Wakuu mwaka 2018 naona ni mwaka wa Baraka kwangu kwa macho ya rohoni.. Maana mwaka 2017 nilijaribu kufuga kuku wachache kwa majaribio kwa kiasi flan nikajua nini nifanye.. Lakini nilikumbwa na changamoto hizi zifuatazo..
1.ugonjwa WA ndui kwa vifaranga.hapa vifaranga sijajua nitumie dawa gani ili wasipate zile ndui ama vijipu flani machoni
2.namna ya kuchanganya vyakula vya kuku kulingana na umri... Yan formula sina kwa vifaranga na kuku wakubwa
3.namna ya kuvilea vifaranga mara baada tuu ya kutotolewa na Mama yao.. Maana vilikufa vifaranga zaidi ya 80 kwa mpigo kuna kitu nkajifunza.. (I) kutochanganya vifaranga wenye umri tofauti maana wanang'atana (II) dawa maalumu ya ndui naomba nijue
MALENGO
1.nimepanga nifuge kuku 100 tetea wenye umri sawa na jogoo 10 WAKUBWA (mbegu bora)... Tatzo lipo kwenye aina ya kuku wa kufuga wanao kua haraka na kutaga sanaa vile vile wenye umbo kubwaa
2.nivune kuku wangu 2018 kipindi cha mwaka mpya na Christmas maana nime assume tetea 100 kila mmoja ata totoa vifaranga 10+ hvyo wakitotoa wote ntakua na kuku 1000.. Hili nimelifanyia jaribio nimeona kabisa naweza maana kuku mmoja aliweza totoa hadi vifaranga 13
3.kuuza mayai, mbolea ya kuku,
4.kununua incubator baada ya mavuno ya kuku
5.kufungua kiwanda cha kuuza vyakula vya kuku pamoja na madawa ya kuku baada ya kupata uzoefu...maana na assume baada ya muda ntakua nauza vifaranga maana ntakua na incubator hvyo Wateja wangu hao wananiungisha hvyo vyakula na madawa..
NAONA MAFANIKIO MAKUBWA MBELE YANGU LAKINI CHANGAMOTO YA VIFARANGA INANIPA SHIDA NAOMBA SHULE...
Dawa niliokua natumia kwa kuku wakuba ilikua
1.newcastle
2.gomboro
Kama kuna dawa nyingine naomba nieleweshwe...
NIMEDHAMIRIA NA NAWEZA FANYA
nawasilisha kwenu wakuu ushauri napokea
Vyakula Special bei iko hiviMkwere Sumbawanga Au kinundu
Ila bei ya chakula yasumbuwa, yala faida yote...
Wenzetu tutajieni bei za Starter 50kg
Bei ya Grower 50kg
Na
Bei ya finisher nayo 50kg?
Please
Kwa Broilers..Vyakula Special bei iko hivi
Layers-45,000/=
Growers-48,000/=
Broiler-55,000/=
Ila pia waweza kufanya kuchanganya mwenyewe kama wajua formula
Naona mtandao hauko vizuri nita upload muda sio mrefuKazi ufugaji kuku yahitaji moyo, kwa ujumla kitu cha msingi katika ufagaji wa kuku ni:-
1.Usafi wa banda lako au maeneo wanayoishi.
2.Kinga na tiba ya magonjwa mbalimbali, jitahidi usiruhu kifo cha kifaranga kitokee na kikitokea chukua tahadhari ya kuwatibu mapema vifaranga vyako
3.Lishe kwa kuwapatia vyakula vilivyoshauriwa kwa kila umri na kama unajitengenezea ufaute uwiano wa kitaalam
Mwisho kuna nyuzi nyingi za ufugaji humu upitie, na hapo chini nimekupatia jarida la Mwongozo wa Ufugaji wa kuku wa kienyeji ukipenda ulisome kwa makini litakusaidia katika mafanikio yako ya 2018,
Litume mkuu...Naona mtandao hauko vizuri nita upload muda sio mrefu
Broiler starter 55,000/=Kwa Broilers..
Starter?
Finisher?
Juju walk hawafi mkuu?Walipotaga waliatamia 2 tu na wakawalea wao, mwingine akabaki na jogoo sikuwa hata na banda kubwa, wakakua 30 mara 3, nikawa na kuku 90 ndo nikajenga banda, ilichukua muda mrefu lakini, niliuza majogoo nikabakisha 5 jike 50, ndo nikaanza kufuga kibiashara, Sasa hivi natotolesha mara 1 kwa miezi 2, muda mwingi nauza mayai, kwa kweli nilianza kikawaida sana bila gharama kubwa, huu mwaka wa 5 sasa
Hilo group halifanyi kaziUFUGAJI WA KUKU
click [emoji115][emoji115]hiyo link ili uweze kujiunga kwenye hilo group la wafuga kuku
share kwa watu wote wanao fuga kuku
Mkuu nipe link la group0766728326. Naomba uniunge mkuu.
Hao vichepere unawapataje?Nimevitiwa sana mimi mwaka jana nikuwa nafuga hawa wa mitandao koroiler wanaitwa. Nilisoota sana wanamagonjwa kila kukicha, wanakula kaa wanahama, hayana habari na kutamia. Nikawauza december, nikaanza kununua pure kienyeji waswahili wanaita chep4ere wanapedwa sana kwa biashara niligundua nilipofika soko la chogo handeni nikiwa mgeni kabisa mji huu na koroiler wangu kuuza. Hapa wachuuzi toka dar ni makumi wengi mno. Nilipata wakati mgumu kwani wengi waliwaita wa kisasa na kusema nyama yao sii nzuri ka ya kienyeji. Wenye vichepere waliuza vyote hadi alipoingia mkenge tajiri mmoja wa sheli akinuwia kufuga akanunua kwa jumla bei sawa na pungufu kidogo kwa kienyeji.
Niliporudi kazi ilikuwa kutafuta chepere hadi february nilikuwa na mitetea 80 mwezi wa sita wakaanza kutaga, wasaba mwishoni nikaanza kuwaatamisha hadi niandikapo nina vifaranga wa umri tofauti 412. Nimejifunza kuku wa kienyeji ni encubator tosha, ni ngumu kuugua, garama za chakula ni ndogo sana na soko ni kubwa lao mno. Fuga kienyeji hata ukikosa hela ya chakula hujiokotea wenyewe wakisubiri upata haya mengine utaumia.
Ufugaji changamoto hakunaga kitu rahisiDah..mnatuchanganya kwelikweli......
USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija
Upo mkoa gani bossWakuu mwaka 2018 naona ni mwaka wa Baraka kwangu kwa macho ya rohoni.. Maana mwaka 2017 nilijaribu kufuga kuku wachache kwa majaribio kwa kiasi flan nikajua nini nifanye.. Lakini nilikumbwa na changamoto hizi zifuatazo..