Ufisadi Mkubwa Ndani ya Adventist Tanzania Union Mission-Unaofanywa na Ndg Denis Wairaha

Ufisadi Mkubwa Ndani ya Adventist Tanzania Union Mission-Unaofanywa na Ndg Denis Wairaha

Mleta mada anaonekana kuwa na hasira hivi. Je inawezekana kweli ana uchungu na huo anaouita ufisadi au kuna la zaidi ya hapo? Nashawishika kuamini kuna zaidi ya kuchukia ufisadi ndio maana uzi wake uko kishari zaidi.&nbsp;<br>Pole sana kama jamaa alikuzidi akili.
 
Ikumbukwe ndg Denis wairaha kabla hajawa mhazini Tanzania union.. alikua akifanya kazi NBC bank pale samora branch near Jay mall... samora avenue......... so mali zake zinaweza zikawa na skurce from his previous job at NBC ,mikopo.. bse aliacha kazi so pension na vitu kama hivyo.... ila zaidi ya yote kama still kuna doubts fuata taratibu zinazo takiwa as in church au serikalini.
PCCB Act inatoa mandate kwa Takukuru kudemand informatikn from any person watakae muhisii.. juu ya jinsi alivyozipata mali zake.. taratibu zipo wazii zifuate...
 
Mimi nalifahamu kanisa la wasabato kuliko mtoa mada kwanza jinsi system ilivyo HAIWEZEKANI mtu akaiba 600m bila kushirikiana na askofu. Pili kanisa halina mapato hayo ya kuiba, tatu Denia haachi kazi, nne hakuna Denia anachoweza kufanya bila kamati kuridhia, tano ukaguzi umefanyika hapo muda si mrefu

Mleta mada ni mhuni na mfitini tu na inaonekana ana Chiki binafsi, anatakiwa kupuuzwa na kuzomewa. Kanisa la wasabato ni imara na ufisadi huo hauwezekani
 
Na tena basi ingelikuwa ni vyema kama angeweka wazi vipato vyake ili kuondoa ugubi ugubi huu.

Dah aisee wewe jamaa unasikitisha sana, angalia tu usije kuugua kichaa! Yani unataka akuelezee vyanzo vyake vya mapato wewe ukiwa kama nani?? Yani unamshangaa mwenzio anamili kumiliki daladala tano?? We hujui mjini hapa kuna watu wahudumu tu kempisk pale na wabamiliki majumba mitaani huku na wanatupangisha mpaka sisi ‘wasomi'!! Mjini mipango kaka, utakufa masikini na wivu wako wa kike.!
 
Dah aisee wewe jamaa unasikitisha sana, angalia tu usije kuugua kichaa! Yani unataka akuelezee vyanzo vyake vya mapato wewe ukiwa kama nani?? Yani unamshangaa mwenzio anamili kumiliki daladala tano?? We hujui mjini hapa kuna watu wahudumu tu kempisk pale na wabamiliki majumba mitaani huku na wanatupangisha mpaka sisi &#8216;wasomi'!! Mjini mipango kaka, utakufa masikini na wivu wako wa kike.!

huyu jamaa huenda ana frustration ya maisha, kuna uwezekano umri wake umeenda sana na akiangalia hajafanya chochote mpaka sasa! anahitaji ushauri.
 
Fimbo ya mungu ni kubwa,Ameandaliwa jeneza mbinguni
 
Nilimuomba mleta mada alete data Zaidi ili tuweze kumsaidiaila naona bado hajaweza kufanya hivyo. Naomba nichangie yafuatayo. Kwenyemchango wangu napenda kusema kuwa simhukumu wala kumtetea mhazini ilaninachangia tu ninachofikiria, naweza nisiwe sahihi.
Kuhusu swala la kununua viwanja/kiwanja Dar cha ekari tisakumbe ni ekari tano inakuwa vigumu kukusaidia kujua ukweli kama hujataja nikiwanja/viwanja vipi. Kuna utaratibu wa kununua viwanja vya kanisa na kwa walewanaofahamu Union ilikuwa na mwanasheria aliyekuwa anashughulukia paperwork yamanunuzi ya assets kama hizo. Lazima kuna mashahidi kwenye ununuzi ni vigumukusema umenunua ekari tisa kumbe ni tano. Kama mtoa haja akitutajia kiwanja/viwanjavyenyewe tutamsaidia kumtafutia ukweli lakini kwa sasa maelezo yakehayajitoshelezi.

Kwa swala la ajira, siku za nyumba katibu alikuwa na mamlakaya kushughulikia human resources sana ila ili kutenganisha kazi yake kamamchungaji na muajiri, Union iliweka mwanasheria aliyekuwa anashughulikia hizoajira. Kwa sasa amestaafu ila mhazini sio anayetoa uamuzi khusu ajira. Piaikumbukwe kuwa kazi ya kanisa si ya pato la juu kwa kweli ni ya kujitolea – ni kaziya wito. Upendeleo wa wakurya unaosema sijauona labda utoe mifano (hauhitajikutaja watu, taja nafasi tu kadhaa ili tuone kama tunaweza kukusaidia kujibu).Upendeleo wa wapare unaousema ninavyoona ni irrelevant. Kama unavyofahamu kwaTanzania kanisa hii lilianzia upareni na wapare ni wengi sana kama washiriki,sitashangaa kuona kuwa wapare wako overrepresented kwenye watumishi pia. Istand to be corrected. Wamisionari walianzisha mission ukuryani (Kubumaye)iliyoelimisha wakurya na nyingine Ikizu iliyosomesha watu wa kanda ya ziwawengi kwa hiyo utaona watu wanaotokea huko wengi kwenye ajira za kanisa. Lakinibado wakurya sio wengi sana (hawako overrepresented) kwenye ajira ya kanisa.Ikumbukwe kuwa mhazini sio muajiri na kiongozi wa sasa wa union is very strong,sio mtu wa kumpindisha.

Kuhusu kuiba hela mil 600, kuna member ameshachangia hapa.Ni vigumu sana kwa pato la kanisa. Kumbuka hiyo ni hela nyingi kupotea kwenyesystem bila kusababisha budget shock kwenye institutions ndogo na not-forprofit kama hili kanisa.

Kuhusu kununua shamba la milioni 600 huko Nduruma, hayo nimambo ya familimia ni vigumu mimi kukusaidia kujua ukweli. Kwanza hujui gharamaza shamba umekadiria. Pili hujui kama alikuwa na shamba au viwanja vinginealivyonunua zamani kutokana na ajira yake ya zamani ambavyo ameuza ili kulipiahilo au kama amechukua mkopo. Kumbuka watanzania bado tuna familia kubwa kwamfano mimi sina hizo fedha ila baadhi ya members wa familia wanaweza kutakakuwekeza Arusha na mimi kama nikiwashauri tukusanye nguvu na kununua hapaitaonekana kuwa ni la kwangu kumbe ni ushirikiano wa wanafamilia. Again,sidhani naweza kukusaidia sana hapa.
Kuhusu swala la mhazini kutokuwa creative kutafuta miradi yakuisaidia kanisa, unless kama focus ya kanisa imebadilika, kanisa lina focus zaidikwenye utumishi and service kuliko entrepreneurship. Kuna investments ambazokanisa inafanya lakini si kwa niya ya kuliendesha kanisa kwa mapato ya miradihiyo. Kama unalifahamu kanisa vizuri miradi ipo kwenye institutions ndogo kamashule na vyuo kama mashamba, mifugo, mashine za kusaga, na kadhalika, ila sikwa ngazi ya juu. Miaka kadhaa iliyopita kanisa liliitisha thinktank kufikiriakama linaweza kuwa na uwekezaji kama kwaa mfano kumekuwa na majadiliano yakujenga kituo cha kukodisha kufanya semina na kadhalika, hususaani sehemu yaKanisa road, yaani kuvunja zile nyumba za kanisa ambazo ni za zamani sana. Kwasasa miradi sio priority ya mapato na kanisa linategemea zaidi utoaji kuendeshashughuli zake za kila siku.


Kuhusu swala la daladala tano hilo pia siwezi kumsaidia mtoamada kwa sababu sifahami mfumo wake wa biashara. Labda mleta mada aatuelezezilinunuliwa zote kwa pamoja au ilinunuliwa moja halafu ikazaa nyingine. Again,ni vigumu kujua kama kuna uhusuano na hela za kanisa kwa hiyo sina chakuchangia zaidi. Kama ni vipanya, wachungaji siku hizi hata wa mitaani wanamagari mazuri nan a gharama kuliko bei ya kipanya. Kuna mikopo mingi tuinatolewa kwa ajili ya manunuzi ya magari kama una collateral. Kumbuka pia kuwamleta mada anaweza kuwa ameambiwa kuhusu hizo daladala kumbe hamna lolote au niza ndugu yake/zake huyo mhazini.

Last but not least, ningemshauri mtoa mada atumie lugha yabusara. Kumuita mwenzako kwa mfano nanukuu, “ Ni bora ukutane na mchawi usiku kuliko kukutana na denisWairaha mchana.” sio ustaarabu ni jazba ambazo ni vigumu kwako kuwaobjective. Nikukumbushe kuwa sisi binadamu sio perfect kama kuna matatizounayaona ukifuatilia na kutoa malalamiko yako kufuata utaratibu unaoelewekautasaidiwa kujua ukweli na kama mhazini ana matatizo wahusika watayatatua.Nimalizie kwa kusema kuwa mimi simtetei huyo mhazini. Nimeshawahi kukutana nayemara moja tu nikiwa likizo Arusha na hata akiniona haweza kunikumbuka ilanimeona niwe objective kuchangia hoja.
Asanteni.

 
Kwenye post yangu ya juu kuna makosa badala ya Kanisa road ni uzunguni Arusha, nafikiri mtaa unaitwa Haile Selaise ila sikumbuki vizuri. Nimejaribu ku edit ila inakataa ku save changes. Asante.
 
Hahahaah hii Siredi ikenkata mbavu...mkuu povu limekutoka,,,...kanshtaki kwa papa joni paulo
 
peleka ushahidi wako ndani ya taasisi huku sio mahala pake mtumishi
 
Ok, mashtaka nimeyasikia hana adabu huyu. Sasa je, torati inasemaje juu ya kokap la namna hii? Tukate mkono au mguu?
 
Umenena vyema mkuu Udassa99...

Barikiwa!
 
Last edited by a moderator:
Habari Wana JamiiForum na Wasabato wote Tanzania!

Kwa neema yake Mungu naomba tushirikiane na kuwaza kwa pamoja kama wakristo wano heshimu neno la Mungu kuhusiana na ubadhirifu wa unaofanywa na Mweka Hazina wa Adventist Tanzania Union Mission Ndugu Denis Wairaha.

Ndugu Denisi Wairaha, ndani ya miaka mitatu ya utumishi wake kama mweka hazina amefanikiwa kupata utajiri wa kupindukia wakati watumishi na waumini wa kanisa wakiendelea kuishi katika maisha duni. Kiongozi huyu ametumia muda wake mwingi kuchumia tumbo na si kuibua miradi itakayo leta ufanisi katika shughuli na kazi za kanisa.

Kwa mfano, ndani ya kipindi hicho kifupi, Denis Wairaha amefanikiwa kununua shamba kubwa la ekari 40 lenye thamani isiyopungua TZS 600,000,000/- milioni mia sita sawa na US$ 375,000/- lililopo Arusha maeneo ya Nduruma. Si kwamba hatupendi yeye kufanya ununuzi huu, LA HASHA! kwani ni kwa manufaa yake binafsi na familia yake, pia kama mtanzania ana kila haki ya kufanya maendeleo yake binafis, LAKINI, swali la kujiuliza, Kipatao chake kama mweka hazina kinamwezesha kufanya manunuzi hayo bila ya kuwa na njia za giza na rushwa? Katika kipindi hicho mpaka sasa Denisi Wairaha anapokea mshahara usiozidi TZS 700,000/- sawa na US$ 438/-

Vilevile, ndugu Denis Wairaha, amefadhiliwa na kanisa kujiendeleza kielimu katika level ya Masters ili kuongeza ufanisi katika kazi, lakini cha kushangaza baada tu ya kumaliza elimu hiyo ameamua kufanya uamuzi wa kuacha kazi. Hii inamaanisha kuwa, amelidanganya kanisa na wauumini wake au/na kutapeli pesa/sadaka za waumini kwa malengo yake binafsi yanayoshabiiana na hulka ya ubinafsi.

Pia, mtajwa hapo juu anamiliki daladala tano zilizopo katika jiji la Dar es Salaam.

Akiwa bado anaongozwa na pepo la kujimbikizia mali kwa manufaa yake binafsi na familia yake huku akiwa amejivika joho la kondoo mtakatifu wa bwana, mnamo mwaka 2013, ndugu Denis Wairaha chini ya mamlaka yake alifanya malipo ya Plot za kanisa zenye ukubwa wa ekari 9 jijini Dar es Salaam. Waumini na kanisa kwa ujumla tukaendelea kuaminishwa kuwa tuna ekari 9 Dar es Salaam kumbe SIVYO. Imekuja kugundulika kuwa ekari zilizo nunuliwa ni 5 TU na si 9.

Swali la kumuuliza ndugu yetu Denis Wairaha, ziko wapi ekari zingine 4? zilizogharamiwa na fedha/sadaka za waumini wa kanisa?

Pia Denis Wairaha amekuwa akihusishwa na kulalamikiwa mara kwa mara kwa kushiriki moja kwa moja katika kushawishi na kutoa ajira katika mazingira ya ukabila..yaani amekuwa akipendelea sana kuajiri watu wanotoka katika kabila lake la Wakurya na wakati mwingine kutokana na mazingira ya kazi yake na his God fathers amekuwa pia akitoa upendeleo kwa watu wa kabila la Wapare. Ukimuona machoni kama mtu lakini ndani ya moyo wake amejaa visasi, chuki, fitina na ubinafsi.

Ni bora ukutane na mchawi usiku kuliko kukutana na denis Wairaha mchana.

Maoni: Ninaelewa mfumo wa kulindana uliopo ndani ya kanisa letu, lakini ningependa kupendekeza kuwa Ndugu Denis Wairaha achunguzwe kabla ya kuacha kazi rasmi. Tupo tayari kutoa ushahidi usiopingika kuhusiana na maswala yote tajwa hapo juu.

Na kwa kuwa yeye, ambaye miaka nenda rudi amekuwa akijikweza na kujifananisha na kondoo safi kuliko wote, namuomba aje atoe ufafanuzi wa yote haya na/au kukanusha kwa uthibitisho.


Nawasilisha
"Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwone, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikia wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru" (Mathayo 18:15-17)

Huo ndio mwongozo wa namna Wakristo wanavyotakiwa kushughulika na wenzao. Ndugu "Msabato Mwema" umekwenda kinyume na agizo la Bwana na ninakushauri umwombe radhi mhusika na kutubu mbele za Mungu kwa kutangaza jambo la mtu kwa watu wasiohusika na hivyo kusababisha wengine kutenda dhambi pasipokusudia.
 
Mnafki mkubwa huyu Msabato Mwema amejawa roho ya wivu, yaani angekuwa mchawi angeshamroga huyo jamaa. We kalia kupiga domo tu wenzako wanashughulisha vichwa!

Mkuu hata maandiko yanasema wazi kwamba pale Sadaka zako zitakapo kuwepo ndipo Moyo wako utakapo kuwepo sasa huyu anaanza kudai matumizi kwani yeye ni "MUNGU'.Unapotoa sadaka unazitoa kwa Mungu hauzitoi kwa Binadamu hivyo iwapo yeyote ataiba au kutumia vinginevyo atakuwa ana mwibia Mungu na siyo wanadamu.AKA SOME KITABU CHOTE CHA MALAKI.Hata Yuda Iskariot ndiye aliyetunza fuko la fedha "hazina" alipokuwa na YESU lakini mpaka siku anamsaliti hakuwahi kutoa hesabu za matumizi ya mafungu yaliyokuwemo katika mfuko ule.

Unapotoa sadaka unamtolea Mungu na ndiye anayefuatilia Matoleo husika Kumbuka Mungu alimtuma Malaika kumwambia Cornelius KATIKA KITABU CHA MATENDO YA MITUME KWAMBA sadaka zako zimefika mbele ya MUNGU.Nina wasiwasi mleta uzi siyo mshirika mzuri wa Kanisa lake na watu wanamna hii huwa ni mabingwa wa kumpelekea Mungu chenji chenji baada ya kumaliza mahitaji na matamanio ya mioyo yao.

Kama anadhani klunajambo lianalofayika kinyume cha Taratibu walizojiwekea basi atoe taarifa kwa Muajiri Mkuu (MUNGU) kwa njia ya Maombi ili Mungu amkemee na si vinginevyo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom