Mkuu katika hao ndege hapo juu mimi ninawafuga kanga kiukweli kanga ni wazuri sana kufuga kwasababu kanga siku akitotolewa vifaranga vyake huwa ni mchaka mchaka havitulii na haviitaji dawa ya aina yoyote zaidi ya maji na chakula na huwa inakuwa vizuri ukinunua mayai yake ukaatamisha kwa kuku ili avilee vizuri vifaranga,vifaranga vya kanga huwa vinakuwa haraka kuliko vya kuku na wakisha kuwa wakubwa watakusumbua tu kwenye kelele vile vile huwa wanataga kwa msimu wako tofauti na ndege wengine na huwa wanapenda kutagia nje au kwenye pori sasa ukishaona wanataka kuanza kutanga inatakiwa unaweka kiota ndani harafu unakuwa unawafungia bandani hadi saa 7 mchana unawatoa hapo wanakuwa wamesha taga kabisa ndio unawatoa nje baada ya hapo unachagua hayo mayai umwachie kanga alalie mwenyewe au uchukue mayai umwekee kuku maana huwa yanakuwa mengi na kanga huwa anataga tu mfululizo.
Kuhusu soko,wewe anza kuwafuga wakishakuwa wengi utaona watu watakavyo kuwa wanakujalia kuulizia mayai na vifaranga hadi utashangaa mwenyewe hao hunaaja ya kujitangaza kelele zao tu zinakuletea wateja nyumbani,mayai moja(2000)
Kifaranga 5000
Kanga wakubwa 30000
Na haina kulemba wanauzika sana baadaye ndakuwekea picha
Kuhusu hao bukini na bata mzinga bado sijajua vizuri ngoja tusubiri wadau
-Ndumilakuwili-