Naomba nianze kwa kushukuru sana JF kwa posts nyingi zinazohusu mambo ya ujasiriamali na hususan ufugaji. Nimejifunza mengi sana hapa. Pia nashukuru mitandao mingine kama vile Mkulima Young na Kilimo ni ujuzi (hivi ni vya Kenya). Baada ya kutafakari watu wanavyotengeneza hela kupitia ujasiriamali, na mimi nimeanza.
Kwa kuanza, nimeanza na vifaranga vya mwezi mmoja 50. Nimeamua kuchagua umri huu kwa sababu ni rahisi kuchagua kati ya tetea na jogoo. Hivyo mimi nimeweka ratio ya jogoo 1 kwa tetea 7. Nimechukua mbegu ya kienyeji ambayo imekuwa crossed (chotara) kwa maana ya mchanganyiko wa kienyeji ya hapa kwetu na wale wa Malawi na wale wa Afrika kusini). Nilivutiwa sana baada ya kuangalia kuku wakubwa kwa huyu jamaa ambaye nimenunua kutoka kwake, yaani utapenda.
Mwisho wa mwezi ujao natarajia kuongeza tena vifaranga vyenye umri wa mwezi mmoja kama nilivyofanya mwezi huu.
Kusema ukweli sina uzoefu mimi binafsi katika kazi hii, lakini nimesoma mengi kuhusu ufugaji wa kuku.
Naombeni uzoefu wenu wapendwa, kwa sasa mambo mengine nafanya kwa kuuliza kwa wazoefu. Ila baada ya miezi michache nitakuwa na uzoefu pia. Nina swali;
- Hivi zile randa tunazotandaza sakafuni inatakiwa ikae muda gani ndo nibadilishe niweke nyingine? Je ni kila siku au baada ya siku ngapi? Kwa sasa mimi natumia tuu uzoefu naangalia zikianza kuchafuka ndo nabadilisha (kwa hiyo yaweza kukaa siku tatu, nne au tano.
- Maswali mengine nitauliza kadiri nitakavyokutana na changamoto