Nina uzoefu mdogo katika hili. Nilienda nikanunua majike 10 ya kienyeji, kwa nyakati tofauti nikawafungia bandani kwa kuwapa mchanganyo wa pumba, mashudu, dagaa na vingine kama vinavyoelezwa kwenye majalida ya Ufugaji.
Kuna jike aliyekuwa akiwa anataga, na aliendelea kwa siku 5 kisha akaacha, wengine kama 4 hivi wakaanza kutaga, akitaga Leo anakaa wiki anataga tena, hali hiyo ilidumu kwa miezi mitatu, hakuna wa kutaga mfululizo hata kwa siku 2 wala wa kuhatamia.
Nikapata hasira nikawafungulia, kwa maana nikawaacha wazurure, wiki moja tangu kuwaachia huru, yule alikuja anataga most ezi mitatu iliyopita akaanza kutaga mfululizo, imepita wiki moja tena wengine watano wakaanza kutaga kwa pamoja na mfululizo na wakahatamia na kutotoa!
Ushauri wa kuwapa majani na kuwaachia nje ndani ya uzio japo kwa jioni au Masaa machache kwa siku ili kufanya mazoezi inaweza kukusaidia.