Ahadi Shitindi
Member
- Aug 17, 2016
- 21
- 15
yah that is what am doing now bro, na faida ipo sana tu.Naamini soko lipo, pigana Kaka! Jiingize kwenye magroup, post Facebook, zunguka kwenye maofisi. Utafanikiwa, kama ni kweli ukishindwa njoo niuzie. Nina mpango wa kuweka kuku wa kienyeji 600
Ahsantee kwa taaarifa mkuu ila nimepitia source yako vitu vingi umeelezea juu juu tu me nadhani ungetoa ufafanuzi hata hapa kuhusu gharama za Yale matangazo yako kule kuhusu hizo heater incubator vifaranga na menginetrey natotolesha sh 10000 tu, pia napatikana Kimara Temboni Dar es salaam..
karibu sana
Ahsantee kwa taaarifa mkuu ila nimepitia source yako vitu vingi umeelezea juu juu tu me nadhani ungetoa ufafanuzi hata hapa kuhusu gharama za Yale matangazo yako kule kuhusu hizo heater incubator vifaranga na mengine
Ahsantee kwa ufafanuzi uluosimama kuhusu kutotolesha mayai ya siku saba inawezekana kupata vifaranga vingapi kwa trei moja na bei ya incubator hiyo ya mayai 48 maana bado mtaji mdogo kwa kweli ningekua naku-pm ila bado sina uzoefu na hii appMASHINE ziko za viwango tofauti tofauti, mfano kuna mashine ya kuanzia mayai 48, 88, 144 ,264, 432, 528 ,726, 1056 , 2112.. na zingine za viwango tofauti..
samahani mara nyingi huwa swala la bei hatuweki mitandaoni kwa sababu tunatoa mizigo yetu nje, na kama unajua huwa dolla unabadilika unaweza leo ukaweka kiasi fulani na dolla ikapanda au kushuka.
Na kuhusu VIFARANGA , Kifaranga mmoja ni shilingi 1500/=( huyo ni wa siku ya kwanza).
Na pi vyote vilivyoandikwa hapo na kule kwenye Blog vipo, ukija kujifunza unaonyeshwa kwa vitendo.
Unapatikana wapi mkuu
Du! Sikulijua hilo,kwa hiyo hata wakisasa nikimwacha ajitaftie chakula na dawa nisimpe anakuwa wa Kienyeji?Kuku wa kienyeji ni yule anayejitafutia mwenyewe....kuku wa kienyeji ukimfungia ndani na kumpa chakula na madawa huyo ni "wakisasa"
Wana JF habari zenu?
Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu kwa Karama ya Ufugaji aliyonijalia.
Mimi ni mfugaji wa Kuku wa kienyeji,nilianza mwaka 2011 na Tetea 2 kwasasa nna Tetea wakubwa 100,Majogoo 20,Vifaranga vya miezi miwili 59,Vifaranga vya Wiki moja 50.
Hao Tetea na majogoo kwasasa wana miezi 7,Tetea ndo wameanza kutaga,kwasasa nakusanya Trei 1.5 kila siku,plan zangu wafikishe Trei 2 Kila siku ili Trei moja Igharamie Chakula chao na dawa,Trei nyingine iwe ni kama faida ya kunisaidia kutunza Vifaranga.
Ila Changamoto iliyonifanya niandike uzi huu ni Ukosefu wa Soko la uhakika la Mayai ya Kienyeji.Na kwa wachache nnao wapata nakutana na majibu haya:
"Mh! Haya mayai ya Kienyeji?,mbona mengine makubwa kama ya kisasa?.Mh! Kiini chake mbona sio njano sana?,au yamechakachuliwa,Afu mayai ya kienyeji huwa na ganda jeupe nje yakwako mbona mengine brown?Hao kuku umefugia wapi kama ni hapa mjini Hakuna kuku wa kienyeji wote wamechakachuliwa"
Kiukweli majibu haya yananikatisha tamaa sana mpaka najiona niliingilia mlango wa kutokea,Kuku nimewafuga kwa shida sana mpaka walipofikia,nilijua huu utakuwa muda kupumua baada ya kaz ngumu,matokeo yake nimekutana na Changamoto ya Soko la mayai,ambayo ndo Msingi wa faida ya mfugaji yeyote yule.Na mimi nna rafiki yangu amefuga kuku wa kisasa yaani mwenzangu saizi anapiga pesa ni balaa,sababu ni kwamba mwenzangu Soko lipo nje nje tu.
Na Kiukweli kama wana JF,hamtonisaidia kuikabili Changamoto hii naapa Kuwauza kuku wa Kienyeji wote,na nianze kufuga wa Kisasa.Sababu ni kwamba Watanzania tunapenda vitu vya Bei rahisi hata kama vina Athari kwa afya zetu.Tathmin yangu butu inanionesha kuwa Mayai ya kisasa yanaliwa na watu wengi zaidi kuliko ya Kienyeji.
Naombeni msaada wa Soko kwa anaelifaham,au nihamie Upande wa pili!
Ahsante mkuu kwa maelezo yako mazuri,tupo pamoja.Mkuu pole kwa changamoto za ufugaji, nisingependa kukukatisha tamaa ila ni vyema nikupe ushauri utakaokusaidia kama ukiamua kuufanyia kazi. binafsi niko katika sekta ya ufugaji na nimejipatia uzoefu mkubwa kidogo tangu nianze hii shughuli. ukweli uliomchungu ni kwamba, kibiashara, hasa ya mayai na nyama, kuku wa kienyeji pure hawalipi. kwanini nasema hawalipi.
Biashara ya Mayai.
kwa asili ya kuku wa kienyeji,huwa wanatabia ya utagaji mara nyingi ni siku kwa siku 10 mfululizo, utamiaji -siku 21, na uleaji wa vifaranga -siku 50-60. hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka. Idadi hii ya mayai haina tija kibiashara kwani kuku mmoja anaweza kukuzalishia tray 1 mpka mbili kasoro pekee kwa mwaka ambayo kwa bei ya soko si Zaidi ya shilingi za kitanzania 20,000 tu kwa mwaka.
Changamoto kwenye soko la mayai ya kienyeji. nilianza kusambaza mayai ya kienyeji kwenye supermarkets miaka mitatu iliyopita.. Haya mayai yako fertilized, (yamerutubishwa na majogoo) hivyo storage yake ni ngumu Zaidi ukilinganisha na mayai ya kuku wa kisasa kwa vile hayana mbbegu. nilipata sana tatizo la mayai kuharibika hasa yasipotoka ndani ya kipindi cha week moja au Zaidi kutegemeana na hali ya joto.
Mwiaho ni gharama za mayai husika, bei ya mayai ya kienyeji iko juu ukilinganisha na gharama za mayai ya kuku wa kisasa. soko kubwa la mayai ni pamoja na vibanda vya chips, migahawa na hoteli. hawa wanauhitaji mkubwa sana wa mayai na soko liko juu muda wote wa mwaka. Soko la mayai ya kienyeji lipo Zaidi kwenye households. (soko la familia) hasa kwa vigezo vya kuzingatia afya Zaidi. Soko hili la familia sio kubwa, ni soko dogo na mara nyingi hutumia tray moja kwa kipindi cha wiki mbili au Zaidi. kwa mzalishaji mkubwa wa mayai ya kienyeji ni lazma awe na soko la familia pana Zaidi kuweza kupata faida ndogo, nasema faida ndogo maana ili kuzalisha mayai tray kumi (mayai 300) kwa siku, utahitaji Zaidi ya matetea 700 mpaka 1000 ya kienyeji pure. idadi ambayo ni kubwa kuliko idadi ya mayai yanayopatikana.
Biashara ya Nyama.
Na declare interest, mimi pia ni msambazaji wa nyama ya kuku wa kienyeji, hivyo naongea kwa uzoefu, na niko tayari kukosolewa. Pamoja na kufugwa katika misingi ya kijani (organic rearing), iyo pekee haitoshi kumpa thamani inayostahili huyu kuku sokoni. Thamani ya kuku sokoni ni uzito alio nao, organic component ni jambo la ziada lililo muhimu pia. tunavyo jadili bei ya soko ya kuku huyu ni lazma tumliganishe na gharama za bidhaa pinzani zilizoko sokoni. Haitawezekana kumuuza kuku mwenye kilo moja au pungufu kwa bei ambayo tunashawishiana humu ya 15000-20000 wakati bidhaa pinzani (nyama nyeupe) kama samaki sato toka mwanza wanauzwakwa 7500 kwa kilo, au kitimoto, numa ya ngombe ambazo nazo kilo ni 7500-8000. Hivyo basi. hoja yangu hapa ni uzito wa kuku husika. Ukiachana na jamii chache za kuku wa kienyeji (kuchi etc) wenye uzito mzuri, majority ya kuku pure wa asili/kienyeji kwa majogoo huwa na pungufu ya kilo moja na nusu. Kumbuka uzito wa kuku hawa sio kwasababu ya malisho duni, laah hasha, bali ni kutokana na vinasaba (genes) vyao kuwafanya kuwa na maumbo madogo madogo. kwa kuku wa aina hii, sitegemei mfugaji kama atafanikiwa kuwapeleka sokoni na kuweza kupata bei nzuri toka kwa mlaji wa mwisho.
Nini kifanyike.
ili ufugaji uwe wenye tija kibiashara ufanyike, ni lazma wafugaji tuamke na kuachana na ufugaji wa kuku hawa asilia kwani hawana tija. Nikisema hivi simaanishi watu waache kufuga, hapana, ila wafuge aina /breeds za kuku zenye tija kibiashara. Kuku pekee unaoweza kuwafuga kwa mbinu za kienyeji na bado wakakuletea mfugaji faida nzuri kibiashara, ni kuku aina ya chotara (cross breeds). hii ni aina ya kuku wenye sifa zote za ukienyeji kwa misingi ya mbinu zao za kuwafuga pamoja na namna walivyo nauwezo wa kuhimili mazingira hasa ya vijijini. Kuna aina mbalimbali ya kuku hawa ikiwamo Black/ white australorps, kroiller, Rhodes island red, red hamshire, Sussex etc. Hawa ni kuku ambao wanaserve purpose zote za mayai na za nyama. Mfano kuku aina ya black/white australorps wao wanauwezo wa kutaga mpaka mayai 250 kwa mwaka, tofauti na wa kienyeji, mayai ya kuku hawa huwa makubwa na yenye kasha jeupe na kiini cha njano kama utawafuga kwenye mazingira na mbinu asilia (za kienyeji). Ukilinganisha uwezo wa utagaji wa kuku hawa utagundua utagaji wao ni Zaidi ya asilimia 500% ukilinganisha na ule wa kienyeji pure. Idadi hii ya mayai toka kwa kuku mmoja kwa mwaka, anaweza kumwezesha mfugaji kuzalisha mayai kwa wingi na kushusha Zaidi bei ya mazao yake (mayai) kuwa chini kuweza kuliteka soko kwa urahisi Zaidi. Kumbuka, bei ya juu ya mayai ya kienyeji ni kwaajili ya kulipia gharama kubwa za utunzaji wa kuku huyu ilihali utagaji wake ni hafifu.
Pili, kuku hawa wana nyama nyingi Zaidi kuliko hawa wa kienyeji kwa majogoo hufikia mpaka uzito wa kilo 3-3.5. huku matetea hufikia kilo 2-2.5 na huwa na nyama nzuri, iliyokomaa vyema na yenye ladha. kwa uzito huu kwa majogoo, kuku hawa uuzwa kwa bei ya 20,000 - 25,000 wakiwa hai. bei ambayoni kwa mujibu wa bei ya soko kwa makadirio ya shilingi 8,000 kwa kilo kwa nyama nyeupe.
Mapungufu.
Pamoja na ubora wa kuku hawa katika ufugaji wa kibiashara, kuku hawa pia wanachangamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na uwezo wa kutamia. Pamoja na hii kuwa changamoto pia ni fursa kwani kwa yeye kutotamia kunamwongezea nafasi ya yeye kuendelea kutaga mara nyingi Zaidi bila kupumzika. hivyo changamoto hii ni faida kwa mfugaji anaelenga kufuga kwa tija. kwa vile mayai haya huwa yamerutubishwa na majogoo, nirahisi kwa mfugaji kuongeza idadi ya kuku kwa kupitia kutotolesha kwa mshine za kuangulia vifaranga au kumpa kuku mwingine ayatamie kwa niaba.
kwa ushauri Zaidi kuhusu shughuli za ufugaji, tuwasiliane kwa namba 0755815174. pia pata fursa kusoma ya Makala mbali na utaalamu kutoka kwenye mtandao wetu www.backyard.co.tz
Hahahahaaaaa...swali zuri sanaDu! Sikulijua hilo,kwa hiyo hata wakisasa nikimwacha ajitaftie chakula na dawa nisimpe anakuwa wa Kienyeji?
Asante kwa comment yenye akili: Watu wengi hawaelewi hili na wanadanganywa sana sana. Wanadhani kuku wa kienyeji ni yule anayetaga mayai madogo na ya rangi fulani. Lakini ukweli ni kwamba, kuku anakuwa wa kienyeji au wa kisasa kutokana na anavyofugwa. Wa kienyeji akifungiwa kama wa kisasa huyo ni wa kisasa. Wa kisasa akiachiwa ajitafutie huyo ni wa kienyeji.Kuku wa kienyeji ni yule anayejitafutia mwenyewe....kuku wa kienyeji ukimfungia ndani na kumpa chakula na madawa huyo ni "wakisasa"
Sidhani kama hii ndio tafsiri halisi ya kuku wa kienyeji na wa kisasa... mfumo wa ufugaji haibadilishi maana ya kuku wa kienyeji..hii ni sawa na kusema ukienda ulaya unakua mzunguAsante kwa comment yenye akili: Watu wengi hawaelewi hili na wanadanganywa sana sana. Wanadhani kuku wa kienyeji ni yule anayetaga mayai madogo na ya rangi fulani. Lakini ukweli ni kwamba, kuku anakuwa wa kienyeji au wa kisasa kutokana na anavyofugwa. Wa kienyeji akifungiwa kama wa kisasa huyo ni wa kisasa. Wa kisasa akiachiwa ajitafutie huyo ni wa kienyeji.
HII QUATATION IMENIGUSA lakini pia somo lako nimelielewa vema mkuu,popote uliko nakupa hongera"MWANAFUNZI anatakiwa asikilize,atafakari, achunguze na kudadisi na atoe maoni yake na sababu za maoni hayo.Kisomo ambacho kinamfanya mtu aone tabu kurudi vijijini si kisomo bali ni mapambo. Kupata shahada ni matokeo tu na si msingi wa elimu ya chuo kikuu " Julai 4 1977 Ibrahim Kaduma
Pengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.
Viko vitabu vingi na tena siku hizi zinatolewa DVD za jinsi ya kufanikiwa katika maisha. Utashangaa mpaka unamaliza kusoma au kutazama DVD hizo hujapata njia ya wazi sana sana utajilaumu tu kwa kuendelea kupoteza fedha kwa kuchangia miradi ya wajanja hao. Wengine wanakuambia "amini tu kuwa wewe ni tajiri na utafanikiwa" mh! INAWEZEKANA? Afadhali hao, balaa zaidi ni wale ambao wanayanadi mafanikikio na utajiri kwa mizizi, hirizi na hata roho za binadamu wenzao!
Somo langu ni dogo lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana. Sasa kuwa makini zaidi.
Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo. Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4 .
Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa makoo(majike) watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga. Utakuwa na kuku 200 + 25 =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700.
Ndugu mwanajamvi, hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000. Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku 1,000. Mwaka 2. 750(majike) x 10 = 7500 (uza wengine) 3000 x 10 = 30,000. Kutegemea na uwezo wako mpaka mwisho wa mwaka wa pili utakuwa umefanikiwa sana.
Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi huku ukiacha kando uzushi wa vitabu vya wasanii na DVD zao pia. NB. Kumbuka kuku ninao wazungumzia hapa ni wale wa kawaida sio wale mataahira (wa kisasa).Fuatilia zaidi kuhusu matibabu na matunzo mengineyo.
==============
MAELEZO ZAIDI:
UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI
SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI
Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kwa namna moja au nyingine kutoa mchango wangu kwa mtindo huu. Huu ni kama mwongozo tu wa nini utakabiliana nacho au unatakiwa kufanya katika zoezi zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji. Nimeamua kuuleta kwenu wana JF ili kwa mtu mwenye malengo ya kufanikiwa kupitia ufugaji wa kuku ajue mlolongo mzima na changamoto ambazo atakabiliana nazo.
A.KWA NINI KUKU WA KIENYEJI?
1. Wastahimilivu wa magonjwa lakini ni muhimu wakikingwa na magonjwa ya kuku kama mdondo, ndui ya kuku n.k ili kuweza kuwaendeleza.
2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini.
3. Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa na kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu kama ukame, baridi n.k
4.Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.(PATA SUPU YA KUKU WA KIENYEJI ILI UTHIBITISHE)
5. Wana uwezo wa kujilinda na maadui kama mwewe n.k . Pamoja na sifa hizi ni muhimu muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wakawekwa kwenye mabanda mazuri, wakapewa maji na chakula cha kutosha.
B.FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI.
Faida ni nyingi na zinafahamika lakini nitaeleza zile ambazo kwa wengine huenda zikawa ni ngeni kwao.
- Mayai huweza kutumika kwa tiba. (Pata maelezo jinsi yai la kuku wa kienyeji linavyoweza kutumika kwa tiba kutoka kwa wataalam wa tiba mbadala)
- Kiini cha njano cha yai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya nywele (shampoo)
- Manyoya yake yanaweza kutumika kama mapambo.
Fuga kuku upate faida kwa kuzingatia:
Chanjo ya mdondo kila baada ya miezi mitatu na chanjo ya ndui mara mbili kwa mwaka
Zuia viroboto, utitiri na minyoo.
Chagua mayai bora kwa ajili ya kuatamiza
Panga kuuza kuku kwa makundi uongeze kipato
Kula mayai na kuku kadri uzalishaji unavyoongezeka.
Kipato unachokipata utenge pia na kiasi kwa ajili ya uendelezaji wa kuku
C:MAPUNGUFU
Yako mapungufu mengi yanayofahamika lakini hapa naomba niweke lile la muhimu zaidi. MAGONJWA kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku kutokana na kutokuzingatia kuchanja kuku kwa wakati.
D: KABILA ZA KUKU WA KIENYEJI
Kuna maelezo ya kusisimua sana kuhusu makabila ya kuku wa kienyeji, hata hivyo kuna ugumu kidogo kuweza kuyachanganua makabila hayo kutokana na muingiliano mkubwa wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Hata hivyo kuku hawa wana tofauti za kimaumbile zinazosaidia kwa kiasi fulani kutambua uwepo wa baadhi ya makabila ya kuku. Kabila hizi pia zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na eneo kuku wanakotoka. Baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kwa maumbile yao Mfano:
a. Kishingo - kuku wasio na manyoya shingoni
b. Njachama au Nungunungu - Hawa ni wale wenye manyoya yaliyosimama.
c. Kibwenzi - Ni wale wenye manyoya mengi kichwani.
d. Kibutu- Hawa hawana manyoya mkiani
Mwingiliano wa vizazi unaweza ukasababisha kuku kuwa na aina ya maumbile mchanganyiko. Mfano kuku aina ya kuchi anaweza kuwa na alama ya kishingo, Njachama, Kibwenzi au Kibutu.
Hivyo kabila za kuku zifuatazo zinaweza kutambuliwa kama ndiyo kabila za kuku wa kienyeji kulingana na maumbile yao na maeneo wanakotoka.
(i) KUCHI
Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa Kg. 2.5 na mitetea kg 1.5 mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gm 45. Kuku hawa hupatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Zanzibar.
(ii) CHING'WEKWE
Kuku hawa ambao jina lao ni gumu kidogo kwa mtu asiyekuwa na meno kulitamka wana sifa zifuatazo.
Majogoo wana wastani wa kg 1.6, Mitetea wastani kg 1.2, mayai wastani wa gm 37. Kuku hawa wenye umbo dogo hupatikana zaidi maeneo ya CHAKWALE mkoani Morogoro na pia sehemu za umasaini. Kuku hawa hutaga mayai mengi sana kuliko aina nyingine ya kuku wa kienyeji waliopo Tanzania, kwa hiyo wanafaa sana kwa biashara ya mayai.
(iii)UMBO LA KATI
Majogoo wana uzito wa wastani wa kg. 1.9, Mitetea kg. 1.1, Kuku hawa ndio hasa wanaoitwa wa kienyeji(wa kawaida) Wana rangi tofauti. Utafiti umeonyesha kuwa kuku hawa hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa mdondo (Castle desease)
Muhimu - Mfugaji akifanya uchaguzi kutoka kwenye aina hii ya kuku na kutoa matunzo mazuri kwa hao kuku waliochaguliwa, Hakika anaweza kupata kuku walio bora na wenye uzito wa kutosha pia kutaga mayai mengi na makubwa.
(iv) SINGAMAGAZI
Ni aina ya kuku wakubwa wa kienyeji wanaopatikana zaidi TABORA, kuku hawa wana utambulisho maalum kutokana na rangi zao. Majogoo huwa na rangi ya moto na mitetea huwa na rangi ya nyuki. Uzito - Majogoo uzito wa wastani wa kg 2.9, mitetea wastani wa kilo 2 mayai gramu 56.
(iiv) MBEYA
Kuku hawa wanapatikana Ileje mkoani mbeya. Asili hasa ya kuku hawa ni kutoka nchi ya jirani ya Malawi na si wa kienyeji asilia bali wana damu ya kuku wa Kizungu "Black Australop". Majogoo Kg 3 mitetea kg 2 mayai gram 49
(iiiv)PEMBA
Hupatikana zaidi Pemba. Majogoo Kg.1.5 Mitetea Kg 1 mayai wastani gm 42
(xi) UNGUJA.
Majogoo Kg 1.6,mitetea kg 1.2 mayai gm 42. Kuku hawa wa Unguja na Pemba wanashabihiana sana na Kuchi isipokuwa hawa ni wadogo.
SEHEMU YA PILI
1. MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.
A. MFUMO HURIA
Katika mfumo huu kuku huachiwa wakitembea toka asubuhi wakijitafutia chakula na maji na kufungiwa kwenye vibanda visivyo rasmi wakati wa usiku. Huu ni mfumo rahisi lakini si nzuri kwa mfugaji wa kuku wengi kwani atahitaji eneo kubwa la ardhi.
FAIDA.
Mfumo huu una faida za gharama ndogo za uendeshaji kiujumla.
HASARA
Uwezekano mkubwa wa kuku kuliwa na vicheche, kuibiwa mitaani n.k
Kuku huweza kutaga popote na kusababisha upotevu mkubwa wa mayai.
Ni rahisi kuku kuambukizwa magonjwa
Utagaji unakuwa si nzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Uwekaji kumbukumbu si nzuri.
Ni vigumu kugundua kuku wagonjwa hivyo kusababisha ugumu katika utoaji wa tiba.
UTUMIAJI NZURI WA MFUMO HUU
Kuku wajengewe banda kwa ajili ya kulala nyakati za usiku na liwasaidie wakati mwingine wowote hali ya hewa inapokuwa si nzuri.
Kuku wapatiwe chakula cha ziada na maji.
Kuku waandaliwe kwa viota vya kutagia.
Kuku 100 ni vizuri wakitumia eneo la ardhi la ekari 1.
B.MFUMO NUSU HURIA
Huu ni mfumo ambao kuku hujengewa banda rasmi na banda hilo huzungushiwa uzio/ wigo. Mfumo huu ni ghari kiasi ukilinganisha na mfumo huria lakini huweza kumpatia mfugaji faida haraka sana.
FAIDA
Sehemu ndogo ya kufugia hutumika kuliko ufugaji huria, utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha na mfumo huria, Ni rahisi kutibu magonjwa ya mlipuka kama mdondo (Newcastle desease), Upotevu wa kuku na mayai ni mdogo sana ukilinganisha na mfumo huria.
C. MFUMO WA NDANI
Kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani. Mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa matandiko ya makapi ya mpunga, takataka za mbao(randa), maganda ya karanga au majani makavu yaliyokatwa katwa.
FAIDA
Mfumo huu unahitaji eneo dogo la kufugia, uangalizi mzuri na rahisi wa kuku, Joto litokanalo na matandiko lina uwezo wa kuua vimelea vya maradhi, kuku wanakingwa na hali ya hewa mbaya na maadui wengine.
HASARA
Uwezekano wa kuku kudonoana ni mkubw na pia Gharama za ujenzi wa mabanda
UTUMIAJI MZURI WA MFUMO HUU.
1. Matandiko yageuzwe kila siku
2. Kila mara matandiko yawe makavu kwa kuwa na madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha, ambayo yatatoa unyevunyevu hewa chafu ikiwemo ammonia.
4. Mita mraba moja hutosha kuku 5 hadi 8.
UTATUZI WA KUKABILIANA NA VIKWAZO KATIKA UFUGAJI.
Mambo ya kuzingatia:
Mabanda bora - Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.
Sifa za banda bora (Waone wataalam wa mifugo)
Kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi
Kuwa makini na aina ya mitetea na majogoo unatakiwa kuchagua ili kuwa na kizazi bora.
UTAGAJI WA MAYAI
Kwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho.
Hakikisha ya fuatayo.
Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.
UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji na uanguaji wa asili
KUCHAGUA MAYAI YA KUANGUA.
Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia yawe na sifa zifuatazo
Yasiwe na uchafu yawe masafi
Yasiwe na nyufa
Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo
Yasiwe madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
Yasiwe mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.
KUMTAYARISHA KUKU WA KUATAMIA
Pamoja na matayarisho hayo zingatia kumuwekea mayai yasiyozidi 15 pia ni vizuri yasipungue 12. Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa, utitiri n.k. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na kutotulia kwenye viota vyao. Hali hii husababisha kuanguliwa kwa Vifaranga wachache.
Sasa unatakiwa kufanya yafuatayo:-
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu ndani ya kiota
Pia mnyunyuzie dawa kuku anayetarajia kuatamia
Weka mayai kwenye kiota huku mikono yako ikiwa imepakwa jivu ili kuepuka kuwa na harufu kwani kuku anaweza kuyasusa.
Ni vizuri kuifanya kazi hii ya kumuandaa kuku anayetaka kuatamia wakati wa usiku. Pia ifahamike kuwa kwa kawaida kuku huatamia mayai yake siku 21.
PIA JIFUNZE MBINU ZA KUATAMIA MAYAI MENGI KWA NJIA ZA ASILI
Iwapo una kuku wengi wanaotaga kwa wakati mmoja ni vema ukawafanya wakaatamia na kutotoa pamoja.
Unachotakiwa kufanya ni kuchagua mayai ya kuatamia ukianzia na yai la mwisho kutaga.
Unaweza kuwaandaa kuku wako zaidi ya mmoja ili waanze kuatamia kwa pamoja na kupata vifaranga vingi kwa mara moja kuku wa kwanza anapoanza kuatamia. Mwekee mayai viza au ya kuku wa kisasa kwani kuku huatamia hadi mayai yanapoanguliwa hivyo ukimuwekea mayai yasiyo na mbegu atakaa hapo muda mrefu hadi vifaranga watoke.
UTEKELEZAJI WAKE
Kuku anapotaga kila siku weka alama ya namba au tarehe kulinganisha na siku anayotaga
Yanapofika mayai matatu yaondoe na muwekee mayai viza au ya kisasa huku ukiendelea kuweka alama mayai yanayotagwa kila siku.
Mara kuku anapoanza kuatamia muongezee mayai ya uongo yafikie 8 hadi 10
Fanya hivyo kwa kila kuku anayetaga hadi utakapoweza kupata idadi itakayoweza kukupatia vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
Wawekee kuku wote mayai siku moja kwa kuondoa mayai ya uongo na kuwawekea mayai ya ukweli wakati wa usiku.
MUHIMU
Mayai ya kuatamia yasishikwe kwa mkono ulio wazi na wala yasipate harufu za mafuta ya taa, manukato n.k.
JIFUNZE PIA KUTAMBUA MAYAI YALIYO NA MBEGU NA YALE YASUYO NA MBEGU.
Mfugaji anaweza kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasiyo na mbegu siku ya saba baada ya kuanza kuatamia iwapo atapima mayai kwa kutumia box lililotengenezwa maalum pamoja na tochi yenye mwanga mkali ndani ya chumba chenye kiza. Hii itamuwezesha mfugaji ayatumie mayai yasiyo na mbegu kwa chakula cha familia au kuyauza.
TAMBUA VYAKULA NA UZALISHAJI WA KUKU - Sitalielezea hili naomba ufuatilie mwenyewe.
JIFUNZE MBINU ZA KUZALISHA KUKU WENGI KWA MUDA MFUPI
Zoezi hili linawezekana iwapo uleaji wa vifaranga kwa njia ya kubuni utatumika. Kuku mmoja anaweza kutotoa zaidi ya mara saba kwa mwaka.
Taz.
Hesabu ya uzalishaji wa kuku wengi kwa mwaka kwa kutumia mtetea mmoja tu.
Mpaka mwisho wa mwaka unaweza kuwa na idadi ya vifaranga 252 kwa kadirio la vifaranga 8 kila mzao. Hivyo kama una kuku 10 wanaotunzwa vizuri utakuwa umezalisha jumla ya vifaranga 2520.
Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo ili ufundishwe zaidi kuhusu mbinu hiyo ya kuzalisha kuku wengi.
ULEAJI WA VIFARANGA
NJIA YA KUBUNI
NJIA YA ASILI
Njia zote mbili zinafahamika kama huzifahamu tafadhali fuatilia kwa mtaalamu aliye karibu nawe.
MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA KUKU WA KIENYEJI NA JINSI YA KUKINGA.
A. MAGONJWA.
Ugonjwa hatari - Mdondo/ Kideri (Newcastle desease) Hapo nyuma dawa ya kukinga ugonjwa huu ilikuwepo lakini ilikuwa inahitaji kuhifadhiwa kwenye hali ya ubaridi (Friji) Hali hiyo ilisababisha iwe ngumu kutumika vijijini kwa dawa hiyo. Hivi sasa kumepatikana chanjoa ambayo inastahimili joto ambayo inaweza kutumika hata vijijini.
Pamoja na mdondo yapo pia magonjwa yanayoshambulia kuku hapa nchini
Ndui ya kuku(Fowl pox)
Mafua ya kuku(Infectious coryza)
Homa ya matumbo (Cocciodiosis)
Minyoo na wadudu kama viroboto, chawa, utitiri na kupe wa kuku.
DALILI ZA KUKU MGONJWA.
Huzubaa
Hali chakula/maji vizuri
Hujitenga na wenzake
Hujikunyata au kuinama
Hutetemeka
Hutembea kwa shida
Utagaji wa mayai hupungua au hukoma kabisa
MAGONJWA YA KUKU HUSABABISHWA NA NINI?
Yako mambo mengi yanayosababisha lakini matunzo hafifu pia huchangia.
ATHARI ZA MAGONJWA.
Hili liko wazi
Maelezo haya ya magonjwa ni mengi hivyo tuwe wafuatiliaji kwa wataalam.
MATIBABU
KIDERI - Sifahamu tiba ya kitaalam ya ugonjwa huu kama kuna ambaye anafahamu tunaomba atufahamishe lakini ziko dawa za asili na za kitaalam ambazo zinafaa zaidi kwa chanjo.
Ugonjwa huu unaweza kuukinga kwa kuwapa kuku chanjo ya Mdondo. Pia usichanganye kuku wako na kuku ambao huna taarifa zao za chanjo.
KUMBUKA
Mdondo au kideri ni ugonjwa tishio ambao huweza kuua kuku wote
Mdondo ukitokea vifo huwa vingi pia kuku hupumua kwa taabu, hupooza na wengine huzunguka na huzungusha vichwa.
Mdondo unaweza kuzuilika kwa chanjo kila baada ya miezi 3
NDUI YA KUKU
HOMA YA MATUMBO (Fowly typhoid)
MAFUA YA KUKU(Infectious coryzya)
KUHARISHA DAMU(Coccidiosis)
Minyoo na wadudu wanaoshambulia kuku kama viroboto n.k
Kwa magonjwa na wadudu tuliowataja hapo juu please wasiliana na mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe Kwani siwezi kueleza kila kitu hapa wataalamu tunao naamini watatusaidia.
TIBA ZA ASILI
Kuna madawa ya asili ambayo hutokana na mimea ambayo hukinga kuku.
BAADHI YA MIMEA INAYOTIBU NA KUKINGA MARADHI YA KUKU.
MWAROBAINI - Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda
ALOEVERA - Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda,ngozi na Cholera. Tutaelekezana zaidi namna ya kuandaa dawa hii.
Hapa nataka niorodheshe baadhi ya madawa ya asili ambayo yanasaidia kutibu na kukinga kuku.
Mwarobaini, Aloevera, Mtakalang'onyo(Euphorbia),Mbarika, mlonge, Ndulele/dungurusi/tura/ndura, Majani ya mpapai, Mwembe, Minyaa na Pilipili kichaa.
NAWASHUKURU PIA NAOMBA MWENYE MCHANGO ZAIDI AENDELEE KUONGEZEA TUSIWE WACHOYO WA MAARIFA KIDOGO GAWANA NA MWENZIO
hamna shida hata hapa tunaweza kuwasiliana vizuri na ple kwa late reply.. kuhusuhiyo mashine ya mayai 48 unaweza kupiga sim namba 0754 467423 na ukapata ufafanuzi na maelez mazuri,,.Ahsantee kwa ufafanuzi uluosimama kuhusu kutotolesha mayai ya siku saba inawezekana kupata vifaranga vingapi kwa trei moja na bei ya incubator hiyo ya mayai 48 maana bado mtaji mdogo kwa kweli ningekua naku-pm ila bado sina uzoefu na hii app