Ufugaji wa kisasa wa Nyuki: Faida, Utaalam na Masoko

mkuu shukrani kwa elimu unayotoa, mimi napenda kujua kwa wastani mzinga mmoja unaweza ukavuna mara ngapi kwa mwaka kwa eneo lenye vegetation kwa wingi?
 
 
Mheshimuwa ninahitaji kujua ni miti au maua ya aina gani ni mizuri kupanda kwenye shamba la nyuki
 
Ni vema pia kuwa na Kalenda ya ufugaji nyuki ( Beekeeping Calendar ) ya eneo husika , hiyo itakuwa mwongozo mzuri wa kuongoza kifanyike na kwa Wakati upi, mf. Kuandaa eneo la manzuki,kuandaa mizinga, kuambika, usimamizi na ukaguzi wa mizinga,kurina na kuchakata makao ya nyuki n.k
 
Mkuu,

Kiukweli kuna aina nyingi sana za miti na maua / mimea yenye maua yapendayo na nyuki. Upandaji pia unategemea sana mipango yako ya muda mfupi na muda mrefu katika mradi wako wa ufugaji nyuki, pia eneo ulipo.

Naomba nitaje michache na rahisi kupanda;

Miti: Miembe, Milonge, mizambarau, michungwa, mipera, papai, mi-passion, minazi, miparachichi, kahawa, karafuu, eucalypts n.k

Maua: Aina zote, ikiwemo maua pori kama bidens pilosa (manata nguo)....

Mazao: Alizeti (pollen kwa wingi), mbaazi, mahindi, karanga, carrots, maharage, mpunga n.k


Kibiashara, uchaguzi wako wa miti / mazao ya kupanda shambani ufanyike kwa kuangalia mimea ambayo utakuwa unavuna na ikawa sehemu ya kipato.



Mheshimuwa ninahitaji kujua ni miti au maua ya aina gani ni mizuri kupanda kwenye shamba la nyuki
 
Real G,

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mzinga na mzinga kwenye uvunaji kutegemea na aina / design hata kama yote itawekwa kwenye eneo moja lenye mazingira sawa.

Kujibu swali lako vizuri, frequency ya uvunaji kwa mzinga kama eneo lina vegetation kwa wingi linaweza kuwa zaidi ya mara sita kwa mwaka (yaani unaweza kuuvuna mzinga mmoja zaidi ya mara sita kwa mwaka). Lakini, wingi wa vegetation kwenye eneo haudetermine sana frequency ya uvunaji bali "rotational flowering" ya vegetation husika. Mfano, ukiwa na eneo lenye alizeti kwa wingi na hiyo alizeti inatoa maua mara mbili tu kwa mwaka, tafsiri yake ni utavuna mara mbili. Lakini ukiwa na eneo lenye alizeti kwa wingi, milonge, maembe, maua mbali mbali n.k basi utavuna mara nyingi.

Niliwahi kumtembelea mfugaji nyuki anayefanya rotational farming na kuhakikisha kila kipindi cha mwaka ana maua, kila mzinga anavuna mara 15 kwa mwaka.


mkuu shukrani kwa elimu unayotoa, mimi napenda kujua kwa wastani mzinga mmoja unaweza ukavuna mara ngapi kwa mwaka kwa eneo lenye vegetation kwa wingi?
 
Karibu sana mkuu.

Kuona kwa macho ni tofauti sana na kusikia.


Mkuu maswali yote umejibu vizuri kwa hekima kuu, Mungu akubariki. Naomba unielekeze uliko siku moja nikutafute nije kujifunza kwa macho shambani kwako kwa maujuzi zaidi
 
Karibu sana mkuu.

Kwa sasa ninafanya hizi shughuli za ufugaji nyuki Saadan, Morogoro na Kisarawe.


Salute kwako Allan,nimejifunza mengi sana...kama hutojali kutuambia Shamba la nyuki wako lilipo angalau siku moja tukatembeleana.
 
mkuu shukrani tena, soko la asali kwa sasa hivi likoje, maana uzi ni wa tangu mwaka 2013, soko linaweza kuwa limebadilika
maana changamoto kubwa kwenye kilimo ni soko la uhakika
 
Salute
 
Nataka Kujiunga na Chuo cha Nyuki Tabora!Nina Ufaulu wa Geography=B,Biology=D,English=C!
A-level:
Geography=E,English=S!
Naweza Kupokelewa?
Na Ada Zake Zikoje?
Kama Kuna Mtu Mwenye Mawasiliano Naomba Anipe!
 
ninataka kuanzisha ufugaji wa nyuki ninawaomba mwenye uzoefu busness plan anisaidie
 
Shamba la kufugia nyuki, linapaswa kuwa na ukubwa gani, mf: ekari moja inakaa mizinga mingapi!? Halafu kwenye mzinga unajuaje kama asali imejaa?
 
Idadi ya mizinga inategemea upatikanaji wa maua na maji. Hivyo ni very critical. Kama hivyo sio tatizo, unaweza kuwa na mizinga.kati ya 100-200 kutegemeana na jinsi unavyoitundika. Njia ya vichanja inabeba mizinga.mingi zaidi.

Kuhusu kujua kama mizinga.imejaa, ni suala la calendar.
 
JE UNATAKA KUFUGA NYUKI KWA NJIA YA KISASA NA KIBIASHARA ZAIDI

THE HIVE LTD TANZANIA WANASHUGHULIKA NA MAMBO HAYA

MPIGIE MENEJA MIRADI BW. Nicas Mbeikya 0653 930 391 au 0653242627 Kwa maelezo ya kupatikana kwa soko,mizinga na vifaa vyake vya kisasaaa.
 

Attachments

  • 13932736_1167722699965536_1271352412995484818_n.jpg
    53 KB · Views: 264
  • 14022270_1167718709965935_861364356177463643_n.jpg
    125.4 KB · Views: 297
  • 14045772_1167719939965812_4200483841395713158_n.jpg
    118.3 KB · Views: 291
  • 14046035_1167720653299074_2808127119109415584_n.jpg
    109.6 KB · Views: 276
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…