Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Huu uzi ningekutana nao mwezi ulopita,ningekupa deal. Kuna mtu anatuletea mayai ya kienyeji ofisini tray 12000, ametushika staff wote. Jamaa anapiga hela. Pole lkn pambana.
 
nimenunua huyo kuku wa kienyeji aliyefugwa mjini kwa kweli ni hasara tupu.mgumu ladha 0 ,bei ghali sana nikajilaumu sana.bora ningechukua wa kisasa nijue moja
 
Huyo wa trey 12,000 niunganishe nami awe ananiletea. Wengi wanauza 16,000 hadi 18,000. Note watanzania tunapenda vitu vya bei rahisi.....
Sawa ntafanya hivo. Na akiishiwa mayai, mimi huwa nayafuata Magomeni sokoni, pale usalama, reja reja wanauza moja 500, huwa nachukua tray2 kwa Tshs 25000-27000
 
Pole kaka... lakn usikate tamaa, kila kitu kina changamoto zake ,hata hao wa mayai kuna kpnd masoko yanasumbua, inafikia kpnd wanauza mayai kwa bei ya hasara maana hayakai muda mref ukilinganisha na ya kienyej.
Komaa kutafuta soko zur ,,never give up
 
Kama unafuga mjini bado sio sababu ya kukosa soko,ingia gharama wapatie vitu vya kuwafanya wawe wa kienyeji,wape majani kwa wingi,hata kama ya kununua,mm kuku wangu nawanunulia fungu moja la mchicha au spinachi kila siku.

Mm nauza tray 10,000,hlf nikuhakikishie,soko la kienyeji liko tyr kuliko hao wa kisasa,achana na wateja wanaosumbua,km mtu ana swali mweleweshe km haelewi achana nae,kwa changamoto zilizopo kiafya watu wanapenda mayai ya kienyeji,unless km hao kuku huwafugi kienyeji,ie kuwafungulia watoke nje wajitafutie na ww kuwapa nyongeza kidogo ya chakula hada majani.
 
Hongera kwa kujiajiri
Na pole kwa changamoto bro
Ila usikate tamaa na hzo changamoto
Mimi kama mtaalamu wa Mifugo nakushauri mambo yafuatayo
1.Chagua mbegu bora ya kuku ili uweze kuzalisha mayai ya aina moja
2.Zingatia chakula bora ili kukabiri soko mfano mahitaj ya kiin cha njano na ukubwa wa mayai
3.Ili ukaribiane na changamoto ya kupata hasara jitahid kufuga kuku mchanganyiko yaani wa kienyeji na wa kisasa ili uzibe mwanya wa mashindano ya soko lako
4.Boresha lugha ya kibiashara ili uwavutie wateja wako
Mwisho tutazid kuwa pamoja
By animal scientist
 
Umesomeka mkuu,ila hyo namba 3,nimeielewa sana.
 
Ahsante kwa wazo,mimi nauza kwa 12,000 nilichojifunza kwako suala la bei.Nadhani natakiwa nipunguze bei kidogo ili niwe kwenye mzunguko wa haraka.
 
Pole sana, mimi ninao 30 nilipitia changamoto hizo, nikaamua niwe nawapa majani kwa wingi, taratibu kiini kikaanza kuwa cha njano. Ila kiukweli soko la mayai ya kienyeji sio la wazi...hii pia ikanifanya kufuga kuku wa mayai ya kisasa. Mayai ya kisasa yanasoko linaloonekana na pia yanawalaji wengi.
Ushauri, uwape kuku majani kwa wingi, Pia jitahidi kutafuta soko katika maofisi mbali mbali kwa Dar ukiuza tray 12,000 lazima yatoke.
 
Pole sana ndugu. Kweli kuna changamoto kwenye soko. Niliwahi kupata shida ya kuuza mayai ya kienyeji. Tafuta mahali watakapokuamini uuze. Tafuta bank, hospitali, sehemu yenye wafanyakazi supply hapo mara kwa mara. Ukiweza tafuta mteja atakayechukua kwa bili na mpelekee mayai fresh. Mimi nafuga kwale na nauza mayai kwa bili sihangaiki na soko. Usiuze reja reja niliwahi kusumbuka kila mtu anakugongea geti anataka yai moja mawili, matatu ni usumbufu. Pia tumia unaweza kutumia njia ya kubadilishana. Mimi mayai yangu ya kienyeji nampa mtu wa gengeni hela sichukui nachukua bidhaa kama nyanya, mboga mboga, na mahitaji mengine.
 
Mayai ya kwale soko kuu ni kwenye vitengo, tatizo ukitoka pale washikaji wakikuona wanaweza pakazia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…