Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Habarini wapendwa wafugaji wenzangu,mm no mgeni humu,napenda kujua Hui ugonjwa was mdondo tiba take,kwani no ugonjwa unaoniulia Kuku Wangu kwa wingi
 
Naomba nianze kwa kushukuru sana JF kwa posts nyingi zinazohusu mambo ya ujasiriamali na hususan ufugaji. Nimejifunza mengi sana hapa. Pia nashukuru mitandao mingine kama vile Mkulima Young na Kilimo ni ujuzi (hivi ni vya Kenya). Baada ya kutafakari watu wanavyotengeneza hela kupitia ujasiriamali, na mimi nimeanza.

Kwa kuanza, nimeanza na vifaranga vya mwezi mmoja 50. Nimeamua kuchagua umri huu kwa sababu ni rahisi kuchagua kati ya tetea na jogoo. Hivyo mimi nimeweka ratio ya jogoo 1 kwa tetea 7. Nimechukua mbegu ya kienyeji ambayo imekuwa crossed (chotara) kwa maana ya mchanganyiko wa kienyeji ya hapa kwetu na wale wa Malawi na wale wa Afrika kusini). Nilivutiwa sana baada ya kuangalia kuku wakubwa kwa huyu jamaa ambaye nimenunua kutoka kwake, yaani utapenda.

Mwisho wa mwezi ujao natarajia kuongeza tena vifaranga vyenye umri wa mwezi mmoja kama nilivyofanya mwezi huu.

Kusema ukweli sina uzoefu mimi binafsi katika kazi hii, lakini nimesoma mengi kuhusu ufugaji wa kuku.
Naombeni uzoefu wenu wapendwa, kwa sasa mambo mengine nafanya kwa kuuliza kwa wazoefu. Ila baada ya miezi michache nitakuwa na uzoefu pia. Nina swali;
  1. Hivi zile randa tunazotandaza sakafuni inatakiwa ikae muda gani ndo nibadilishe niweke nyingine? Je ni kila siku au baada ya siku ngapi? Kwa sasa mimi natumia tuu uzoefu naangalia zikianza kuchafuka ndo nabadilisha (kwa hiyo yaweza kukaa siku tatu, nne au tano.
  2. Maswali mengine nitauliza kadiri nitakavyokutana na changamoto
 
hongera mkuu hatua nzuri uliyo amua pia fuata karenda ya chanjo, muone mtaalam uliye karibu nae akupe kalenda hiyo na uifuate.
 
Wanajamii mimi ni kijana niliemaliza chuo na ctaki kuajiri ila nataka kuwa na biashara yangu mwenyew na biashara ninayopenda kuifanya ni kufuga na kuuza kuku pamoja na mayai nilikuwa naomba ushauri kwa m2 mwenywe uzoefi na biashara hio je mtaji wake ni kiac gan na matayarisho yake yakoje
Tafadhal naomba mnisaidie kwenye hili
 
inategemea na idadi ya Kuku unaotaga kuanza kufuga, kwa mfano kwa hali ya sasa ilivyo Kuku 400 broiler inahitaji mtaji wa sh 1,600,000/= vifaranga
400×1300=520000
chakula magunia 25×46000
madawa=50000/=
nakutakia kila la heri kijana mwenzangu
 
pitia na baadhi ya post humu jamvini kama alivyoshauri Ndugu barafuyamoto, Ila kwa hali ilivyo sasa bei zimepanda vifaranga vilikuwa 1100 Ila kwa sasa 1300, chakula kizuri kilikuwa 42000 Ila sasa hivi 46000 jitahidi kuweka order mapema za vifaranga usidanganyike kununua chakula cha bei rahisi Kuku watachelewa kukua, chakula kizuri ni falcon au kinachotengenezwa na interchick, ukitaka kupata faida nzuri subiri Kuku wafikishe week 5, bei ya kuuzia jitahidi isiwe chini ya 5000
 
inategemea na idadi ya Kuku unaotaga kuanza kufuga, kwa mfano kwa hali ya sasa ilivyo Kuku 400 broiler inahitaji mtaji wa sh 1,600,000/= vifaranga
400×1300=520000
chakula magunia 25×46000
madawa=50000/=
nakutakia kila la heri kijana mwenzangu

samahani naomba kujua hapa mtaani kuna dogo naye anataka kuanza uFugaji wa kuku wa nyama ila mtaji wake ni mdogo so anataka kuanza na kuku 100 na kukuza hadi kiwango cha juu, swali je hii anaweza kwa hio idadi kukuza mtaji wake?????
mimi sina sana utAalamu wa kufuga kuku wa nyama, ntashukuru msaada wako
 
samahani naomba kujua hapa mtaani kuna dogo naye anataka kuanza uFugaji wa kuku wa nyama ila mtaji wake ni mdogo so anataka kuanza na kuku 100 na kukuza hadi kiwango cha juu, swali je hii anaweza kwa hio idadi kukuza mtaji wake?????
mimi sina sana utAalamu wa kufuga kuku wa nyama, ntashukuru msaada wako
Malila ....
 
Last edited by a moderator:
inategemea na idadi ya Kuku unaotaga kuanza kufuga, kwa mfano kwa hali ya sasa ilivyo Kuku 400 broiler inahitaji mtaji wa sh 1,600,000/= vifaranga
400×1300=520000
chakula magunia 25×46000
madawa=50000/=
nakutakia kila la heri kijana mwenzangu

Mkuu umefanya vema kutoa mchanganuo huo,lkn vipi kuhusu makazi yao yaani nyumba yao?.
 
Wana jamvi, tujuzane namna bora zaidi kufuga kuku wa kienyeji kwa tija.... Kwa anayejua naomba kumwelewa
 
Naomba kufahamishwa Namna ya kumuwekea kuku Mayai. Je una mkamata na kumtoa pale ktk kiota?

Mayai naweza yawekea Alama kwa Pensil au Marker pen?
 
Nimefurahi sana kwa maada hii. Mimi ninadawa inayoweza kuwaponya kuku WANAOUMWA KIDELI. Nitafute kwa anayehitaji 0763797853
 
Back
Top Bottom