Ufugaji na kilimo unalipa sana

Ufugaji na kilimo unalipa sana

MalafyaleP

Senior Member
Joined
May 23, 2013
Posts
187
Reaction score
387
Wana JF,

Nimeona mm pia nitoe testimonial kwa faida ya wajasiriamali wanaopenda kilimo na ufugaji.

Ndoto yangu imekuwa kutafuta ujasiriamali utakaoniwezesha kuachana na ajira at 40 yrs. Baada ya kujaribu biashara mbalimbali nikagundua kuwa faida zilizopo kwenye kilimo na ufugaji ni kubwa mno especially kama una kamtaji ka kuanzia kapo. Nikaanza kutafuta mashamba. Nikapata kadhaa ila hili la Maseyu ndilo hasa linazaa matunda. Kwa wale wanajua Morogoro road, hicho kijiji kipo baada ya bwawani au km6 kabla ya Mikese. Shamba lipo km1.5 toka barabarani. Nilinunua eka 100 mwaka 2011.

Immediately nikaanza kufyeka na kung'oa visiki. Nikalima eka10 za mahindi na alizeti mwishoni 2012. Nililima eka 2 za tikiti maji, mazao yanastawi si mchezo. Masika ya 2013 nikalima eka 20 za alizeti na mahindi. Pia nikaanzisha mradi wa nguruwe. Nilianza na nguruwe 8 jike na dume mmoja. Sasa nina nguruwe kama 70 hv. Nilipata changamoto kidogo, nguruwe watatu walikufa. Kwa changamoto hizo nimepata uzoefu mkubwa. Mambo mengi kama kuchoma chanjo na kutibu baadhi ya magonjwa naweza kufanya mwenyewe kwa maana madaktari nao ni changamoto.nategemea kuanza kuuza nguruwe wakubwa by April.wadogo nauza though soko lake sio kubwa sana.

Pamoja na upungufu wa mvua mazao yangu ya vule yamekomaa, nna tikiti kama eka10 na mahindi kama eka 25. Next month nategemea kulima eka kama 70 hivi, nataka kulima mahindi, alizeti, ufuta, mtama na maboga. Vyote kwa biashara na chakula ya mifugo yangu.

Nataka niweze kuuza nguruwe 20 kila mwezi by this year. Mwaka jana nimevuna zaidi ya gunia 200 za mahindi na 150 za alizeti, fuso 2 za tikiti maji. Cha zaidi nimetoa ajira kwa vijana kazaa. Tatizo la maji shambani nimetatua last year kwa ku-design bwawa na matank cheap.

Karibuni wajasiriamali, future ipo kwenye kilimo.
 
Wana JF,
Nimeona mm pia nitoe testimonial kwa faida ya wajasiriamali wanaopenda kilimo na ufugaji.
Ndoto yangu imekuwa kutafuta ujasiriamali utakaoniwezesha kuachana na ajira at 40yrs.Baada ya kujaribu biashara mbalimbali nikagundua kuwa faida zilizopo kwenye kilimo na ufugaji ni kubwa mno especially kama una kamtaji ka kuanzia kapo.Nikaanza kutafuta mashamba.Nikapata kadhaa ila hili la Maseyu ndilo hasa linazaa matunda.kwa wale wanajua morogoro road,hicho kijiji kipo baada ya bwawani au km6 kabla ya mikese.Shamba lipo km1.5 toka barabarani.Nilinunua eka 100 mwaka 2011.Immediately nikaanza kufyeka na kung'oa visiki.Nikalima eka10 za mahindi na alizeti mwishoni 2012.Nililima eka 2 za tikiti maji.mazao yanastawi si mchezo.masika ya 2013 nikalima eka 20 za alizeti na mahindi.pia nikaanzisha mradi wa nguruwe.
Nilianza na nguruwe 8 jike na dume mmoja.sasa nina nguruwe kama 70 hv.Nilipata changamoto kidogo,nguruwe watatu walikufa.kwa changamoto hizo nimepata uzoefu mkubwa. Mambo mengi kama kuchoma chanjo na kutibu baadhi ya magonjwa naweza kufanya mwenyewe kwa maana madaktari nao ni changamoto.nategemea kuanza kuuza nguruwe wakubwa by April.wadogo nauza though soko lake sio kubwa sana.
Pamoja na upunyufu wa mvuA mazao yangu ya vule yamekomaa.nna tikiti kama eka10 na mahindi kama eka25.
Nextmonth nategemea kulima eka kama 70 hv.nataka kulima mahindi,alizeti,ufuta,mtama na maboga.vyote kwa biashara na chakula ya mifugo yangu.
Nataka niweze kuuza nguruwe 20 kila mwezi by this year.
Mwaka jana nimevuna zaidi ya gunia 200 za mahindi na 150 za alizeti.fuso 2 za tikiti maji.Cha zaidi nimetoa ajira kwa vijana kazaa
Tatizo la maji shambani nimetatua last year kwa ku design bwawa na matank cheap.
Karibuni wajasiriamali,future ipo kwenye kilimo.unauza mazao yako hamna mtu anakuuliza kodi! Hahaa
Ili mpate feel ya shambani see attachment
 
Attachments

  • IMG-20140105-WA0025.jpg
    IMG-20140105-WA0025.jpg
    44 KB · Views: 2,070
  • IMG-20140105-WA0008.jpg
    IMG-20140105-WA0008.jpg
    44.5 KB · Views: 1,778
  • IMG-20140105-WA0032.jpg
    IMG-20140105-WA0032.jpg
    75.6 KB · Views: 1,741
  • IMG-20140105-WA0017.jpg
    IMG-20140105-WA0017.jpg
    102.5 KB · Views: 1,707
  • IMG-20140102-WA0000.jpg
    IMG-20140102-WA0000.jpg
    56.6 KB · Views: 1,771
Mkuu ulianza na capital ya kiasi gani?, ulipata assistance gani? na nini net asset ( assets-liabilities) ya project yako? Nimeulia hivyo kwa sababu nime-note kasi kubawa ya kukua kwa mradi.

Capital kubwa ilikuwa kununua shamba,nilipata eka 100 kwa 10m.Hayo mengine niliweza kuyafanya on a monthly bases.nimeajiriwa so every month nilikuwa natenga kiasi kwenda shamba. Baada ya kuanza kilimo,sehemu kubwa shamba linajiendesha.na kilimo kule ni relatively cheap.in tye next 3 years nitakuwa mbali sana
 
MalafyaleP hili swali ni muhimu sana yaani kwa kuanzia ondoa hizo gharama za kununua ardhi
Zile za matayarisho ya shamba, ununuzi wa nguruwe, malipo ya vibarua au trekta la kulimia, ununuzi wambegu na mbolea maana kuna mbolea ya kupandia na ile ya kukuzia, gharama za palizi na hado uvunaji
 
Last edited by a moderator:

Mkuu,
Shambani kwangu hatutumii mbolea za kisasa bado. Ardhi bado bikira. Gharama za kulima mahindi kwa mfano,kupanda,mbegu,kupalilia (unapalilia mara 1 tu) hadi kuvuna ni approximately 120k kwa heka. Na hukosi gunia 15 kwa heka! Plan ni kutumia mbolea ya wanyama kwa sababu nafuga. Nguruwe niliwanunua kwa average ya 350k wakiwa na mimba za at least mwezi mmmoja. Sikununua wote kwa pamoja bali kwa hatua ndani ya miezi mitatu. Aliyeniuzia alinipa guidance jinsi ya kuwafuga vema.
Ukiangalia kwa makini sehemu kubwa ya chakula kinatoka shambani.
Kuna gharama ofcourse!Ninacho jaribu kuonyesha hapo ni kwamba inawezekana kufanikiwa kwenye project ya namna hii, kwa wenye moyo wa kutenda. Gharama za shamba haziwezi kuwa sawa kila sehemu na kila muda. Mi nilinunua 100k/eka lakini sasa ipo btn 250-300k per eka.
Mi nadhani jambo muhimu ni kwa walio na interest ya kufanya project kama hii. Tuliotangulia tupo tayari kuwa guide ipasavyo kutokana na uzoefu tulioupata. Sidhani kama unaweza kupata detail zote za project yangu kwenye forum hapa!The question is how do you start when you have that desire to start?!
Kuna mtu anauza nguruwe 200 kila mwezi na alitoa post humu humu!!
 
Hongera sana mkuu. Heri ulijitambua mapema kabisa. Mnazidi kututia moyo tunaoanza.
Nina swali moja, eka moja mahindi yaliyopata mbolea na mvua za kutosha unakadiria kuvuna kiasi gani?
Capital kubwa ilikuwa kununua shamba,nilipata eka 100 kwa 10m.Hayo mengine niliweza kuyafanya on a monthly bases.nimeajiriwa so every month nilikuwa natenga kiasi kwenda shamba. Baada ya kuanza kilimo,sehemu kubwa shamba linajiendesha.na kilimo kule ni relatively cheap.in tye next 3 years nitakuwa mbali sana
 
Hongera sana mkuu. Heri ulijitambua mapema kabisa. Mnazidi kututia moyo tunaoanza.
Nina swali moja, eka moja mahindi yaliyopata mbolea na mvua za kutosha unakadiria kuvuna kiasi gani?

Kaka bado sijaanza kutumia mbolea hizi za kisasa. Nalima tu at the moment na napata at least magunia 15 kwa eka. Mbolea za kisasa ni expensive and I do not see it necessary kwa shamba hili at the moment..Hizi mbegu za ukanda wa pwani performance yake ni magunia 25-35 kama mazingira ni optimal (ikiwa ni pamoja na mbolea ya kisasa). Magunia 15 kwa eka kwangu mm ni reasonable ukilinganisha na gharama. Kwa vile ninafuga,plan ni kutumia mbolea ya wanyama for the next 5 years then nita review performance.
 
Nitangulize shukran kwa moyo mkuu wa kutushirikisha shughuli yako. Maneno yako yanakuwa chachu kwa wengine, nafikiri siku moja nasi ndugu zako tuliosimama njia panda tutaitikia wito wako na kuchagua kupita njia uliyopita.
Ubarikiwe.
Salaam.
 
Asante sana barikiwa. Nami ninataka kujaribu mahindi kwa ajili ya mifugo eneo kidogo, linalobaki nitapanda miti. Uzi wako umenitia moyo
Kaka bado sijaanza kutumia mbolea hizi za kisasa. Nalima tu at the moment na napata at least magunia 15 kwa eka. Mbolea za kisasa ni expensive and I do not see it necessary kwa shamba hili at the moment..Hizi mbegu za ukanda wa pwani performance yake ni magunia 25-35 kama mazingira ni optimal (ikiwa ni pamoja na mbolea ya kisasa). Magunia 15 kwa eka kwangu mm ni reasonable ukilinganisha na gharama. Kwa vile ninafuga,plan ni kutumia mbolea ya wanyama for the next 5 years then nita review performance.
 
Mkuu,
Shambani kwangu hatutumii mbolea za kisasa bado. Ardhi bado bikira. Gharama za kulima mahindi kwa mfano,kupanda,mbegu,kupalilia (unapalilia mara 1 tu) hadi kuvuna ni approximately 120k kwa heka. Na hukosi gunia 15 kwa heka! Plan ni kutumia mbolea ya wanyama kwa sababu nafuga. Nguruwe niliwanunua kwa average ya 350k wakiwa na mimba za at least mwezi mmmoja. Sikununua wote kwa pamoja bali kwa hatua ndani ya miezi mitatu. Aliyeniuzia alinipa guidance jinsi ya kuwafuga vema.
Ukiangalia kwa makini sehemu kubwa ya chakula kinatoka shambani.
Kuna gharama ofcourse!Ninacho jaribu kuonyesha hapo ni kwamba inawezekana kufanikiwa kwenye project ya namna hii, kwa wenye moyo wa kutenda. Gharama za shamba haziwezi kuwa sawa kila sehemu na kila muda. Mi nilinunua 100k/eka lakini sasa ipo btn 250-300k per eka.
Mi nadhani jambo muhimu ni kwa walio na interest ya kufanya project kama hii. Tuliotangulia tupo tayari kuwa guide ipasavyo kutokana na uzoefu tulioupata. Sidhani kama unaweza kupata detail zote za project yangu kwenye forum hapa!The question is how do you start when you have that desire to start?!
Kuna mtu anauza nguruwe 200 kila mwezi na alitoa post humu humu!!
Mkuu unanitia moyo sana unapozungumzia ufugaji wa nguruwe na hio output aiseeee

Kuna mtu alileta mchanganuo wake humu jamvini kuwa almost 80% ya gharama za ufugaji wa guruwe ni chakula, hii ina maana kuwa kama unalima mwenyewe umepunguza gharama kwa almost 50% hivi, kitu ambacho economically ni very feasible.

Nitarudi baadae kukuuliza maswali mawili matatu kuhusu huu ufugaji wa nguruwe na kilimo cha matikiti maji kwani na mie nategemea kuanza soon ukanda huo kwani kwa sasa niko Rufiji na huku kelele za Imani ni nyingi unapofuga huyu mdudu na vyanzo vya maji ninavyotumia nina-share na community, ila mdogo mdogo tu tutatoka mkuu

Safi sana mkuu
 
Karibu kaka,
Aliyeleta mchanganuo wa chakula ni mm.Hiyo heading ya topic yangu nna maanisha kuwa ufugaji na kilimo vikienda pamoja,utaweza kupata manufaa kwa kiwango kikubwa kwa maana hizo sector zina leverage each other.Bei za vyakula hubadilika sana,ukilima mwenyewe inakupa unafuu sana
 
asante kaka tumekomalia jiji wakati mikese ni km sijui 200 toka dar lakini kama tumerogwa vile na hili jiji wewe ndio mjanja umetufumbua macho sana barikiwa sna mkuu,mimi nilikuwa na mpango wa kutafuta mashamba ila sikujua bei yake
Kusema kweli mashamaba ni mengi ila inatofautiana kulingana na eneo.kuna mashamba kibaha,mlandizi,kisarawe,mkuranga,bagamoyo,chalinze,morogoro na mikoani ndo zaidi.Cha msingi ni kujua unataka shamba kwa shughuli gani hasa.na pia hali ya hewa ya eneo. Kuna baadhi ya sehemu ukame ni mrefu zaidi etc.jinsi unavyokuwa karibu na dar bei inakuwa kubwa zaidi.
 
Mkuu,
Shambani kwangu hatutumii mbolea za kisasa bado. Ardhi bado bikira. Gharama za kulima mahindi kwa mfano,kupanda,mbegu,kupalilia (unapalilia mara 1 tu) hadi kuvuna ni approximately 120k kwa heka. Na hukosi gunia 15 kwa heka! Plan ni kutumia mbolea ya wanyama kwa sababu nafuga. Nguruwe niliwanunua kwa average ya 350k wakiwa na mimba za at least mwezi mmmoja. Sikununua wote kwa pamoja bali kwa hatua ndani ya miezi mitatu. Aliyeniuzia alinipa guidance jinsi ya kuwafuga vema.
Ukiangalia kwa makini sehemu kubwa ya chakula kinatoka shambani.
Kuna gharama ofcourse!Ninacho jaribu kuonyesha hapo ni kwamba inawezekana kufanikiwa kwenye project ya namna hii, kwa wenye moyo wa kutenda. Gharama za shamba haziwezi kuwa sawa kila sehemu na kila muda. Mi nilinunua 100k/eka lakini sasa ipo btn 250-300k per eka.
Mi nadhani jambo muhimu ni kwa walio na interest ya kufanya project kama hii. Tuliotangulia tupo tayari kuwa guide ipasavyo kutokana na uzoefu tulioupata. Sidhani kama unaweza kupata detail zote za project yangu kwenye forum hapa!The question is how do you start when you have that desire to start?!
Kuna mtu anauza nguruwe 200 kila mwezi na alitoa post humu humu!!

Mkuu MalafyaleP asante sana kwa ufafanuzi wako na mimi najiandaa mwaka huu lazima niingie kwenye kilimo aise maana hii biashara ya kukaa na kusubiri wengine walime na sisi tununue sio kabisa
tatizo Arusha mashamba ni bei balaa ni bora kutoka nje kabisa ya arusha kuangalia namna ya kuanzisha kilimo
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi wako
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom