Ufugaji ni Utajiri, kilimo ni mali

copied and pasted

Kwa ushauri wa Baba Mmoja ukitaka mali utaipata Shambani
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli, iwafae maishani.
Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa, kifo kina nikabili,
kama mnataka mali, mtayapata shambani.
 


Huyo mwandishi alikuwa na maono ya mbali sana. Bahati mbaya shairi hili laimbwa kwa wototo wadogo kabisa ambayo hawawezi kuelewa nini maana ya huo ujumbe wa Maisha. Binafsi hilo neno kwangu linaishi.
 
Post yako imenikumbusha mbali kuna shemeji yangu alikuwa mwanajeshi,ana rafiki yake ambaye naye alikuwa mwanajeshi bt yy aliacha kazi baada ya mwaka 2 tangu kuajiriwa akaanza kazi ya ufugaji ngombe wa kienyeji morogoro baada ya miaka 10 alikuwa na ngombe zaidi ya 3000.mwaka 2010 shemu alisitaf kazi huku akiwa hajamaliza nyumba yake siku moja huyo rafiki yake akamtembelea akiwa na VX mpya kwa kwel shemu alishangaa sana jamaa akamununulia shemu milango,madirisha,na vigaye vyote vya ndani! Toka siku hyo shemu anajuta kwa nini alikaa kwenye kazi muda huo wote,anasema angesikiza ushauri wa rafik yake naye angekuwa mbali
 

Mfano mzuri unahamasisha
 
NARUDIA TENA
VIJANA UFUGAJI SIYO KUKU NA NGURUWE TU.
TUAMKE
TANZANIA NI NCHI NZURI NA RAFIKI KWA VIJANA WOTE
Usiishie hapo kuwahasa vijana wape na orodha ya mifugo wanayoweza kufuga
 
mkuu,huu ushauri wako nimeulewa sana

naamini ukinunua ng'ombe wadogo ukawaweka kwa miaka mi 5 au 7,wakiwa wakubwa utawauza kwa bei kubwa mno

japo umeongea kwa vijembe,ila ni ushauri mzuri
 
hebu dadavua kidogo mkuu dume wangapi na malisho yamekugharimu kiasi gani mpaka hapo changamoto tuzipite vipi kiufupi mimi mkulima mdogo
 
Habari za Jumapili Jamii. Kama kuna mtu ana kitabu cha ' THE RICHEST MAN IN BABYLON" BY GEORGE S. CLASON asaidie kukiattach apa. kina ujumbe ambayo natamani mtu yeyote ambaye hajakisoma akisome. ni kitabu maarufu sana.
Ninacho nashindwa kukiweka hapa. Kama una telegram, ni pm namba yako nikutumie
 
Ninacho nashindwa kukiweka hapa. Kama una telegram, ni pm namba yako nikutumie

Ninacho pia ila nilishindwa kukiweka. Nilitamani kwa wapenzi wa kusoma vitabu wakipitie pia
 
Wadau angalieni fursa nyingine ya ufugaji hiyo

Hao NTV wana video nyingi zinahamasisha namna ya kufuga ng'ombe pia, na mazao mengine mifugo.
Wata
 
Okay yote ni sawa Ufugaji ni utajiri na kilimo ni mali although vs ni sawa ila ungetueleza ulinunua ngombe kwa bei gani na operation cost mpka wamekomaa unategemea kuwauza usisahau ya madalali then jumlisha pamoja na ugawanye kwa idadi ya hao ng'ombe utuambie faida ya ng'ombe mmoja ni kiasi gani?
Pia ujilipe mda wako uliokuwa ukiutoa kufuatilia mifugo yako
 
Usomaji wa Vitabu huongeza maarifa na uwezo wa kuona mbali
 
How do you manage risks? Je ngombe wana Insurance?
 
Risk hatuwezi epuka ila twaweza punguza. Sina Insurance Said
 
How do you manage risks? Je ngombe wana Insurance?
Kila biashara ina insurance mkuu...
kuna insurance za mifugo, mazao, usafirishaji n.k n.k

kuna hadi insurance against loss... kua ukipata hasara kwenye biashara yako kwa sababu nje ya uwezo..,,unalipwa... insurance zipo za kila aina..ushindwe wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…