Ufugaii Nguruwe vs ufugaji Kuku

Ufugaii Nguruwe vs ufugaji Kuku

Kingine zipo mbegu za nguruwe wakisasa hazina asili ya mafuta hivyo hupelekea nyama kuwa nyingi zaidi ukilinganisha na wakienyeji.

Nakupa mfano wa rafiki yangu juzi amechinja nguruwe wakisasa wenye umri miezi7 na katika wote waliochinjwa nguruwe alietoa kilo chache ametoa 50kg lakini waliobaki wametoa 60kg-70kg jambo ambalo kwa nguruwe wakienyeji hio haiwezikani.

Najilinganisha na Mimi mwenye nguruwe wa miezi 6 licha ya matunzo mazuri lakini wanawastani wa 34kg na kumbuka Chakula walichokula ni kiwango sawa na nguruwe wakisasa.

Hivyo majibu mepesi ni kwamba upo umuhumu wakutumia mbegu za kisasa kwenye ufugaji ili kuongeza tija zaidi.
Aisee..
Hao wasio na mafuta mengi ndo mpango mzima sasa!
 
The more unainvest capital the more u gain profit
Ok,
Kwanza ipo tofauti kiuwekezaji kwenye fugo hizi mbili,kuku itakutaka pesa kidogo kuwekeza ili walau upate kipato lakini nguruwe itakutaka uwekeze pesa nyingi ili walau uone faida.

Mfano kinda mmoja wa Nguruwe wakienyeji anaanzia 50000 na pure breed wanauza kinda kuanzia 200,000.

Ukilinganisha kifaranga wa kuku chotara anauzwa 1400,wamayai 2500,broiler anarange 1000-1500.
Hivyo tutakubaliana kwamba kwenye kuku panahitaji kiwango kidogo cha pesa cha uwekezaji ukilinganisha na nguruwe.

Kama utaanza na nguruwe wachache itakuhitaji muda mrefu kuanza kuona faida ya ufugaji.
Chukua mfano wa mimi nina wastani wa matetea 200 wa chotara ambao ninapata 400000-500000 faida kwa mwezi kwa kuuza mayai.

Nimeanza kufaga nguruwe sasa ni kama mwezi hivi hivyo bado sina maarifa yakukupatia kwakua bado ni mchanga,hata hivyo wanaenda vizuri,nguruwe nilioanza nao ni local breed ambao Mungu akipenda nitahamia kwenye pure breed ili nipate matokeo zaidi.
All in all kufuga ni kuzuri.
 
Kwa sasa pure breeds na hybrid zinaonekana kua na faida zaidi ya kuchinja mfano mtoto aliechishwa anauzwa kuanzia laki 2 nakuendelea ukiangalia kwenye chakula anakua ametumia kiwango kidogo sana mpaka kufikia hapo zaidi ya kunyonya kwa mama kwa maoni yangu ukiwa breeder utapata pesa zaidi.
Maelezo mazuri sana.
Ninafuga nguruwe pia, nimefuga hawa crossed(sio locals sio pure)

Nahitaji kujifunza, unahisi nikitaka kufuga hizi pure breeds nikilenga wapi hasa patanilipa.

Kuwa breeder au kwaajili ya nyama, ukizingatia bei ya pure breed pamoja na gharama ya kuwatunza ili niweze kufikia matunda yao vyema kabisa..
 
Kwa sasa pure breeds na hybrid zinaonekana kua na faida zaidi ya kuchinja mfano mtoto aliechishwa anauzwa kuanzia laki 2 nakuendelea ukiangalia kwenye chakula anakua ametumia kiwango kidogo sana mpaka kufikia hapo zaidi ya kunyonya kwa mama kwa maoni yangu ukiwa breeder utapata pesa zaidi.
Ahsante sana
 
Ndio Nani huyo?

Huyo aliyekupatia jinsia yako ya kike, mbona huelewi??.

Kuna maswali ya aina mbili ambayo watu wanachanganya; mfano mtu anapouliza wewe ni nani na wewe jina lako nani, hayo ni maswali mawili tofauti na hivyo yanakuwa na majibu tofauti.
 
Tatizo wewe unamjua alietoa jinsia Mimi simjui...ndo nataka uniambie Ni Nani huyo
 
Tatizo wewe unamjua alietoa jinsia Mimi simjui...ndo nataka uniambie Ni Nani huyo

Tatizo wewe unashindwa kuuliza unachokihitaji, unapouliza; "Ni nani ??"---- hapo unataka kujua Wasifu wa mtu, kiumbe nk, sasa mimi nakupa Wasifu wa huyo unayetaka kumjua, Yeye pamoja na sifa zingine alizonazo sifa mojawapo aliyonayo ni kutupatia sisi viumbe wake jinsia zetu kwani hakuna mtu au kiumbe hai yeyote anaweza kudai kwamba alijichagulia jinsia yeye mwenyewe.

Kama unataka kujua jina lake Yeye anaitwa Mwenyezi Mungu (The Almighty God).

Jina lake:----Mwenyezi Mungu.
Ni nani:- ---- Yeye ndiye aliyekuchagulia kisha akakupa jinsia jinsia uliyonayo na pia akakupa akili ambayo kwa ujinga wa nafsi yako unatumia akili hiyo kumkana Yeye.
 
Kwani wapi Nimemkana??
Mi nataka nimjue.
Haya....jinsia anachaguaje?
 
Back
Top Bottom