Habari wanajamvi na poleni kwa uchovu wa pasaka. bila kuchelewa turudi tena kwenye mada yetu.
kipomo cha chakula cha hao kuku wanao tafuta umri wa miezi miwili kwa siku huwa nawapa gm4/kuku kwa wiki ya kwanza na pili kwa wiki ya tatu na ya nne na wapa gm4.5/kuku.mfano nina kuku labda 20 kama ni wiki ya kwanza nita wapa gm80 kwa siku.
Ulishaji wa hawa kuku huwa nitofauti kidogo na vifaranga wadogo.vifaranga wadogo nawawekea chakula wanakula muda wote usiku na mchana ila kwa hawa wakubwa nagawa share ya chakula ya siku hiyo katika nusu mbili,nusu moja nawapa wale asubuhi wakimaliza hicho chakula siwapi iliyobaki kwa muda huo pia siwaachi wakae bila kula ninacho fanya nachukua chakula chochote nafuu nawaning'inizia waendelee kudonoa taratibu hadi mida ya saa tisa hapo nawawekea nusu nyingine wamalizie mgao wa siku.chakula cha kuning'iniza kinaweza kikawa kabichi nzima,mboga za majani,majani mf.michunga,matikiti pori yaliyo katwa vipande nk.