Ufaulu wa darasa la nne, kidato cha pili na nne umepaishwa ili kuwafurahisha wapiga kura; ushahidi huu hapa

Ufaulu wa darasa la nne, kidato cha pili na nne umepaishwa ili kuwafurahisha wapiga kura; ushahidi huu hapa

Huu ni mpango mahsusi uliopangwa kimkakati na serikali ya CCM ili kuwezesha kuzalishwa vilaza wengi zaidi kwa maslahi ya kuendelea kubaki madarakani. Mungu anawaona hawa wanaIsaya!
 
Tusisahau kuwa mwaka 2024 ni mwaka wa uchaguzi. Hivyo, serikali ya CCM inafanya kila juhudi matokeo yawe mazuri ili kuwafurahisha wapigakura. Na hii ndiyo sababu iliyopelekea waanzishe mitihani ya kubet tofauti na mitihani ya zamani ambayo mwanafunzi alitakiwa kukokotoa hesabu mwenyewe na pia kujaza majibu ya mitihani mingine yeye mwenyewe.

Mitihani ya kubet ni moja ya mikakati kabambe iliyoanzishwa na serikali ili kuwafaulisha wanafunzi kiubwete kwa misingi ya kisiasa pasipo kuangalia madhara kwa taifa kwa muda mfupi na mrefu.

Matokeo ya mwaka 2023 yametoka; mwendo ni uleule wa serikali kupika matokeo kwa sababu ya kuwahadaa wapigakura. Nchi ngumu sana hii.
 
Ukitaka kujua elimu imeshuka kutana na Hawa vijana waliomaliza chuo kikuu, wengi hawana uwezo wa kujenga hoja au kujielezea pia uwezo wao wa kuchanganua Mambo ni mdogo Sana
 
Watanzania tumerogwa; yaani tunafurahia matokeo feki huku elimu yetu ikizidi kushuka kila mwaka. Aliyeturoga kafa. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya matokeo ya darasa la nne (SFNA), kidato cha pili (FTNA) na kidato cha nne (CSEE) kutolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) hivi karibuni na kuonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia mbili (2%) ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2020.

Baada ya kufuatilia namna mitihani inavyotungwa na kusahihishwa kwa muda mrefu nimegundua kadri miaka inavyokwenda mbele mitihani inazidi kurahisishwa ili wanafunzi wengi zaidi wafaulu. Hii ni sera ya serikali kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kila mwaka ili wapate cha kusema mbele za wazazi (wapiga kura) kila baada ya miaka 5 ya uchaguzi.

Nikianzia kwenye suala la utunzi wa mitihani, siku hizi mitihani inatungwa kwa urahisi sana na kwa njia ya ajabu. Tangu serikali ilipoanzisha mitihani ya kubashiri (kubet) wanafunzi wengi wasiojua kusoma wala kuandika hufaulu kujiunga na shule za sekondari na wanaendelea hivyo hivyo hadi kidato cha nne.

View attachment 2085385
Wanafunzi hawa wakifika kidato cha nne, serikali tena hutunga mitihani rahisi ili wengi wao wafaulu kujiunga kiadato cha tano kwa ubwete. Utafiti wangu umeonesha kwamba kadri miaka inayoenda mbele mitihani ya kitaifa kwa ngazi zote imekuwa ikirahisishwa kwa makusudi ili kuwafaulisha wanafunzi kisiasa. Tazama mtihani wa Biology wa NECTA 1996 ulinganishe na mtihani wa NECTA 2017 utapata jibu mwenyewe. Zamani kupata divisheni wani halikuwa jambo la mchezo. Lakini kwa maswali mchekea kama haya (2017) hata mkulima ambaye hakwenda shule hakosi kupata divisheni wani!

NECTA 1996
View attachment 2095342

NECTA 2017
View attachment 2085333
Hali ni hiyo hiyo hadi kwenye mitihani ya kidato cha sita (ACSSE) ambapo wanafunzi vilaza hupenya hadi kuingia vyuo vikuu. Na huko vyuo vikuu, mchezo ni uleule…..kazi inaendelea. Tazama mtihani wa uliotungwa kwa wanafunzi wa mwaka wa pili kutoka chuo kikuu kimoja hapa nchini Tanzania. Hali inatisha kwa kweli.
View attachment 2085338
View attachment 2085340
Mtihani gani wa kijinga kama huu? Unampima nini mwanafunzi wa chuo kikuu kwa mtihani wa kizembe kama huu? Tuache masikhara jamani; huu mtihani hata ukimtungia mwanafunzi wa darasa la nne atapasua pasi na shaka. Sasa iweje wanafunzi wa chuo kikuu tunaowategemea kuja kulitumikia taifa baada ya kuhitimu watungiwe mtihani wa ovyo kama huu? Inasikitisha sana, ten asana.

Jambo jengine ambalo serikali imeamua kulifanya kwa makusudi ni kuondoa penalty kwa wanafunzi wanaofeli hesabu (Mathematics) tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma. Pia somo la Bible Knowledge siku hizi linajumlishwa kwenye ufaulu ili kuwaboost wanafunzi wengi zaidi wapate divisheni wani za magumashi kisiasa. Tazama kielelezo kifuatacho:

View attachment 2085344

Ndugu wadau wa elimu, sio mimi tu ninayelalamikia uchakachuaji wa elimu hapa nchini. Kila mtu ni shahidi juu ya uhuni unaoendelea katika kudidimiza kiwango cha elimu na kuwafanya watanzania wavivu wa kufikiri ili watawalike kirahisi. WanaJF wengine pia wamewahi kuguswa na jambo hili na kuliongelea kwenye nyuzi zifuatazo:

Wahadhiri vilaza huzalisha wasomi vilaza

Kwanini wahadhiri hawapelekwi tena kusoma 'postgraduate degrees' kwenye vyuo vyenye hadhi kubwa duniani kama ilivyokuwa zamani?

Nini kifanyike?
Nchi hii imefika mahali pabaya sana kielimu na endapo mchezo huu utaendelea, elimu ya nchi hii itaingia kaburini. Kumbuka kama tutakaa kimya, sisi na kizazi chetu chote tutaangamia pamwe! Je, nini kifanyike kurejesha elimu yetu kwenye reli? Karibu tujadiliane.​
Wakifaulu halafu wasiwe na ajira yanakuwa yaleyale. Kuruka majivu na
kisha kukanyaga moto!
 
Wakifaulu halafu wasiwe na ajira yanakuwa yaleyale. Kuruka majivu na
kisha kukanyaga moto!
Kwa kweli serikali imeamua kufanya jambo la kipumbavu sana ambalo halina tija yoyote kwa maendeleo ya taifa hili la kusadikika.
 
Ndugu wadau wa elimu, tunatengeneza kizazi cha ovyo sana. Baada ya miaka michache ijayo, taifa hili litakuwa na mijitu yenye uelewa mdogo kama mbegu ya hardali.
 
Wakifaulu halafu wasiwe na ajira yanakuwa yaleyale. Kuruka majivu na
kisha kukanyaga moto!
Sasa wewe unataka wawe vilaza wasipate hata maarifa ya kuwasaidia kupambana na mazingira yao? Unajua watu wengine mnakeera sana!
 
Ili elimu imsaidie mtoto, lazima msingi uwe imara.

Mtoto wa mwaka 0-7 kisaikolojia ndipo ugunduzi wa uwezo wake unapopatikana, ndipo mahali mwl. anapaswa kujifunza kwa mtoto, na sio mtoto kujifunza kwa mwl. Kwa Tz yetu na Afrika kwa ujumla ndio umri ambao mtoto akisikia habari na shule anachukia kwa nini? Shule imekuwa kama adhabu kwa mtoto, wakati ulipaswa kuwa wakati sasa wa mtoto kuitaka shule kila mara.

Kidogo shule binafsi zinajitahidi (sio wameweza hapana kidogo wanajitahidi).

Elimu inapaswa kutolewa na kumsaidia mhitimu aweze kukabiliana na maisha kwa ujumla wake. Elimu yetu sasa hivi ni kwa ajili ya ajira tu, wakati zama tulizopp ni changamoto na huko tuendapo ndio kabisa kunaogopesha.

Tujikite kwenye Elimu ya:-

1. Sanaa.
2. Biashara na ujasiriamali.
3. Kilimo

Hizi ndizo zitamkomboa Mtz. Kwa siku za usoni.

Wenzetu kumkuta mtu ana elimu yake kubwa lkn anakitumikia kipaji chake au yupo kwenye kilimo na masters yake ya biashara, ni mfugaji na ana phd ndani kawaida. Hawajalelewa katika hali ya kuona elimu ni kwa ajili ya kukaa ofisini.

Atakayekuja kufumua mitaala ya elimu,
Atakayekuja kurudisha nchi kwa wana nchi, huyo ataandikwa kwenye historia ya nchi hii kama Nyerere au kumpiku Nyerere pia.
 
Kweli kabisa. Hii elimu ya kubet ambayo watoto wetu wanafundishwa na CCM mashuleni haina tija hata kidogo.
 
Back
Top Bottom