Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

habari wakuu, kama topik isemavyo hapo juu....siku za karibuni kumeibuka watu mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii wakinadi aina mbali mbali za kuku wa kienyeji/chotara kwa biashara ya mayai, najua humu kuna watu washajaribu hizo aina tofauti basi ni vyema tukashea ujuzi/matokeo ya tafiti zenu kutokana na walivo-perfom kwenye soko la mayai.

pia ni vyema kama mtatufahamisha wapi pakupata mbegu bora grade one sio mchakachuo ili tusije lia kwenye biashara.

mi nilishasikia majina kama kuroiler,sasso,tabora,malawi etc,

ni tumaini langu mtatusaidie sie wafugaji/wajasiriamali chipukizi kwa ushauri wenu.

mbaki salama, na heri ya christmass na mwaka mpya.
 
Ndugu yangu wafugaji wa humu
Ni miyeyusho tuu
Wanaongea sana wakati hata hawafugi
 
 

Mm nna mbegu mchanganyiko tu,kuroiler,rhode island,kuchi na wa malawi aka australop,sina takwimu sahihi za utagaji lkn naweza kusema hawajawahi kuniangusha.

Kuhusu mbegu grade 1 sina hakika km unwz kupata tanzania,na nakushauri usitafute cuz utakutana na matapeli tu wanaojifanya wanauza kuroiler pure kwa bei kubwa kumbe sio kuroiler,la muhimu nunua kwa mtu unayemwamini kuwa anazingatia line-breeding na sio in-breeding.
 

asante kwa kua honest, mimi nligundua wengi wanaojitangaza especially aina ya kuroiler sio pure jamaa yangu aliingia kichwa kichwa unakuta ni 3rd/4th generation hata wakienyeji wanawapita kutaga, sasa mkuu vipi bei ya mayai ya hao malawi je unauza bei sawa na kienyeji au bei ndogo...? i mean unapouza sokoni unayauza kama ya kuku wa kienyeji 12k/15k kwa trei ama unauza kama ya hawa broiler 7k?? nataka kujua thamani yake sokoni.
 

Mm sijalenga kuuza mayai,nauza vifaranga,mayai hailipi.Naona kama unataka kuuza mayai bora ufuge layers wa kisasa.
 
Mm sijalenga kuuza mayai,nauza vifaranga,mayai hailipi.Naona kama unataka kuuza mayai bora ufuge layers wa kisasa.

ni kweli lengo langu ni kuuza mayai zaidi, vifaranga i think inahitaji mtaji mkubwa zaidi wa mashine ya kutotolesha na mtandao wa kuuza hivo vifaranga kwa wafugaji wapya, bahati mbaya kutokana na nature ya mazingira yangu naona kama kuuza vifaranga itaniwia vigumu kuliko kuuza mayai. kwanini unasema hailipi mkuu wakati naona mayai ya kienyeji yanauzwa bei ghali kuliko hayo ya kisasa?
 

Sio mbaya,km una soko uhakika la mayai,kuku chotara km rhode island ni wazuri kwa mayai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…