Ufuatao ni 'Mjumuisho' wangu wa 'Kiuchambuzi' baada ya kuiona Simba SC jana katika 'Simba Day' yao

Hapa uliandika ukiwa umetulia Sana..Good analysis

Genta siku akiacha kuranduka anaandika point Sana,ila kuna siku anaamka na vibe la "kwani wewe Unasemaje sasa?"
 
Aisee kumbe mwanamke unajua fabo namna hii...sii tukuoe simba queens
 
Popoma huyu mzungu ndie alikufanya ukaanza kupayuka kama chizi wiki iliyopita, leo unamsifia kama katuni, jifunze kufunga mdomo wako.

Unasema.....!!!!!

Ngoja aone hiki ulichokiandika.
 
Mnafiki huyo
Yaani Genta ni mnafiki siyo! Kwa hiyo ndiyo kusema juzi kati tu hapa alikuwa anawatishia viongozi wake kumsajili Manzoki, badala ya huyo Mzungu!

Halafu leo baada ya Mzungu kucheza kwa dakika chache tu; tayari kamsahau Manzoki, na pongezi na sifa zote anazipeleka kwa Mzungu yule yule aliyemponda hapo kabla!
 
Oeee
Hajitambui huyo
 
Kuna maeneo sikubaliani na wewe
 
Nahisi week hii kina tangazo.....kanoute anauzwa au mkopo....manzoki anaingia
 
Hujawahi kuniangusha Kwa uchambuzi ulioshiba. Lakini kuna Mtu umemuacha na Mimi ni shabiki wake mkubwa lakini Jana kaniangusha vibaya. Victor Akpan. Huyu jamaa ana nguvu na akili za wastani, ana mwili unaotosha Kwa vurugu za dimba la chini lakini namuona kama ameathiriwa na maneno ya Kocha kumkataa wakati amesajiliwa juzi tu. Anatakiwa kujua anachezea timu kubwa na pia ni mchezaji wa kulipwa (professional). Kiwango alichoonyesha Jana bado ana kazi kubwa ya kuwaonyesha mashabiki na walimu wake kwamba anafaa kuwa hapo vinginevyo ajiandae Kwa mkopo January 2023.
Kuhusu Inonga uko sahihi. Humu huwa tunabaki wawili tu tunaomsema maana wengine wakipenda hata chongo wataita kengeza. Varane wa Bongo ana tatizo mahali, anapenda Sana sifa kama Wahaya (samàhani), Angeacha Tabia ya kucheza na jukwaa msimu huu tungekuwa tumemsikia anatafutwa Ulaya kufanya majaribio.
Israel bado ndugu, nadhani Israel mtoa roho anamvuta ili amtoe Simba. Wakati mwingine makocha Wana mawazo binafsi na macho ya pekee, lakini Kwa macho ya kawaida inashangaza Duchu kuwa Geita Gold na Israel kuwa Simba.
Kuhusu Kanoute ha ha ha ha! Kijana yule anapewa nafasi ambayo yeye analazimisha awepo ili aguse mpira mara nyingi awe star. Kanoute hawezi kusukuma timu, apewe winga ya kulia awe backup ya Mtu mwingine katika mfumo wa 4-3-3.
Kuna Wachezaji wawili toka Zambia wameingia Tanzania mwaka huu, Phiri na Kambole. Hawa jamaa saikolojia Yao nadhani ilikuwa kwenda Ulaya wakashitukia wameangukia Afrika Tanzania.
Okrah ni Sakho wa Mwanzo aliyetaka kuachwa na Simba mwaka Jana. Kwa bahati mbaya hawajui Watanzania, mashabiki wa Simba hawana tofauti na Wa Manchester Utd atazodolewa aombe kuondoka. Ni mzuri lakini asiharakishe kutafuta ufalme.
Okwa ameijua njia, Hana makuu na hajui kama anashangiliwa au anazomewa yeye Yuko kazini.
Muzamiru na Mkude Mungu aendelee kuwapambania, Kwa Umri wao Jana wamefanya vema.
Chama asante Kwa Utulivu, lakini ni kama mwili na roho vinaongea lugha tofauti. Asante kocha Kwa kumfanya kuwa sub.

MZUNGU WAKO SASA;
Yule jamaa mpira anaujua, tena anaujua vizuri tu Ila usiniambie Hakuna striker kama yeye hapana. Kwa mastriker walioko Sokoni anaifaa Simba. Tatizo lake anacheza Afrika huku akitaka kuendelea kuwa Mzungu. Siku huyu Bwana atakapopangwa hakikisha nyuma yake yupo Chama. Vinginevyo alitakiwa apate Mtu kama Saidoo nyuma yake.
 
Kocha big NO
Akpan big NO
Kuhusu kocha nadhani Jana aliruhusu Kila mchezaji aonyeshe kipaji na si mafundisho. Lakini kama ndo mfumo wake basi aanze upya maana Wachezaji hawakumuelewa kabisa matokeo yake kipindi cha pili kocha alikuwa Clotius Chota Chama.
Akpan mtampenda akijua kilichompekeka. Bado Nina Imani naye, lakini akiendelea hivi atafanya watu walionicheka nilipompendekeza yeye badala ya Calvin Nashon wanizodoe zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…