Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Aisee, nani angeweza kujua kuwa ndani ya CHADEMA kuna ujambazi wa kutisha wa fedha za wanachama na wananchi. Hiki kinyang'anyiro cha kugombea uenyekiti wa chama umeibua mambo mazito na kukianika wazi hiki chama kuwa ndani yake kuna mijizi kwelikweli.
Leo katika press conference ya Lema, aliyekuwa mjumbe wa Technical team ya chama aliyehusika kusajili namba ya chama iliyotumika kwa ajili ya kukusanyia pesa za Join the Chain, akijibu swali la mwandishi wa habari ameuhabarisha umma kuwa kulikuwa na namba nyingine ambayo wananchi walipewa wachangie lakini namba hiyo siyo ya chama na haijulikani ni ya nani.
Bwana huyo akasema kuwa namba rasmi ya chama ilikuwa ni 0744446969 ambayo mzungumzaji aliisajili yeye kwa niaba ya chama na alama za vidole ni za kwake, na hii namba ilisajiliwa pindi viongozi wa CHADEMA wamefungwa na wakawa wanatafuta namna ya kuwatoa. Lakini cha ajabu zilitengenezwa vest za kuhimiza watu kuchangia kupitia "join the chain" zenye namba ambayo "kiujanja" ni tofauti na hiyo yaani 0744444969.
Akasema kuwa yeye binafsi haijui namba hiyo nyingine, na akawaomba waandishi wamuulize katibu Mkuu wa CHADEAM aeleze hiyo namba nyingine ilikujajekujaje kwenye kukusanya michango.
Hili suala zima la Join the Chain mwanzoni lilianza vizuri sana likiwa na lengo la kukifanya chama kiweze kujiendesha lakini tangu Mbowe alivyotoka gerezani, zoezi likahujumiwa na hata mapato na matumizi ya hilo zoezi yalikuwa hayatolewi wazi mpaka jana Mnyika alivyoeleza pesa zilizopatikana.
Kabla ya Mnyika kuzielezea hizo pesa bwana Wenje alidai eti hizo pesa zilikuwa zinakusanywa na akina Lissu na Lema ili kumpindua Mbowe kitu ambacho Mnyika alikipinga kwa ufafanuzi wake wa jana. Hata hivyo maswali bado yangalipo katika ishu nzima ya pesa za join the Chain hasa kuhusiana na namba hiyo feki ya kukusanyia pesa