ELNIN0
JF-Expert Member
- Nov 26, 2009
- 4,161
- 1,476
Mkuu Kanyagio, umenivunja mbavu jioni ya leo, Elnino amejikita ktk ufugaji wa Mayai. na kilimo cha mahindi alipoanza kilinitia moyo nami nikaanza kuota ndoto za kulima mahindi,nadhani sasa atakuwa akivuna na kutengeneza chakula cha kuku wa mayai
Wakuu, ni vugumu kutenganisha kilimo na ufugaji, kwa mafano kwenye ile formulla ya Kuku wa mayai unaona kabisa mahindi ni kilo 500 katika kila tani. soko la sasa hapa dar kilo ni sh 490 - jumla ni Tshs. 245,000.
Sasa mimi badala ya kununua haya mahidi ninaji - supply mwenyewe. Kifupi bado nafanya Kilimo na ufugaji kwa pamoja. Kilimo changu pia kinaendana sambamba na ujasiliamali kwamba wakati wa mavuno pia nanunua mazao toka kwa wakulima wenzangu na kuweka kwenye stoo zangu, ampamo chakula hiki hutumia kulishia mifugo yangu.