Kwa mimi binafsi jinsi nilivyo ni kwamba kila mfugo unaowezekana kufuga mimi huwa nafuga huwa sisubiri kusikiliza kwa mtu kwa upande wa sungura huwa nawapenda kwasababu ufugaji wake ni rahisi sana na hauna gharama,ni kuwatengenezea banda zuri harafu unanunua mbegu hapo unaweza anza na wawili tu dume na jike na baada ya hapo utapata sungura wengi sana baada ya muda mufupi hadi utashangaa.
Chakula chake hununui unang'oa majani unawawekea ni bure kabisa na mabaki ya vyakula wao wanagonga kwa wale wenye mashamba na bustani yale majani ya kupalilia unayakusanya unawawekea wanagonga vizuri ambayo wewe ungeyatupa.
Hawaumwi kizembe na wala huwezi poteza gharama kununua dawa.
Sasa ninamaana mtu unaweza kuwafuga kwa mapenzi yako kwasababu hawana gharama ikitokea mtu anawahitaji unaweza muuzia (hapa huwa wanajitokeza sana kununua wakisha jua tu unao sungura)na vile vile unaweza watumia wewe mwenyewe wakakupunguzia gharama za kitoweo(hapo wewe ni mboga za majani na kitoweo cha nyama ya bure hiyo utaamua wewe uchome ,ukaange na nk)
KWA WENYE SHAMBA NA BUSTANI.
sasa hivi samadi inauzwa sasa wewe sungura watakupatia samadi nyingi bure na mkojo utakaotumia kunyunyiza kwenye mimea yako .
USISIKILIZE ETI NGOJA NIPATE SOKO LA MKUPUO WEWE ANZA KUFANYA FAIDA ZA HICHO KITU UTAZIPATA MBELE NA UTASHANGAAA.
Mfano,kuna watu huwa wanabeza hata wale bata wa kienyeji kwamba hawana soko kama wanavyobeza sasa kwa sungura lakini kuna watu wanafanya biashara ya kuchinja na kupaki nyama ya bata vizuri na kuziuza kama kuku kitu ambacho kinawezekana kwa nyama ya sungura nimeweka picha hapo chini.
Angalizo hizo picha sio za kwangu nimechukua kwa mjasiliamali yuko Dar.
View attachment 726571View attachment 726572