Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Nimesoma maelezo yenu ama kwa hakika yamenivutia nilikuwa na uvivu wa kuanza kufuga sasa mmenipa moyo wa kuanza.ningependa kuwa na mtiririko mzuri wa kuandika ili iwe rahisi kwa msomaji aweze kupata elimu kwa ufasaha!ila nimefaidika sana kwani kuna ucheshi ndani yake na pia elimu kubwa zaidi kwa moyo huu tutafika mbali sasa ni vitendo vinahitajika.naanza na matayarisho ya banda kwanza ahsanteni.
 
Karibu mkuu,
kuku wa kizungu athari zake kiafya ni nyingi kuliko wa kienyeji,unaweza kufuga wa kizungu kwa ajili ya pesa na wa kienyeji kwa ajili ya afya yako 🙂
 
Asante sana for sharing, swali lang; Je kuku mmjoa anaweza kutaga mayai mangapi kwa mwezi?

 
Karibu mkuu,
kuku wa kizungu athari zake kiafya ni nyingi kuliko wa kienyeji,unaweza kufuga wa kizungu kwa ajili ya pesa na wa kienyeji kwa ajili ya afya yako 🙂
sikutegemea mtu mzoefu kama wewe Newmzalendo utoe post iliyo general kama hii... hebu tupe sababu za kisayansi kusema kuwa kama unataka kufuga kuku kwa ajili ya afya ufuge wa kienyeji tu na wa kisasa ni kwa ajili ya pesa... si vizuri kutoa general statement zinazopotosha kwa sababu watu wengi wanasoma JF.
 

ha haa haaa haaaa

sijui niwe upande upi hapa. .., labda tujiulize swali moja, kuku wa kisasa hufugwa kwa muda wa hadi kuanzia wiki saba na kuwa tayari kwa matumizi na kuku wa kienyeji hufugwa kwa hadi wiki 20 , je tofauti hii ya muda maana yake ni nini kisayansi?
 

wanajamvi, ni muhimu kufahamu kuwa katika ufugaji ni lazima uzingatie ufugaji bora kama unataka kulinda afya za walaji iwe umefuga kienyeji au kizungu au kisasa. unachotakiwa kuzingatia ni wakati gani unawapa kuku wako dawa, na upite muda gani kabla ya kutumia product za hao kuku (i.e. mayai na nyama). kila dawa inakuwa na maelezo ya muda unaotakiwa upite kabla ya kuchinja au kutumia mayai endapo utakuwa umewapa hiyo dawa.

Na katika ufugaji wowote wa kuku lazima utakinga na/au kutibu magonjwa iwe ni kuku wa kienyeji au wa kisasa. lazima utawakinga au kuwatibu dhidi ya kideri/mdondo, ndui, homa ya matumbo, gumboro, mafua n.k.

kwa ufupi, kinacho-matter si aina ya kuku ulionao (kienyeji/kisasa) bali ni utaratibu/mbinu gani unatumia katika ufugaji wa kuku wako (i.e. practices).

nawashauri wanajamvi msidhani kuwa kwa kuwa kuku ni wa kienyeji basi ni bora kwa afya- bila kujua kuwa kuku huyo anaweza kuwa na ugonjwa au amepewa dawa siku za karibuni. the same applies kwa kuku wa kisasa!
 
<br />
<br />
Vipi kuhusu suala la ladha? Kuku wapi ni watamu waidi?
 
Reactions: LAT
Naomba kujua uwezo wa kutaga wa kuku wa kienyeji uko vp? I mean ni mayai mangapi labda kwa muda gani? Nasikia kuku wa kienyeji akiwa anataga na unayatoa mayai haumpi kuyaatamia anaendelea tu kutaga bila kuacha ni kweli au maneno ya mtaani tu?
kwa mtago mmoja kuku anataga mayai 10-15 na wengine wanataga mpaka mayai 20. Kwa hiyo kwa mwaka anaweza kutaga mpaka mayai 45......Inawezekana kabisa kuku akaendelea kutaga pale unapompokonya mayai asiyaatamie, lakini pia kuna njia nyingine ya kienyeji niliwahi ikuta kijijini kumzuia kuku asiatamie mayai, ambapo alikuwa anawekwa kwenye maji, hasa sehemu ile ya kifua....
 

kweli Jf ni shule
 
Wana JF

Msaada wenu unahitajika katika hivi vitu viwili

1. Kuku wangu wa kienyeji nafugia ndani (siyo huria), wameanza kutaga ila mayai yao yanafanana sana na ya kuku wa kisasa wa mayai. Inaniletea tatizo kupata wateja wanahisi ni ya kisasa. tatizo lipo wapi?

2. Nitapata wapi mashine ndogo ya kutotolesha ya kutosha mayai kati ya 30 hadi mia?


Asanteni sana
 

Elnino, nimeipenda sana hii coment yako, nashukuru kwa kutufumbua macho mana hata nami nina wazo hili la kufuga, ila sikujua nianzaje! Endelea kutuelemisha zaidi!
 
Karibu mkuu,
kuku wa kizungu athari zake kiafya ni nyingi kuliko wa kienyeji,unaweza kufuga wa kizungu kwa ajili ya pesa na wa kienyeji kwa ajili ya afya yako 🙂

Kimaadili ya kiubinadamu na kibiashara ni muhimu kuzingatia afya ya walaji/wateja na sio kupata pesa tu.......ni mtazamo tu!
 
Hii nzuri sana sijui kwanini haijawekwa kule juu tukafaidi maana nimechelewa
kuiona. Tunaomba muiweke juu kwa faida ya wengine pia.
 
Nimesikia kuku wa kisasa ukiwapa maji yenye ARV zinawanenepesha kweli kweli
 
Imetulia ....kilichobaki ni utekelezaji tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…