Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

hangera kwa hapo ulipofika.....pole kwa kupoteza kuku 80.

ndui ya kuku ni miongoni mwamagonjwa yanayo sababishwa na viruses na huwa hayana tiba ili kuepuka ndui nakushauri uwape chanjo ya ndui kuku wako Mara tu wanapo timiza miezi miwili,hakikisha chanjo unanunua kwa wauzaji wanao aminika ili usije uziwa chanjo fake au iliyokwisha muda wake.

pia uwe makini kuna ugonjwa unafanana na ndui kiasi fulani na wengi wanachanganya na ndui,ugonjwa huo ubasababishwa na kuku kukosa vitamini A huu ugonjwa unatibika kwa kuwapa kuku vitamini A pia na kutibu vidonda na macho kwa kutumia ayodini,maji ya vuguvugu yaliyochanganywa na chumvi pamoja na mafuta ya alizeti.

kuhusu mbegu kubwa ya kienyeji pure unaweza kufuga kuchi.


kama kuku wako unawaachia wajitafutie chakula wenyewe kuhusu fomula ya chakula isikuumize kichwa sana pumba inatosha kwa kuku wakubwa ila sivibaya kama utawapa dagaa n.k kama vinapatikana kwa unafuu lakini kwa kuku wadogo kilicho changanywa ni muhimu sana hasa cha kununua ni vizuri kama utapata cha kiwaandani kama utanunua tofauti na cha kiwandani basi ununue kwa mtu ambae anaaminika na yuko competitive .
 
Mtoa mada anaulizia chanjo ya ndui kwa vifaranga, wengi wenu mnakuja na majibu ya kinadharia ya kuchanja kifaranga akiwa na miezi miwili wakati huo ameshapata ndui na amekufa utamchanjaje?
 
Mtoa mada anaulizia chanjo ya ndui kwa vifaranga, wengi wenu mnakuja na majibu ya kinadharia ya kuchanja kifaranga akiwa na miezi miwili wakati huo ameshapata ndui na amekufa utamchanjaje?

sasa ulitaka tuje na majibu ya kivitendo?kama ujaelewa ni bora kuuliza.

mlolongo wa chanjo unaendana na umri wa kuku ambapo siku kifaranga kinapototolewa udungwa chanjo ya marek,baada ya siku saba chanjo ya kideri,baada ya siku 14 gumboro na mwisho baada ya wiki 6 hadi 8 chanjo ya ndui,hapo hautarudia chanjo zote isipokuwa chanjo ya kideri ndio utarudia kila baada ya miezi mitatu zoezi hilo ni endelevu.
 
Ni jambo jema ku-share na wengine maarifa na fursa, hasa na wale wenye moyo wa uthubutu!
 
Kwa Arusha wanunuzi wa kuku wa kienyeji na mayai ya kienyeji wa jumla wako wapi?
 
Ufugaji wa kuku
 
samahan wakuu, bei ya kifaranga cha layers sasahivi ni kiasi gani, kwa kifaranga kimoja
thanks.
 
Habari,nauza Kuku wa kienyeji wa nyama,majogoo wapi 3,bei kila mmoja Tsh 20,000,mawasiliano 0652199902
 
Habari naomba kusaidiwa namna yakuanza kufuga kuku kuanzia kifaranga mpaka hatua ya mayai au kuuzwa...na list ya madawa na chakula
 
Kama hujawahi kuwafuga usiongee maana unaweza amka ukawakuta wote wamekufa
Acha tu mkuuu mimi nina kuku na nguruwe ...mvua ili nyesha ukuta uka anguka nguruwe nikawala hifadh banda zur jiran na banda la kuku bwana eheeee...waka vunja banda lao kuvamia la kuku waka bomoa mabati na skia makelwleee vimejikusanya eneo moja nguruwe akipitisha mdomo ana toka na kuku wa tatu nilitaman kulia nikawa na jikuta na zungumza mwenyewe tu,nika bakisha kuku 80 kat kat ukiamka ukikuta kuku ameanguka swla la kawaida Mungu mwema wamebaki 80
 
Mimi kuku wangu hawalei vfaranga manake nawachukuwa mara tu baada ya kutotolewa... Nilicheka sana pale rafiki yangu alipoona nachukua vfaranga toka kwa mama kuku ingali yupo kwenye kiota chake akasema niwaache wanyonye japo kwa wiki moja...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…