Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Je, ni tofauti gan kati ya kuku hawa na Kuchi?
 
Hivi masoko ya kuku yapoje upande wa dodoma na pia naombeni ushauri nifuge wa aina gani
 
Nahitaji vifaranga broiler kama 100 nataka kuanza ufugaji wa kuku wa kisasa/kizungu. Mwenye nao ani PM.
 
Anae jua bei ya chicken feeder anijuze jaman, nataka kununua kwa ajili ya kianzio wa kuku wangu
 
Habari wapendwa napenda kufahamu nikitaka kufuga kuku wakienyeji ni nini nahitajika nifanye ama nipate ukiachilia mbali banda
 
pata muongozo wa chanjo na siku za kuwapa chanjo.....unaweza andaa pia box kubwa la mbao au utaratibu mwingine kwa vifaranga....

Pata utaratibu wa chakupa chakuku stahili kwa umri na kwa ujazo mkuu, na nini kinatakuwa kwenye mchanganyiko wa kuku.....pia sehemu za kutagia inabd uziandae mapema, kama kuku utakaochukua ni wakubwa.

Jifunze pia dawa za asili mbalimbali, ili ikitokea shida ujue unasolve vipi.....

Usafi wa banda na malazi ya chini, pumba za mpunga au maranda ni msingi kuzizingatia , binafsi nilitumia Pumba za mpunga ila zile zinaleta utitiri usipozutoa baada ya muda mchache kama wiki 1 na siku 3 unatoa ukiacha sana znaleta sana utitiri....ila baada ya kutumia mchanga chini na nyasi naona mafanikio....
 
Binafsi nafuga kuku wa kienyeji ila kuna kitu kikubwa nataka kufanya.....

Nataka nifuge kuku kuroiler wale wakubwa sana kimuonekano,

plan A ni nifuge majogoo tu ya kuroiler yami nipate vifaranga 100 by mwez wa 4 nianze navyo by mwezi wa 12 zile sikukuu ndio nakuwa nawapeleka sehemu mbalimbali kuwauza.....kwamaana wakikua kama 75 basi nitakuwa na faida kubwa.....

Plan B ni kifuga wote tetea na majogoo na kuwachanganya na wakienyeji pure kwaajili ya kuhatamia mayai maana, Kuroiler tetea wake wanataga tu bila kuhatamia mayai....

miezi 6 inakuwa tayari kutoa kuku wako na ukutarget majogoo na sikukuu unakuwa katika advantage ya kuwatoa wengi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…