Ufaulu wa darasa la nne, kidato cha pili na nne umepaishwa ili kuwafurahisha wapiga kura; ushahidi huu hapa

Huu ni mpango mahsusi uliopangwa kimkakati na serikali ya CCM ili kuwezesha kuzalishwa vilaza wengi zaidi kwa maslahi ya kuendelea kubaki madarakani. Mungu anawaona hawa wanaIsaya!
 
Tusisahau kuwa mwaka 2024 ni mwaka wa uchaguzi. Hivyo, serikali ya CCM inafanya kila juhudi matokeo yawe mazuri ili kuwafurahisha wapigakura. Na hii ndiyo sababu iliyopelekea waanzishe mitihani ya kubet tofauti na mitihani ya zamani ambayo mwanafunzi alitakiwa kukokotoa hesabu mwenyewe na pia kujaza majibu ya mitihani mingine yeye mwenyewe.

Mitihani ya kubet ni moja ya mikakati kabambe iliyoanzishwa na serikali ili kuwafaulisha wanafunzi kiubwete kwa misingi ya kisiasa pasipo kuangalia madhara kwa taifa kwa muda mfupi na mrefu.



 
Matokeo ya mwaka 2023 yametoka; mwendo ni uleule wa serikali kupika matokeo kwa sababu ya kuwahadaa wapigakura. Nchi ngumu sana hii.
 
Ukitaka kujua elimu imeshuka kutana na Hawa vijana waliomaliza chuo kikuu, wengi hawana uwezo wa kujenga hoja au kujielezea pia uwezo wao wa kuchanganua Mambo ni mdogo Sana
 
Wakifaulu halafu wasiwe na ajira yanakuwa yaleyale. Kuruka majivu na
kisha kukanyaga moto!
 
Wakifaulu halafu wasiwe na ajira yanakuwa yaleyale. Kuruka majivu na
kisha kukanyaga moto!
Kwa kweli serikali imeamua kufanya jambo la kipumbavu sana ambalo halina tija yoyote kwa maendeleo ya taifa hili la kusadikika.
 
Ndugu wadau wa elimu, tunatengeneza kizazi cha ovyo sana. Baada ya miaka michache ijayo, taifa hili litakuwa na mijitu yenye uelewa mdogo kama mbegu ya hardali.
 
Wakifaulu halafu wasiwe na ajira yanakuwa yaleyale. Kuruka majivu na
kisha kukanyaga moto!
Sasa wewe unataka wawe vilaza wasipate hata maarifa ya kuwasaidia kupambana na mazingira yao? Unajua watu wengine mnakeera sana!
 
Ili elimu imsaidie mtoto, lazima msingi uwe imara.

Mtoto wa mwaka 0-7 kisaikolojia ndipo ugunduzi wa uwezo wake unapopatikana, ndipo mahali mwl. anapaswa kujifunza kwa mtoto, na sio mtoto kujifunza kwa mwl. Kwa Tz yetu na Afrika kwa ujumla ndio umri ambao mtoto akisikia habari na shule anachukia kwa nini? Shule imekuwa kama adhabu kwa mtoto, wakati ulipaswa kuwa wakati sasa wa mtoto kuitaka shule kila mara.

Kidogo shule binafsi zinajitahidi (sio wameweza hapana kidogo wanajitahidi).

Elimu inapaswa kutolewa na kumsaidia mhitimu aweze kukabiliana na maisha kwa ujumla wake. Elimu yetu sasa hivi ni kwa ajili ya ajira tu, wakati zama tulizopp ni changamoto na huko tuendapo ndio kabisa kunaogopesha.

Tujikite kwenye Elimu ya:-

1. Sanaa.
2. Biashara na ujasiriamali.
3. Kilimo

Hizi ndizo zitamkomboa Mtz. Kwa siku za usoni.

Wenzetu kumkuta mtu ana elimu yake kubwa lkn anakitumikia kipaji chake au yupo kwenye kilimo na masters yake ya biashara, ni mfugaji na ana phd ndani kawaida. Hawajalelewa katika hali ya kuona elimu ni kwa ajili ya kukaa ofisini.

Atakayekuja kufumua mitaala ya elimu,
Atakayekuja kurudisha nchi kwa wana nchi, huyo ataandikwa kwenye historia ya nchi hii kama Nyerere au kumpiku Nyerere pia.
 
Kweli kabisa. Hii elimu ya kubet ambayo watoto wetu wanafundishwa na CCM mashuleni haina tija hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…