UFISADI: $350 million stolen from Tanzanians in Vodacom scandal

Wa jk , wa kingunge, wa Zakia meghji, hawajafikiwa zamu zao za kutajwa?
 
Kumbe huku ndo nguvu inapotokea,tutayajua mengi sana mwaka huu 2015
 
Vodacom ndio mtandao wa hovyo kuliko wote Tanzania watu wengi wanatumia kwa sababu ya Mpesa tu usingekuwa mpesa basi Vodacom ingebaki historia.
sijuim-pesa unayaizungumzia ni ipi.Juzi nimenunua umeme kwa m-pesa hadi leo tar 1 saa 13:14 sijapata token yoyote...nimewapigia jana usiku na leo asubuhi wanasema niendelee kuwa mvumilivu itakuja tuu,aisee voda siipendi sema tu hapa nilipo duka la airtel money ni moja tu na wanawahi kufunga otherise line yao hata kwa dharura kama hizo isingenikuta
 
aaahaa!sasa nimeelewa ndio maana lowassa anamwaga hela kumbe za kwetu.sasa zitto hapo ndo unanichanganya ,wakunyumba unamtamani lowassa kivipi.eti ohoo tangaza mali zako jiunge [act] zipo kwa watoto wake na ndunguze.unanunulika sana bro noma acha hizo umeshapata kama gari alishakupa mkono mb
 
Pesa zetu ndizo wanapewa maasikofu na mashehe na wanafunzi pale Dodoma!!!!
 
This country is fuc.ked from left, right and center. As a nation, where the heal are we heading to?
 
Dola za kimarekani milioni 350 sawa na shillingi za kitanzania bilioni 675 zimeibiwa kutoka kwa Watanzania
katika kashfa ya Vodacom

Imechapishwa tarehe 27 Aprili 2015
• Matajiri Tanil Somaiya na Rostam Aziz wanahushishwa katika kashfa hiyo.

• Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza amepokea rushwa ya dola za kimarekani milioni 5 ili
kuhifadhi siri.

• Kodi yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 121 milioni 500 imetoweka katika mpango huo.

•Taasisi za kiserikali TAKUKURU, TCRA, Mamlaka ya Mapato Tanzania hazikupata taarifa ya kashfa kubwa kuliko
EPA na Escrow pamoja.

Watanzania wameibiwa kitita cha dola za kimarekani milioni 350 (zaidi ya shilingi bilioni 675) katika kashfa kubwa
inayohusisha uuzaji wa vocha feki za kielektroniki za Vodacom Tanzania kwa wateja.
Kashfa, ambayo ni kubwa kuliko kashfa maarufu za Benki Kuu kuhusiana na malimbikizo ya malipo ya nje ya Tanzania
(EPA) na akaunti ya IPTL Tegeta ya escrow kwa pamoja, inahusisha Tanil Somaiya, mfanya biashara aliyejihususha na
mikataba kadhaa ya kutatanisha nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kashfa ya rada ya kijeshi na BAE Systems ya
Uingereza.

Uzalishaji wa vocha za kielektroniki unafuatia kusainiwa kwa mkataba kati ya Vodacom Tanzania na Shivacom Group
ya Tanil mwaka 2007/08. Hii ina maana kwamba Shivacom imeshiriki kama muuzaji mkuu wa Vodacom, mchapishaji
na msambazaji wa vocha za kielektroniki, katika mutadha wa migogoro dhahiri ya kimaslahi.

Katika kashfa hiyo iliyopangwa kitalam, kampuni ya Tanil, Shivacom Group, imechapisha mamilioni ya vocha ya
shilingi 500 (Jero Jero) kati ya 2008 na 2012 kwa kushirikiana na makampuni mengine yanayomilikiwa na Fred
Lowassa (Alphatel) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB Peter Noni (Planetel ) ili kusambaza
vocha nchini Tanzania.
B

Fred Lowassa ni mkurugenzi wa Alphatel, muuzaji Mkuu wa Vodacom, wakati Noni, aliyekuwa afisa mwandamizi wa
Benki kuu Tanzania (BoT), pia akimiliki kampuni nyingine ya uuzaji Mkuu wa Vodacom, Planetel.

Kwa pamoja, Shivacom ikishirikiana na Alphatel na Planetel wamefanya udanganyifu mkubwa katika uzalishaji,
usambazaji na uuzaji wa vocha haramu zenye thamani ya zaidi ya shillingi za kitanzania bilioni 675 bila Vodacom
kufahamu hadi kashfa ilipogundulika mwaka 2012.

Pia kulikuwa na ukwepaji mkubwa wa kodi katika kashfa hiyo pamoja na Ongezeko la Thamani (VAT) yenye thamani
ya zaidi ya shilingi bilioni 121 zilizokwapuliwa na Shivacom na washirika wake, jambo ambalo tafsiri yake ni kosa
kubwa la jinai.

Viongozi waandamizi katika vyombo vya seriakli ya Tanzania vya udhibiti na ukaguzi kama vile Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) walikuwa aidha wameshiriki katika kashfa hiyo au basi walikuwa hawakupata taarifa.
Shivacom pekee imesambaza zaidi ya nusu ya vocha feki, wakati vocha nyingine haramu zikisambazwa na washirika
wake - Alphatel na Planetel.

Vocha za "Jero Jero" ni vocha ambazo zinauzwa haraka nchini Tanzania, huku Shivacom ikichapisha mamia ya
mamilioni ya vocha feki kwa kutumia pini zilizotolewa na Vodacom Tanzania.

Kashfa hiyo si tu imeisababishia Vodacom Tanzania hasara ya fedha kubwa, lakini pia imesababisha kuwapotezea wateja
imani. Hii ni sababu moja wapo kwa Vodacom Tanzania kupoteza umaarufu katika sekta ya simu za mkononi nchini
Tanzania, wakati Airtel na Tigo sasa zikitishia kushindana kwa umbali zaidi katika soko la usambazaji wa kampuni hiyo.
Inaelezwa kwamba Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amegundua kashfa hiyo mara baada ya
kuwasili nchini Tanzania kutoka Kenya kuchukua nafasi ya mkurugenzi mkuu wa Vodacom Tanzania.

"Rene Meza amemkabili Tanil kuhusu kashfa na kudai dola za kimarekani milioni 10 ili kulinyazimsha hilo. Lakini
Tanil kwa kiburi amemjibu kwa kauli chafu, hivyo Rene ili kurudisha kisasi akaitisha bodi ya Vodacom na kuamuru
barua iandikwe kwa Shivacom kusitisha makubaliano na kwa uvunjaji wa mkataba, " imeelezwa na chanzo chetu.
"Tanil alisafiri kwenda kumuona Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Afrika Kusini -South Afrika's Group, Shameel,
aliyepewa rushwa ya dola za kimarekani laki nne. Hivyo basi, Shameel akatoa maagizo kwa Vodacom Tanzania kutatua
suala hilo na Shivacom. Hatimaye Rene Meza akatulia kwa kupewa rushwa ya dola za kimarekani milioni 5 kutoka kwa
Tanil na Vodacom kulazimishwa kumlipa Tanil fidia kubwa kwa kusitisha mkataba licha ya udanganyifu dhahiri. "
Mawakili wa Vodacom Tanzania walitoa ushauri wa kisheria kwamba mkataba lazima usitishwe, na lazima Shivacom
alipe fidia kwa Vodacom kwa udanganyifu. Hata hivyo, baada ya rushwa kadhaa, Shivacom kasitisha kulipa fidia na
Vodacom licha ya kuwa chanzo cha udanganyifu mkubwa.

Katika kashfa hii yote, Tanil amemtumia mwanasheria mwenye makazi yake mjini Dar es Salaam, Dilip Kesaria, kujibu
maswali ya kisheria kutoka Vodacom.

Awali, Kesaria alifutwa kazi nchini Uingereza kwa makosa mengine lakini kwa kutumia udanganyifu ameruhusiwa
kufanya kazi kama mwanasheria nchini Tanzania ambapo ndiye mkuu wa kitengo cha mawakili wa kampuni ya Kesaria
& Company.

Zifuatazo ni tarehe za matukio muhimu katika kujipatia kitita hicho cha shilingi bilioni 675 kwa udanganyifu kuhusiana
na uuzaji wa vocha za Vodacom Tanzania, maarufu kama Jero Jero:
Matukio na Takwimu

• 2008. Makubaliano ya miaka 10 yameanza kuwa na matokeo kwa ajili ya Shivacom Tanzania Limited ili kutoa vocha
za kielektroniki (EVD) kwa Vodacom Tanzania Limited. Hii ina maana kwamba Shivacom amekuwa na majukumu
mawili ikiwa ni pamija na kuwa muuzaji mkubwa wa Vodacom na msambazaji wa Vocha(EVD) kwa njia ya mikataba
tofauti.

• 2008-2012. Udanganyifu mkubwa uliotekelezwa na Shivacom kwa kipindi cha miaka mitano ni wa thamani ya zaidi
ya dola za kimarekani milioni 350 (sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 675), ambayo ni kubwa kuliko kashfa ya
Benki Kuu ya Tanzania EPA na Akaunti ya Tegeta Escrow pamoja. Udanganyifu huu ulifanywa na Shivacom katika
uchapishaji wa vocha feki za kielektroniki za shilingi 500 maarufu kama Jero Jero na kwa kuzisambaza katika soko bila
ya Vodacom kuwa na taarifa.

Wafanyabiashara washirika wengine wa Vodacom ni Alphatel na Planetel, wao pia wakihusishwa moja kwa moja na
ushirikiano na Shivacom kwa kusambaza vocha hizo haramu.

• Tarehe 31 mwezi Julai mwaka 2012. mwanasheria mkuu na Afisa mdhibiti wa Vodacom Tanzania Ltd ameiandikia
barua kampuni ya Shivacom Tanzania Ltd kuhusu usitishwaji wa mkataba huo. Hii imetokea baada ya Vodacom
Tanzania Ltd kugundua kwamba Shivacom amekuwa akifanya udanganyifu mkubwa katika kipindi cha miaka 5
(2008-2012) kwa kuchapisha na kusambaza vocha feki kwa kutumia namba za siri zinazotolewa na Vodacom. Barua
hiya kwa kweli imevunja mkataba wa vocha baina ya Vodacom Tanzania Ltd na Shivacom Ltd

• Tarehe 3 mwezi Agosti mwaka 2012. Shivacom alijibu barua ya Vodacom, akibishana kufuatia uamuzi wa kusitisha
mkataba wa vocha baada ya ushauri wa Kesaria.

• Tarehe 3 mwezi Septemba mwaka 2012. Mkurugenzi Mtendaji wa Shivacom Group, Tanil Somaiya, aliandika barua
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Group CEO nchini Afrika Kusini, Shameel Aziz Joosub, kuomba mkutano wa
kujadili kusitishwa kwa mkataba huo wa Vocha. Tanil alifanikiwa katika mkutano huo na Shameeel, ambaye ametoa
maagizo kwa Vodacom Tanzania kutatua suala hilo na Shivacom na kulipa fidia kwa kampuni yake kwa kusitisha
mkataba huo licha ya udanganyifu. Mkutano baina ya Tanil na Shameel na viongozi waandamizi wengine wa Vodacom
ulifanyika tarehe 1 mwezi Novemba mwaka 2012.

Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, alipokea rushwa ya dola za kimarekani milioni 5 kutoka kwa
Tanil Somaiya ili kutatua suala hilo.

• Tarehe 9 mwezi Novemba mwaka 2012. Tanil aliandika barua kwa Shameel, akisema kuwa alikuwa tayari kutoa
ushirikiano wake mkubwa kwa niaba ya Shivacom kwa ajili ya mauzo. Shivacom alitoa kwa Vodacom haki ya kwanza
ya kukataa kuomba ridhaa ya kuchunguza kwa karibu uwezekano wa kuwapata wanunuzi mbadala ikiwa Vodacom
haikuwa na nia ya kutoa dili hiyo.

• Tarehe 14 mwezi Novemba mwaka 2012. Mwanasheria mkuu na Afisa mdhibiti wa Vodacom Tanzania Ltd aliandika
barua kwa Shivacom kutoa fidia ya malipo kwa ajili ya kusitishwa kwa mkataba, licha ya ushauri wa kisheria
uliotolewa na wanasheria wa Vodacom kwa kampuni kusitisha mkataba na Shivacom, kutokana na ukweli kwamba
Shivacom amevunja mkataba kwa kutoa vocha feki za shilingi 500.

• Tarehe 29 mwezi Novemba mwaka 2012. Tanil aliandika barua kwa Shameel kukataa fidia ndogo ya Vodacom. Tanil
alidai fidia kubwa kutokana na hasara ya faida, gharama za vifaa na programu ya uzalishaji wa vocha pamoja na
gharama za malighafi ambazo azitatumika.

• 2012-2015. Vodacom wamekubaliana na Shivacom kwa kulipa kampuni dola za kimarekani milioni kadhaa za fidia
licha ya kuwa kampuni hiyo imefanya udanganyifu mkubwa. ITAENDELEA... HAYA SI MLIKUWA MNAISOMA JUUJUU HASA WENZANGU WALEEEE...LUGHA YENU HIYO HAPO..NASEMA HIVI HAYA HAYAKUBALIKI HATA KIDOGO.LAZIMA NISEME
 
Attachments

... wamefanya udanganyifu mkubwa katika uzalishaji,
usambazaji na uuzaji wa vocha haramu zenye thamani ya zaidi ya shillingi za kitanzania bilioni 675 bila Vodacom
kufahamu hadi kashfa ilipogundulika mwaka 2012.
Hivi leo ni tarehe ngapi?
 
Mi sijaelewa umerudia rudia sana na ku personalize hadi itaonekana una ajenda na watu fulani. Na pia kampuni ya kibiashara kulala usingizi na kuibiwa mkwanja mwingi hivyo lazima itakuwa haina Board of Directors
 
Dola za kimarekani milioni 350 sawa na shillingi za kitanzania bilioni 675 zimeibiwa kutoka kwa Watanzania
katika kashfa ya Vodacom
Imechapishwa tarehe 27 Aprili 2015
• Matajiri Tanil Somaiya na Rostam Aziz wanahushishwa katika kashfa hiyo.
• Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza amepokea rushwa ya dola za kimarekani milioni 5 ili
kuhifadhi siri.
• Kodi yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 121 milioni 500 imetoweka katika mpango huo.
•Taasisi za kiserikali TAKUKURU, TCRA, Mamlaka ya Mapato Tanzania hazikupata taarifa ya kashfa kubwa kuliko
EPA na Escrow pamoja.
Watanzania wameibiwa kitita cha dola za kimarekani milioni 350 (zaidi ya shilingi bilioni 675) katika kashfa kubwa
inayohusisha uuzaji wa vocha feki za kielektroniki za Vodacom Tanzania kwa wateja.
Kashfa, ambayo ni kubwa kuliko kashfa maarufu za Benki Kuu kuhusiana na malimbikizo ya malipo ya nje ya Tanzania
(EPA) na akaunti ya IPTL Tegeta ya escrow kwa pamoja, inahusisha Tanil Somaiya, mfanya biashara aliyejihususha na
mikataba kadhaa ya kutatanisha nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kashfa ya rada ya kijeshi na BAE Systems ya
Uingereza.
Uzalishaji wa vocha za kielektroniki unafuatia kusainiwa kwa mkataba kati ya Vodacom Tanzania na Shivacom Group
ya Tanil mwaka 2007/08. Hii ina maana kwamba Shivacom imeshiriki kama muuzaji mkuu wa Vodacom, mchapishaji
na msambazaji wa vocha za kielektroniki, katika mutadha wa migogoro dhahiri ya kimaslahi.
Katika kashfa hiyo iliyopangwa kitalama, kampuni ya Tanil, Shivacom Group, imechapisha mamilioni ya vocha ya
shilingi 500 (Jero Jero) kati ya 2008 na 2012 kwa kushirikiana na makampuni mengine yanayomilikiwa na Fred
Lowassa (Alphatel) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB Peter Noni (Planetel ) ili kusambaza
vocha nchini Tanzania.
B
Fred Lowassa ni mkurugenzi wa Alphatel, muuzaji Mkuu wa Vodacom, wakati Noni, aliyekuwa afisa mwandamizi wa
Benki kuu Tanzania (BoT), pia akimiliki kampuni nyingine ya uuzaji Mkuu wa Vodacom, Planetel.
Kwa pamoja, Shivacom ikishirikiana na Alphatel na Planetel wamefanya udanganyifu mkubwa katika uzalishaji,
usambazaji na uuzaji wa vocha haramu zenye thamani ya zaidi ya shillingi za kitanzania bilioni 675 bila Vodacom
kufahamu hadi kashfa ilipogundulika mwaka 2012.
Pia kulikuwa na ukwepaji mkubwa wa kodi katika kashfa hiyo pamoja na Ongezeko la Thamani (VAT) yenye thamani
ya zaidi ya shilingi bilioni 121 zilizokwapuliwa na Shivacom na washirika wake, jambo ambalo tafsiri yake ni kosa
kubwa la jinai.
Viongozi waandamizi katika vyombo vya seriakli ya Tanzania vya udhibiti na ukaguzi kama vile Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) walikuwa aidha wameshiriki katika kashfa hiyo au basi walikuwa hawakupata taarifa.
Shivacom pekee imesambaza zaidi ya nusu ya vocha feki, wakati vocha nyingine haramu zikisambazwa na washirika
wake - Alphatel na Planetel.
Vocha za "Jero Jero" ni vocha ambazo zinauzwa haraka nchini Tanzania, huku Shivacom ikichapisha mamia ya
mamilioni ya vocha feki kwa kutumia pini zilizotolewa na Vodacom Tanzania.
Kashfa hiyo si tu imeisababishia Vodacom Tanzania hasara ya fedha kubwa, lakini pia imesababisha kuwapotezea wateja
imani. Hii ni sababu moja wapo kwa Vodacom Tanzania kupoteza umaarufu katika sekta ya simu za mkononi nchini
Tanzania, wakati Airtel na Tigo sasa zikitishia kushindana kwa umbali zaidi katika soko la usambazaji wa kampuni hiyo.
Inaelezwa kwamba Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amegundua kashfa hiyo mara baada ya
kuwasili nchini Tanzania kutoka Kenya kuchukua nafasi ya mkurugenzi mkuu wa Vodacom Tanzania.
"Rene Meza amemkabili Tanil kuhusu kashfa na kudai dola za kimarekani milioni 10 ili kulinyazimsha hilo. Lakini
Tanil kwa kiburi amemjibu kwa kauli chafu, hivyo Rene ili kurudisha kisasi akaitisha bodi ya Vodacom na kuamuru
barua iandikwe kwa Shivacom kusitisha makubaliano na kwa uvunjaji wa mkataba, " imeelezwa na chanzo chetu.
"Tanil alisafiri kwenda kumuona Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Afrika Kusini -South Afrika's Group, Shameel,
aliyepewa rushwa ya dola za kimarekani laki nne. Hivyo basi, Shameel akatoa maagizo kwa Vodacom Tanzania kutatua
suala hilo na Shivacom. Hatimaye Rene Meza akatulia kwa kupewa rushwa ya dola za kimarekani milioni 5 kutoka kwa
Tanil na Vodacom kulazimishwa kumlipa Tanil fidia kubwa kwa kusitisha mkataba licha ya udanganyifu dhahiri. "
Mawakili wa Vodacom Tanzania walitoa ushauri wa kisheria kwamba mkataba lazima usitishwe, na lazima Shivacom
alipe fidia kwa Vodacom kwa udanganyifu. Hata hivyo, baada ya rushwa kadhaa, Shivacom kasitisha kulipa fidia na
Vodacom licha ya kuwa chanzo cha udanganyifu mkubwa.
Katika kashfa hii yote, Tanil amemtumia mwanasheria mwenye makazi yake mjini Dar es Salaam, Dilip Kesaria, kujibu
maswali ya kisheria kutoka Vodacom.
Awali, Kesaria alifutwa kazi nchini Uingereza kwa makosa mengine lakini kwa kutumia udanganyifu ameruhusiwa
kufanya kazi kama mwanasheria nchini Tanzania ambapo ndiye mkuu wa kitengo cha mawakili wa kampuni ya Kesaria
& Company.
Zifuatazo ni tarehe za matukio muhimu katika kujipatia kitita hicho cha shilingi bilioni 675 kwa udanganyifu kuhusiana
na uuzaji wa vocha za Vodacom Tanzania, maarufu kama Jero Jero:
Matukio na Takwimu
• 2008. Makubaliano ya miaka 10 yameanza kuwa na matokeo kwa ajili ya Shivacom Tanzania Limited ili kutoa vocha
za kielektroniki (EVD) kwa Vodacom Tanzania Limited. Hii ina maana kwamba Shivacom amekuwa na majukumu
mawili ikiwa ni pamija na kuwa muuzaji mkubwa wa Vodacom na msambazaji wa Vocha(EVD) kwa njia ya mikataba
tofauti.
• 2008-2012. Udanganyifu mkubwa uliotekelezwa na Shivacom kwa kipindi cha miaka mitano ni wa thamani ya zaidi
ya dola za kimarekani milioni 350 (sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 675), ambayo ni kubwa kuliko kashfa ya
Benki Kuu ya Tanzania EPA na Akaunti ya Tegeta Escrow pamoja. Udanganyifu huu ulifanywa na Shivacom katika
uchapishaji wa vocha feki za kielektroniki za shilingi 500 maarufu kama Jero Jero na kwa kuzisambaza katika soko bila
ya Vodacom kuwa na taarifa.
Wafanyabiashara washirika wengine wa Vodacom ni Alphatel na Planetel, wao pia wakihusishwa moja kwa moja na
ushirikiano na Shivacom kwa kusambaza vocha hizo haramu.
• Tarehe 31 mwezi Julai mwaka 2012. mwanasheria mkuu na Afisa mdhibiti wa Vodacom Tanzania Ltd ameiandikia
barua kampuni ya Shivacom Tanzania Ltd kuhusu usitishwaji wa mkataba huo. Hii imetokea baada ya Vodacom
Tanzania Ltd kugundua kwamba Shivacom amekuwa akifanya udanganyifu mkubwa katika kipindi cha miaka 5
(2008-2012) kwa kuchapisha na kusambaza vocha feki kwa kutumia namba za siri zinazotolewa na Vodacom. Barua
hiya kwa kweli imevunja mkataba wa vocha baina ya Vodacom Tanzania Ltd na Shivacom Ltd
• Tarehe 3 mwezi Agosti mwaka 2012. Shivacom alijibu barua ya Vodacom, akibishana kufuatia uamuzi wa kusitisha
mkataba wa vocha baada ya ushauri wa Kesaria.
• Tarehe 3 mwezi Septemba mwaka 2012. Mkurugenzi Mtendaji wa Shivacom Group, Tanil Somaiya, aliandika barua
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Group CEO nchini Afrika Kusini, Shameel Aziz Joosub, kuomba mkutano wa
kujadili kusitishwa kwa mkataba huo wa Vocha. Tanil alifanikiwa katika mkutano huo na Shameeel, ambaye ametoa
maagizo kwa Vodacom Tanzania kutatua suala hilo na Shivacom na kulipa fidia kwa kampuni yake kwa kusitisha
mkataba huo licha ya udanganyifu. Mkutano baina ya Tanil na Shameel na viongozi waandamizi wengine wa Vodacom
ulifanyika tarehe 1 mwezi Novemba mwaka 2012.
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, alipokea rushwa ya dola za kimarekani milioni 5 kutoka kwa
Tanil Somaiya ili kutatua suala hilo.
• Tarehe 9 mwezi Novemba mwaka 2012. Tanil aliandika barua kwa Shameel, akisema kuwa alikuwa tayari kutoa
ushirikiano wake mkubwa kwa niaba ya Shivacom kwa ajili ya mauzo. Shivacom alitoa kwa Vodacom haki ya kwanza
ya kukataa kuomba ridhaa ya kuchunguza kwa karibu uwezekano wa kuwapata wanunuzi mbadala ikiwa Vodacom
haikuwa na nia ya kutoa dili hiyo.
• Tarehe 14 mwezi Novemba mwaka 2012. Mwanasheria mkuu na Afisa mdhibiti wa Vodacom Tanzania Ltd aliandika
barua kwa Shivacom kutoa fidia ya malipo kwa ajili ya kusitishwa kwa mkataba, licha ya ushauri wa kisheria
uliotolewa na wanasheria wa Vodacom kwa kampuni kusitisha mkataba na Shivacom, kutokana na ukweli kwamba
Shivacom amevunja mkataba kwa kutoa vocha feki za shilingi 500.
• Tarehe 29 mwezi Novemba mwaka 2012. Tanil aliandika barua kwa Shameel kukataa fidia ndogo ya Vodacom. Tanil
alidai fidia kubwa kutokana na hasara ya faida, gharama za vifaa na programu ya uzalishaji wa vocha pamoja na
gharama za malighafi ambazo azitatumika.
• 2012-2015. Vodacom wamekubaliana na Shivacom kwa kulipa kampuni dola za kimarekani milioni kadhaa za fidia
licha ya kuwa kampuni hiyo imefanya udanganyifu mkubwa
 
Wenzako wameleta hoja hapo kuonyesha jinsi wizi ulivyofanyika,na katika article yote hiyo sijaona mahali CCM imetajwa.Kampuni zinazohusishwa na fraud ni zile ambazo si Rostam wala wenzake wanahusika.Kama Rostam ni shareholder wa vodacom ina maana kwa upande mmoja yeye ni mwathirika wa wizi huo maana wamemkosesha mapato.Ulisikia wapi mtu akajiibia mwenyewe?muda mwingine tuwe tunaufikirisha ubongo wetu kabla ya kukurupuka kuongelea vitu bila kutafakri.

Labda nikuulize katika hizo kampuni zilizotajwa,shivacom,planetel.Alphatel,wamiliki wake umewasoma hapo juu au umesoma juujuu tu?

Wee Panya...,
Yaani unakuja mbiiio hapa jamvini ..., hoja mbili tuu...
Kumlinda Lowassa na CCM...., basi..?!
Na unafikiri wenye akili timamu watakuamini...?!
Anyway.., endelea kumtumikia aliyekuajiri...
 
$350 MILLION (675 BILLION SHILLINGS) STOLEN FROM TANZANIANS IN VODACOM SCANDAL

Tycoons Tanil Somaiya & Rostam Aziz implicated in the scam

• Vodacom Tanzania MD Rene Meza receives $5 million bribe to keep silent

• Tax worth over 121.5 billion/- evaded in the deal

• PCCB, TCRA, TRA caught napping in massive fraud bigger than EPA and Escrow combined

A staggering $350 million (over 675 billion shillings) was stolen from Tanzanians in a massive scandal involving the sale of pirated electronic recharge vouchers from Vodacom Tanzania to customers.

https://255whistleblower.wordpress.com/2015/04/27/hello-world/

All these financial scandals are taking place with the blessings of Kikwete's government; the laws are not observed because senior government officials are involved in these criminal dealings. The laws that founded the Capital Markets Authority and the Dar es salaam Stock Exchange clearly stipulate the time frame within which these cellular phone companies should have been listed on the stock exchange but for criminal reasons the powers that be turn a blind eye to these laws!!

If Vodacom and the other cellular companies operating in Tanzania were listed on the Dar Es salaam Stock Exhange, they would have been mandated to put all their financial accounts open for public scrutiny and as such the chances of these CRIMINAL FRAUDS TAKING PLACE WOULD HAVE BEEN MINIMIZED. ONE BEGS THE QUESTION AS TO WHY THESE COMPANIES ARE NOT OBLIGATED TO BE LISTED? If SAFARICOM IS LISTED ON THE NAIROBI STOCK EXCHANGE why souldn't Vodacom,Airlel, and Tigo be listed on the Dar es salaam stock Exchange? The only plausible explanation is that Kikwete and his cronies are benefitting from these companies not being forced to lay bare their accounts hence fleecing the country of its much needed cash!!.
 
Hapo anayetafutwa na kuchafuliwa ni lowasa kisa,fred anamiliki alphatel ili mje mseme hizo ndo hela anazotumia lowasa kufanyia kampeni,jamani mbona mnamuandama mzee wa watu bila sababu,gwajima alishawaambia
inawezekana huo ndo ukweli hata kama ni ukweli mchungu kwa EL.
 
Katika Taifa la wagagagigikoko wajinga ndio waliwao. ....
 
wee panya...,
yaani unakuja mbiiio hapa jamvini ..., hoja mbili tuu...
Kumlinda lowassa na ccm...., basi..?!
Na unafikiri wenye akili timamu watakuamini...?!
Anyway.., endelea kumtumikia aliyekuajiri...

urt is my employer....na usiharibu majina ya watu please.....mimi sio panya,,im nakapanya
 
Back
Top Bottom