Abdalah Abdulrahman
JF-Expert Member
- Aug 29, 2019
- 222
- 202
Chadema imeendelea kuwathibitishia wanachama wake wachache waliobaki kuwa ni chama cha kundi dogo la watu wanaojali maslahi yao binafsi kuliko maslahi ya mtanzania mwingine yeyote.
Hii inathibitika katika zoezi lililomalizika la uchangiaji wa fedha kwa ajili ya faini za makosa waliyofanya viongozi hao kwa maslahi yao yaliyowatia hatiani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Mambo yafuatayo yanaonesha wazi ubadhirifu uliopo na unaoendelea juu ya michango hii ambayo inalenga kufaidisha kikundi hiki cha watu wachache ndani ya chama.
1.Matumizi ya Namba za Simu Binafsi
Tunafahamu kuwa michango ya chama au ya taasisi inapaswa kutumia simu yenye jina la ile taasisi au jina la lile tukio.Tulitegemea kwa kuwa kuna account na namba za chama ambazo zinatumika kila siku,zitumike kukusanya pesa hizi na zipelekwe mahakamani kuwatoa wanachama hawa.Lakini namba binafsi zimetumika makusudi kuficha ubadhirifu ambao unaendelea kufanyika wa kukwapua mali na fedha za wanachama ndani ya chama.Wapo wenye namba ambao wamesha anza kutoa hela wakidai hela hizo ni binafsi na sio hela za makusanyo ya faini za wanachama.Mkanganyiko huu unadhihirisha wazi kuwa kadiri zoezi linavyoendelea zipo pesa nyingi zitakazopigwa kwa staili hii.
2.Taarifa kuchelewa kuwafikia wanachama
Chadema imefanya makusudi kutumia mitandao ya kujamii kutangaza zoezi la uchangiaji kwa lengo kuwa taarifa za uchangiaji zitafika pole pole kwa wanachama wao na licha ya zoezi kuwa limefungwa,wapo wanachama watakao endelea kuchangia hizo fedha kwa kuchelewa kupata taarifa.Hivyo wale wanufaika wakawa wale wanachama pendwa wa chama ambao ni sehemu ya genge la wapigaji ndani ya chama.Wizi huu unasaidiwa na hoja ya kwanza ya matumizi ya namba za simu za watu binafsi kwa makusanyo ya fedha za kijamii.
3.Ukandamizaji wa Wanyonge
Viongozi wa Chadema wamekua wakipiga kelele kuwa hali ya uchumi ni ngumu,na watu hawana hela,wameenda mbali na kuzunguka katika nchi za wahisani kuzuia mikopo,kwa hoja za kutunga na zile za kutengeneza.
Tunajua mshahara wa Mbunge,tunafahamu marupurupu ya Mbunge,tunafahamu posho za vikao na pesa za jimbo,tunafahamu mali za kila mbunge na account zao nje ya nchi.Tunafahamu pesa iliyopo ndani ya chama,na pesa ambazo mabeberu wanachangia chama.Jiulize,hivi ni sawa kweli kumtaka mtanzania mnyonge mwenye hali mbaya kukopa kwenye tigo pesa au mtu maskini kuchangia kisa ulipe faini ya kosa ulilojitakia wakati una uwezo wa kulipa hiyo pesa?
Ni wazi tabia za mabeberu za alie nacho huongezewa zimekita ndani ya mioyo yao na kutokuwa na huruma kwa Watanzania.
4.Kutokuanisha michango mikubwa katika makusanyo
Taarifa zilizopo zinzonesha kuwa michango mikubwa inayotoka kwa wadhamini wa nje ya nchi wa chama cha Chadema imekua haiwekwi bayana kwani ni sehemu muhimu ya upigaji wa fedha.Michango hii inakadiriwa kuzidi kiwango kilichohitajika kwa ajili ya faini za viongozi hawa wa chama.
5.Kutumia tukio hili kama kitega uchumi
Ni wazi kuwa viongozi hawa wa Chadema walitenda kosa hili bila kujua uimara wa mahakama kwa awamu hii ya tano.Walidhania kuwa mahakama inaweza kuyumbishwa na wanasiasa,walidhani kuwa wanaweza kuwa juu ya sheria.Baada ya kugundua kuwa wanaweza kufungwa kama watanzania wengine waliamua kutumia tukio kisiasa na kupata huruma ya wananchi kupitia michango.
6.Utakatishaji Fedha
Kuna kila dalili ya jinai ya utakatishaji katika zoezi zima la ukusanyaji wa michango,hii inatokana na zoezi lilivyoendeshwa na usiri uliopo kwenye makusanyo.Pili kuna wanachama wengi wa chadema waliokuwa wakijihusisha na madawa ya kulevya ambao wamepata kichaka cha kuhalalisha pesa zao.
7.Hofu ya kuchunguzwa matumizi
Watanzania wote wanajua wazi kuwa Raisi wetu anaupendo mkubwa na watanzania wote,licha ya kuwa yeye ni kiongozi wa chama tawala lakini pia husaidia vyama vingine pale inapobidi.Kwa kuwa Rais ni ndugu wa Peter Msigwa alifuatwa na familia na kuchangia kiasi cha 38m ili Msigwa na wanachama wengine watoke.
Taarifa za ndani zinaonesha kuwa hela aliyotoa ilitakiwa ingie kwenye kapu ambalo halina hesabu akakataa kutokana na wasiwasi wa mchakato mzima.Sote tunamjua Raisi Magufuli pesa yake hailiwi kizembe,aliamua kulipa hela na kuhakikisha Peter Msigwa anatoka.
Ushauri,serikali kupitia taasisi zake za usalama zinatakiwa zichunguze chama hiki kufahamu mapato na matumizi ya michango hii.Pia ni jukumu la wanachama kuhoji juu ya matumizi ya namba za simu binafsi na kiwango kilichochangwa. Vinginevyo kikundi cha watu wachache kitaendelea kuhujumu nchi kupitia wanachama.