Mkuu,
Kiukweli kuna aina nyingi sana za miti na maua / mimea yenye maua yapendayo na nyuki. Upandaji pia unategemea sana mipango yako ya muda mfupi na muda mrefu katika mradi wako wa ufugaji nyuki, pia eneo ulipo.
Naomba nitaje michache na rahisi kupanda;
Miti: Miembe, Milonge, mizambarau, michungwa, mipera, papai, mi-passion, minazi, miparachichi, kahawa, karafuu, eucalypts n.k
Maua: Aina zote, ikiwemo maua pori kama bidens pilosa (manata nguo)....
Mazao: Alizeti (pollen kwa wingi), mbaazi, mahindi, karanga, carrots, maharage, mpunga n.k
Kibiashara, uchaguzi wako wa miti / mazao ya kupanda shambani ufanyike kwa kuangalia mimea ambayo utakuwa unavuna na ikawa sehemu ya kipato.