Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

hutakiwi kukata tamaa kuwa mjanja kutafuta siko la mayai yako ushafika hatua nzuri usirudi nyuma tafuta soko
 
Ndugu. Kwanza tatizo lako ni Dogo Sana. Kuangalia watu wanasemaje. Pili kukata tamaa.

Yakupasa ujue kwamba biashara ni vita, na yakupasa uishinde.

Watanzania wengi wamekuwa na kasumba ya kukosoa bidhaa hasa za watanzania wenzao na kuthamini bidhaa za nje.

Mimi ni mfanyabiashara. Na ninazungumza kitu ninachojikua kwa tabia mbaya walionao baadhi ya watanzania, ni kudhara vya ndani na kutukuza vya nje.

Chamsingi.
Nikutokukata tamaa. Chapakazi kwa bidii Endelea na Ufugaji wako uo huo na kuku Hao Ao.

Fungua macho mikoani, maana hakuna mafanikio bila changa moto.

Changa moto zipo ili ufanikiwe zaidi. Kama hapo mtaani kwako wana yakataa mayai yako, inua Macho Kwingine Pata hasira ya kutafuta Masoko.

Nenda kwenye Mahotel. Vioski vya chips. Nenda madukani, Fungua Duka la kuuza Mayai kwa Bei ya Jumla.

Panuka kimawazo, usiazie Eneo 1 la hao wanao kukatisha Tamaa.

Huwezi kufanikiwa kwa kuangalia watu wanasemaje au wanakusemeaje biashara yako. Fuata Ndoto zako Ona picha ya Kupanuka na kuongezeka sana.

Ukisha Jenga Picha Hii hakika hakuna mtu atakukwamisha katika safari yako ya mafanikio.

Ona unaudumia Africa Nzima Mayai na Kuku wa kienyeji, alafu kila siku jiambie wewe ni mfanyabiashara Mkubwa ulimwenguni.

Alafu anza kutenda mambo yako kwa ufanisi na kutokukatishwa tamaa na mtu Awaye yote.
 

Mkubwa tunakusubiria bila shaka kabisa Kubota; kwani hakika ni na imani ni mbinu mbadala kabisa unakuja nayo mkubwa wangu! Hii uzi ninaisave left kabisa nikitegemea newz toka kwako! Asante sana! Hapa ndiyo Jf jamani!






 
Kiukweli kumufuga kuku wa kienyeji kwa njia ya commercial feeding utegemee kupata faida ni ngumu kidogo,
Nimefuga sana hao kuku, ili upate faida nzur lazima ufuge sehemu ambayo una eneo la kutosha kiasi kwamba muda mwingi utawafungulia wajitafutie wenyewe chakula.
Kwa njia hio pia inaboresha ubora wa mayai utakayopata.
Ukimufungia ndani muda wote kwa kuwalisha vyakula vya kisasa uwezekano wa kupata mayai yenye uharisia wa ukienyeji inakuwa mdogo sana.
 
Mpwa wangu anawafuga shambani, wako huru kutembea na pia gharama ya chakula si sawa na kuwafungia, wanajitafutia ingawa anawawekea pumba zilizochanganywa na unga wa dagaa pamoja na maji ya kunywa asubuhi wakiwa wanatoka na jioni wakirudi. Matatizo ni vicheche na mwewe. Lakini bado anaona faida.
 
Habari za saizi wapendwa, Mimi ni mtanzania mwenzenu niliyebahatika kukua katika FAMILIA ya kiufugaji,(KUKU WA KIENYEJI).
Tuna kampuni yetu iitwayo SHITINDI POUTRY FARM AND HATCHER.

Hii kampuni inajihusisha hasa katika...

  • UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.
  • UTOTOLESHAJI WA MAYAI.
  • UUZAJI WA INCUBATOR(MASHINE ZA KUTOTOLESHEA VIFARANGA).
  • UUZAJI WA VIFARANGA.
Zaidi tunatoa fursa za kutoa SEMINA za bure kabisa bila malipo ya aina yeyote kwa vikundi yva ujasiliamali na kwa mtu mmoja mmoja pia.


Zaidi ya yote madhumuni yangu ya kuja humu na kuandika jambo hili ni kwamba watu wengi na watanzania wenzangu jambo hili liwafikie, nimeiona watu wengi wakifanikiwa kupitia semina zinazoendelea mara kwa mara bilia kukoma.


kwa maelezo na mawasiliano tembelea blog yetu SHITINDI POULTRY FARM AND HATCHER

au kwa simu namba
  • +255 713 071 701
 
malalamiko ya wateja wako kuhusu mayai yako baadhi yana hoja. kuku wa kienyeji kwa mjini tatizo kubwa ni eneo. wanahitaji eneo kubwa wawe huru na kupata vyakula asili, kama wadudu, majani nk. kuwafungia ndani bila kuwalisha 'formula', uasili wake hupungua. la ukubwa na rangi ya mayai si hoja. ukubwa na rangi ya kuku huamua ukubwa na rangi ya yai. kuna kuku asili wakubwa hutaga mayai makubwa mpaka gm 56, ukubwa ambao ni yaidi ya wastani wa mayai ya kuku wa kisasa. waelimishe wateja na kuongeya mbinu za ulishaji.
 
Ahsante kwa wazo,mimi nauza kwa 12,000 nilichojifunza kwako suala la bei.Nadhani natakiwa nipunguze bei kidogo ili niwe kwenye mzunguko wa haraka.

Sio lzm kupunguza,mm nauza hivyo kwa sababu wateja wangu wengi wanakwenda kuuza lkn wale wachache wa kula nawauzia 12,000.
 
Unapatikana wapi unatotoa kwa gharama gani kwa trei bei ya hiyo incubator pia
 
Morogoro wateja wengi sana mpaka mayai yanashindwa kukidhi uhitaji. Wengi wanataka yenye jogoo kwa ajili ya kutotolesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…