Ufisadi wa Sabaya: Mwenge wakataa mradi aliosimamia, Mabaunsa wake walikuwa Wajumbe wa Kamati

Ufisadi wa Sabaya: Mwenge wakataa mradi aliosimamia, Mabaunsa wake walikuwa Wajumbe wa Kamati

Una andikaje UZI mkubwa kama huu wa shutuma nzito bila hata kaushahidi either kapicha au ka video ?
 
20210612_082411.jpg
 
Duh kumbe sabaya alikuwa mhasibu wa miradi na mwenyekiti na muweka hazina duh mavyeo kama yote!
 
K
Mkuu, ukijibishana na Mtu, akaanza kusema, “hata Wewe!” Mara hata nyie mtakufa, hata nyie ni mafisadi, ni ishara ya kufilisika hoja! #pushgang wameishiwa vibaya sana, wanapigwa kotekote bila Huruma!
Kitendo cha kutumia neno 'hata'ni kuhalalisha dhambi kwa dhambi nyngine ambapo hakikubaliki kisheria pia
 
With my naked eyes nmeona gar tatu kwake hapo juz baada ya muda wakatoka jamaa wawil shombeshombe wako na m earphones,muda kidogo jamaa katolewa nje kapandshwa kwny gar wakaondoka nae,ila nlishangaa Hamdun kasema hawajamshikilia
Yeah for public interest lazima waseme hivyo kwanza...! Unachukuliwa unahojiwa kisha unapigwa search ya kibabe, halafu wanalinganisha findings za search, utetezi wako na tuhuma zinazokukabili

Wakishajiridhisha kuna kesi ya/za kujibu wanakukamata officially sasa! Lakini ukamataji wake unakuwa tofauti kidogo, umma unaweza kuambiwa kuwa ni kwa ajili tu ya mahojiano na kutaka ufafanuzi wa masuala fulani, lakini ndio inakuwa imetoka iyo
Kifuatacho ni mahakamani na baadhi ya kesi ni
Matumizi mabaya ya ofisi
Uhujumu uchumi
Rushwa
Mauaji
Nyingi ya hizo tuhuma HAZINA DHAMANA!
 
Mkuu, ukijibishana na Mtu, akaanza kusema, “hata Wewe!” Mara hata nyie mtakufa, hata nyie ni mafisadi, ni ishara ya kufilisika hoja! #pushgang wameishiwa vibaya sana, wanapigwa kotekote bila Huruma!
Wamepigwa mbele na nyuma
 
Ifike mahala Viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru wapewe Uhuru wa kuhoji,kukamata na kufungulia mashitaka yeyote anayehujumu miradi ya maendeleo hata kama tayari alikwisha tuhumiwa na makosa mengine.
Hapo ndipo tutakapowaenzi Waasisi wetu kwa kutuchia tochi yenye Mwanga mkali.
Ni aibu kwa viongozi wa mbio za Mwenge kufika sehemu za uzinduzi na kukuta kuna uhuni na ubadhirifu mkubwa wa mradi, huko ni kuupoteza muda na kuvunja Heshima ya Mwenge wa Uhuru.
Ingelikuwa ni enzi zile za 1970-1983's kuna mtu leo angelikuwa kizuizini.
 
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Luteni Josephine Mwambashi amekataa kuweka Jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Afya kilichopo wilayani Hai kwa madai kuwa ujenzi wa kituo hicho umegubikwa na rushwa. Awali katika hotuba ya ufunguzi ilielezwa kwamba aliyekua mkuu wa wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya ndiye aliunda kamati ya kukusanya fedha kutoka kwa wadau mbalimbali ili kufanikisha ujenzi wa kituo hicho.

Sabaya aliviagiza vyama vya ushirika wilayani Hai vichangie jumala ya TZS 600M ambapo katika hatua ya awali viliweza kuchangia TZS 338M na kuahidi kuendelea kuchanga kadri ujenzi unavyoendelea. Wadau wengine wakiwemo wafanyabiashara na wawekezaji walichangia jumla ya TZS 169M.

Sabaya aliunda kamati ya fedha ambayo ilimjumuisha yeye kama Mwenyekiti, mabaunsa wake wawili kama wajumbe, na watu wengine wawili ambao si watumishi wa umma. Kamati hiyo ndiyo iliyohusika na kutoa pesa kwenye akaunti ya ujenzi wa kituo hicho. Hii ni kinyume na sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 ambayo inataka pawepo na watumishi wa umma katika kamati hiyo.

Hadi sasa zaidi ya 369M zimeshatumika lakini hakuna maandishi yoyote yanayoonesha fedha zilitokaje bank na zilitumikaje. Pia hakuna nyaraka yoyote inayoonesha "signatories" wa kutoa fedha hizo kati ya wajumbe watano wa kamati hiyo.

Hata vyama vya ushirika ambavyo ni wadau wakubwa katika mradi huo hawakushirikishwa kwenye kamati ya fedha ili kujua fedha zao zimetumikaje. "Waliambiwa wachangie na walipomaliza kuchangia, hawakuhusishwa kwenye kamati iliyoratibu ujenzi, hivyo hawajui fedha walizochangia zimetumikaje" amesema Luteni Mwambashi.

Kufuatia hali hiyo, Kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa, ameagiza ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro wafanye uchunguzi, ili kama kuna ubadhirifu watu wote waliohusika wapewe haki yao ya kikatiba.!

Credit: Malisa GJ

My Take
Wafuasi mna kazi kubwa ya kutetea jizi
Wafuasi wala hatuhangaiki na utunzi wa Malisa.

Tunahangaika na kutekeleza ilani ya CCM sssa
 
Back
Top Bottom