani, kusoma diploma ya Clinical officer ilihitajika angalau c c c lakini sasa d d d unaenda bila shida
 
Tanzania ni nchi ya kipumbavu sana. Wakati nchi nyingine za dunia zinapiga hatua mbele kielimu, sisi tunarudishwa nyuma na wanasiasa uchwara wenye matumbo mkubwa kama mapakacha yasiyojaa. Nchi hii imelaaniwa milele! 😳
 
Mimi naona huo wa 1997 ni rahisi kuliko 2017
 
Mimi naona huo wa 1997 ni rahisi kuliko 2017
Kivipi mkuu? Hebu fafanua kauli yako hii tata.

Huo mtihani wa 2017 hata ikiondolewa LIST B unaweza kujaza majibu na ukapata yote. Mtihani huu hata ukimpa mtoto wa darasa la 4 ukamuondolea LIST B ata score 100% bila shida.
 
Huu ufaulu wa kimchingo unaosababishwa na serikali sikivu ya CCM ndio unaopelekea baadhi ya shule kuiba mitihani. Ipo siku CCM wataipeleka kaburini elimu ya nchi hii kama tutaendelea kuwachekea.
 
Mfumo wa Elimu usiomwangalia mwalimu kama Focal person na Hurb ya kukufikisha unapotakea unadhani nini kitatokea?
Walimu wana hali mbaya madeni kama yote stahiki zao hawawezi usitegemee cha ziada kutokea
Hivi hujafuatilia vizur nchi zote zenye mifumo mizuri ya Elimu wanafanya nini kwa Walimu wao???
Sisi ngoja tukomae na siasa
 
Ukisema mitihani ni mirahisi kwa kisa tuu cha kuchagua majibu hapana.
Kwa sasa hutakuta swali la koja kwa moja...yaan 4654+946944=
Yote ni maelezo so kama hajui kusoma hata kusolve na hizo namba hataziona.
Tuweka majungu pembeni hakuna sababu ya kuongeza ufahulu ili uwafurahishe wananzengo....HAPANA
 
Unazungumzua ya mwaka huu au mwaka jana?
 
Sisiyemu tu hao.. hakuna mchawi mwingine...
Kataa ccm ndo mabadiliko yatakuja..
 
Lete mifano halisi mkuu
 
Tatizo ni Siasa kuingilia Wizara ya Elimu

Wanafunzi wengi 80% uwezo wao ni mdogo sana.
Hawa hawakutakiwa hata soma, ila serikali imewalazimisha kusoma na matokeo yake ndo haya tuyaonayo.

Wizara imekuja na Mkakati kuwa kila Rais aliyepo madarakani, mkoa wake au anapotokea usifeli.

Kushindanisha wanafunzi kunasababisha wanafunzi na waalimu kuiba mitihani.

Ukitaka jua wanafunzi ni vilaza, kaulize walimu wa vyuo vikuu
 
Umeongea ukweli kabisa. Asiyeamini akamatafute mhitimu wa darasa la saba amlinganishe na yule aliyemaliza fomu foo.......wa darasa la saba ana nafuu.

Nchi hi imefika hapa kwa sababu ya usikivu wa serikali makini ya CCM.
 
Wa nn hapo kuna vitu viwili
Toa mfano wa kitu komoja kimoja mkuu; wadau watakuelewa. Ndio maana hata mimi nimetoa mifano tofautitofauti kuepuka kuwachanganya watu.
 
Umeongea ukweli kabisa. Asiyeamini akamatafute mhitimu wa darasa la saba amlinganishe na yule aliyemaliza fomu foo.......wa darasa la saba ana nafuu.

Nchi hi imefika hapa kwa sababu ya usikivu wa serikali makini ya CCM.
Shule zinashindana kufaulisha, watoto wanakaririshwa mno. Wakifika chuoni inakuwa changamoto.

Mwisho wanakuja lalamika Tutors wanawaonea
 
Shule zinashindana kufaulisha, watoto wanakaririshwa mno. Wakifika chuoni inakuwa changamoto.

Mwisho wanakuja lalamika Tutors wanawaonea
Hili nalo neno mkuu. Lakini na tutors nao wanakaririsha pia; ni mwendo wa kukaririshana mwanzo, mwisho!
 
Hili nalo neno mkuu. Lakini na tutors nao wanakaririsha pia; ni mwendo wa kukaririshana mwanzo, mwisho!
Nao wamekaririshwa tokea shule za msingi.
Tukikosea shule za msingi tu basi

Elimu ya Tz ni biashara
Kuanzia Chekechea hadi Masters
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…