Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

I am impressed ngoja na mmi nije na mradi wangu hapa muuchakachue. All the best guys!
 
New mzalendo Nitafute nikupe ushauri mambo ni mengi pia mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji soko lipo kubwa sana unatakiwa tu kujua undani wake. But it seems you are not serious hako kajogoo kamoja utafika nako weapi au unaogopa risk? nipigie 0755394701 tuongee mkuu

mkuu kwanini usitusaidie wengi badala yake akupigie simu ili umpe maujanja pekeyake?
 
Cheki hiyo imeisha leo - nimefunga mahesabu yangu ya mwezi huu.
ndugu inaonekana hii biashara ni nzuri nahitaji mafunzo zaidi nami niingie huko!kuna kitu pia nimekiona kuhusu bei ya mafuta ya generator kuwa inakwenda tsh 1600!ulikuwa unanunulia wapi?au haya mahesabu ni mwaka jana?
 
Mi siisha Dar, lakini nakushauri uifanye hiyo kazi mwenyewe na sio kuweka kijana/vijana wa kukufanyia kazi. Kwa sababu we ndo unaanza ninakushauri hivyo kwa sababu ufugaji wa kuku wa kienyeji una faida kubwa sana kwa sababu watu wamepunguza sana ulaji wa kuku wa kisasa. Kuku wanahitaji muda mwingi sana wa kuwahudumia, kuna mambo ya chanjo (vaccination regime) ya ugonjwa wa kideri ambao huua sana kuku, hii hufanywa kwa kila kuku kwa kipindi cha kila miezi 3, sasa ukiwa na kuku kama 400 tu halafu unamuagiza kijana awachanje, mara nyingi hurashia rashia na hatimae kukutia hasara. vile vile malezi ya vifaranga ambao utawatengenezea utaratibu wa kuzaliwa kwa wakati mmoja,hawa huhitaji uangalizi wa karibu sana kwa sababu hawalelewi na mama zao ili uwape uwezo mama zao wa kutaga mapema zaidi.
Kazi unayo mwana JF lakini nakusisitizia mradi huo ni mzuri.Weka bidii na zingatia ushauri utatoka.
 
mmmh tafuta miteea kwanza chotara ambayo ni mikubwa kwa umbo pia yanatoa mayai mengi so ni rahisi kupata maendeleo ya haraka
 
mkuu asante sana, nitapm sasa hivi, maana hii ya kungoja kuku sijui wawili wakue naona inachukua muda sana na ukiangalia mortality yao hadi kufikia kuku walau mia itachukua muda sana, na wazo la incubator zuri zaidi.

hongera sana mkuu, labda mimi kwa kukusaidia nikupe namba ya mtu fulani wa dodoma anatengeneza incubeter nzuri sana kama utataka lakini
 
mi ninao 40 wakubwa na vifaranga 48 - nasogea sogea .
Hongera sana Fuso. Hiyo ni hatua kubwa, ukilinganisha na mimi ambaye ndo kwanza nina wakubwa 6 na vifaranga 5. Vilikuwa 9 lakini 4 vimeliwa na paka. Hata hivyo sikati tamaa, nina mpango wa kuongeza kuku wakubwa ili nisonge mbele - polepole ndio mwendo, nitafika tu.
 
Jamani huu ni mradi mzuri sana nina wazo la kuanzsha kwa muda mrefu lakini nimekosa site kwani naishi ktk nyumba ya kupanga na niko Ar, je nifanyeje?
 
Ni mradi tosha kbs kokote ulipo,Swali langu! Mbona nikiwapa kuku watamie km mayai kumi na3 wanaweza angua 10 ama 8 na hao vifanga ktk siku kadha wanaweza wakasinzia na kuanza kushusha mabawa na hatimaye ni kufa,Je? Mwenye kujua dawa anijuze wajameni juzi tu kuku 2 wameangua zaidi ya vifaranga 18 lakini wote wamekufa.
 
Mimi nimeipenda sana hii biashara nyumbani kwangu mbezi nimeanz na kuku 38 inclusive majogoo 3 nilikuwa nawafungulia wajitafutie chakula wenyewe kwa siku nilikuwa nafunga mayai 15 minimum 10 majiran wakaanza kuniwangia hoo kuku wang wanaharibu mashamba yao bas nikawafungia hawakutaga ten,sasa hiv niko kwenye process ya kuzungusha ukuta fence nianze kuwafungua tena
 
Ni mradi tosha kbs kokote ulipo,Swali langu! Mbona nikiwapa kuku watamie km mayai kumi na3 wanaweza angua 10 ama 8 na hao vifanga ktk siku kadha wanaweza wakasinzia na kuanza kushusha mabawa na hatimaye ni kufa,Je? Mwenye kujua dawa anijuze wajameni juzi tu kuku 2 wameangua zaidi ya vifaranga 18 lakini wote wamekufa.

Sababu za hali hiyo zinaweza kuwa chochote kati ya hivi;
1. ilitakiwa siku za mwanzo ndani ya week uwapatie OTC plus au any vitamin
2. Sehemu wanayolala sio kavu kuku hawataki unyevu
3. Chakula unachowalisha kinakosa virutubisho vwa kutosha

Na kuhusu uanguaji angalia aina na umbo la kuku mwenyewe. Kuna kuku especially cross breed ya kienyeji na za kutoka nje wanataga mayai mengi ila sio hodari wa kulalia. Pia kama kuku ana umbo dogo mpe mayai machache alalie yasizidi kumi, mengine uza ama kula na familia.
 
Hongera sana Fuso. Hiyo ni hatua kubwa, ukilinganisha na mimi ambaye ndo kwanza nina wakubwa 6 na vifaranga 5. Vilikuwa 9 lakini 4 vimeliwa na paka. Hata hivyo sikati tamaa, nina mpango wa kuongeza kuku wakubwa ili nisonge mbele - polepole ndio mwendo, nitafika tu.

Maamuma,
pole sana imarisha banda ili kuzuia mbwa, vicheche na paka wasiingie. Tatizo sugu ni wezi wa kuku mimi nimeibiwa majooo sita ya mbegu, ndio nilikuwa nayatumia kwa ajili ya ku cross breed. Wameniibia Pure Kuchi mmoja, Rhode Island red moja, Half cast ya Kuchi na kienyeji moja, mbegu ya malawi (ile nyeusi moja), Pure kienyeji mawili. Jamaa waliruka fence na kuvunja banda cha ajabu katika mchanganyiko wa kuku wakabeba jogoo peke yake, majike yote yakabaki (Kati ya kuku 338 jamaa wakaweza kuchagua hao 6 tu). Nahisi ni mtu anayefahamu mazingira ya hapa kwangu
 
pole sana mkuu

je bora wangeiba wababa au wamama?
 
safi! kama tatizo sio mtaji basi fuga kuku wa kisasa utanyanyuka kwa haraka na pia utaona nini unafanya! Kuku wa kienyeji ni mradi mzuri ila unachukua muda mrefu kidogo
 
nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji,bado sija survey soko la kuku wa kienyeji likoje,kama kuna mtu mwenye uzoefu na hili anishauri ,pros and cons etc.bye the way nimeanza na Jogoo mmoja,ila natarajia kuongeza kuku within a week,projections ni kuwa na kuku 1000,hapo ndio nianze kuuza,matarajio yangu ni kuuza via interent-hapa nalenga watu wa DAR,ambao wako bize,i can do delivery maofisini within city center,na baadae kuweka vituo vya kufanya pickup wakati watu wanarudi home jioni,e.g mwenge junction,morroco petrol station,etc,malipo via M-pesa,sms banking pia na mahoteli.sitarajii faida ya haraka ,naomba ushauri kwa wale walifanya biashara hii,au wanajua mtu wa karibu aliyeifanya.
its nice
 
Wadau natafuta vifaranga/kuku wa kienyeji ambao ni bora kwa ajili ya kufuga. Kwa aliye nao/mwenye kujua wanapatikana wapi naomba anipatie contact wapi wanapatikana kwa maeneo ya Dar au mikoa ya jirani na Dar.
 
yani nimefurahia sana hii thread, maana na mim nipo mbioni kuanza kufuga kuku, ila sijaamua nifuge wa aina gani. bado nasoma na kujifunza kwanza ili nisiingie kichwa kichwa. asanteni sana na mungu awabariki
 
Back
Top Bottom