Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ndugu yangu Kubota hii mbinu ya kulowesha chakula niliwahi itumia baada ya muda kuku walipata mafua.nilipoenda kwa daktari akanielekeza kuacha kuwapa chakula Chenye unyevu na pumba zao akanielekeza nizikaushie kwenye kivuli.vp wewe haikukupa tabu?

Mama Timmy hilo tatizo ninaimani linaweza kutokea, ingawa sikuwahi kufikwa na tatizo hilo. Sikuwa nakilowanisha sana chakula ni kiasi tu cha kufanya chakula kisiwe katika hali ya unga unga ambao kuku walikuwa wakiurusha nje kirahisi pia ilikuwa inawafanya wakati mwingine wachague chenga tu hasa wanapokuwa wameshiba. Naafikiana nawe kwamba kwa afya njema ya kuku kwa ujumla inashauriwa kuepuka vitu vyenye maji maji.
 

Ulichosema mkuu Dafo ni kweli na ni hakika kabisa. Mimi ni shabiki mkubwa wa msemo usemao ukitaka kujua utamu wa ngoma ingia uicheze. Mambo mengi si rahisi kama yanavyoonekana kwa nje.
 
Ahsante sana kwa darasa zuri. Mimi sijaanza ufugaji lkn najifunza sana katika hii thread na ipo siku nitaanza kazi hii.

Asante mkuu endelea kufuatilia thread hii na zingine nyingi za ufugaji wa kuku hawa hapa JF.
 
Nashukuru kwa darasa ndugu yangu.barikiwa
 

Asante Mkuu Guta kwa kunitia hamasa kwa jinsi unavyoifuatilia stori. Maana unaposimulia kitu halafu unaemsimulia anasinzia sinzia wala hakusikilizi au anaangalia angalia saa yake mkononi ni balaa utajisikia vibaya! Masimulizi ya magonjwa yanakuja muda mfupi bahati nzuri wadau michango yao imeshaongelea kwa uzuri sana eneo hilo la magonjwa ambayo ndiyo masumbufu sana. Nitakuja na mimi na version yangu ingawa mchele ni ule ule tofauti ni mapishi tu!
 

Kubota kweli nimejifunza mengi sana kupitia huu uzi, Hata mimi vifaranga vilikuwa vinakufa sana nikivitenga na mama zao hivyo nikaamua niwe nachagua wachache wavilee sasa nimejifunza mbinu mpya. Lakini bado nina tatizo moja kubwa kuna ugonjwa unanisumbua sana na sijapata ufumbuzi bado kuku wanaadhirika machoni na kunakua na lea kama ya mafuta yaliyoganda ndani ya macho, ikiitoa inatoka, kuku anapoteza uwezo wa kuona macho yanabadilika rangi na anadhoofu kwa kuwa hali vizuri, mwisho anakufa. Kuana mtaalam moja huku kijijini kwetu aliniambia kuwa ni chronic respiratory diseases lakini alishindwa kunipa suluhisho la aina ya dawa ninayoweza kuwapa. Naombeni mchango wenu.
 

Nimeipenda hii, na kila mtu humu JF akitoa utaalamu wake kwetu nazani itafikia hatua tutakuwa hatupigi tena kelele kuhusu mamabo ya siasa maana kila mtu atakuwa busy na mihangaiko yake na aikfika JF anaangalia FORUM ya ujasiriamali na kuendelea na mambo yake. hongera mkuu Kubota
 
1) Nawashukuru Controlers wa JF kwa kufanya Update mliyoifanya kama inavyoonekana.
2) Nashukuru wadau kwa kunitia moyo kupitia comments zenu.
3)Mama Timmy mpendwa na Mkuu LiverpoolFC bado tuko wote, niliporudi toka kwenye mkaa wangu jana nilikuta watu wangu hamjapita kusoma, na mimi ninasubiri hadi msome kwanza ndiyo niendelee, twende hivyo hivyo taratibu jamani.

Right now ninaandika kasheshe za magonjwa, subirini kidogo namalizia, na tanuli langu jipya la mkaa ndiyo ninaliwasha usiku wa leo sasa huwa hatulalagi siku hiyo, likifunguka haupo asubuhi unakuta majivu tu. Kwa hiyo labda nitawasilisha Ijumaa au Jumamosi. Msichoke jamani hapa JF ni kama nyumbani tunakimbilia wapi? Ila tuendelee kujadiliana na kubadilishana uzoefu.
 

Mimi binafsi nimepata maujanja mengi sana hapa JF na imekuwa chanzo cha kubadili maisha yangu and my life will never be the same again! Acha tu niyapange vizuri mahesabu from matanuru yangu ya mkaa, na mimi lazima nitaichangia JF kuishukuru! JF ni kila kitu walahi!

 
Wakuu, Habari ya Utafutaji?

Pamoja na michango mizuri ya Wanajamvi, nami napenda kuchangia kama ufuatavyo:

Karibu kila mtu huwa anataka kuwa tajiri. Tatizo, wengi wetu hatupo tayari kulipa gharama (we are not ready to leave the comfort zone).

Kuna aina kadhaa za umasikini, mojawapo ni umasikini wa fikra/ mawazo. Tukiuondoa kwanza umasikini huu wa mawazo, ni rahisi kuondokana na umasikini wa kipato. Hakuna njia ya mkato zaidi ya kupenda kujisomea/ kusikiliza vitabu / machapisho au cd mbalimbali zinazungumzia maisha ya watu waliofanikiwa au kanuni za mafanikio. Hakuna mbadala.

Ndugu Wanajamvi, tafuteni vitabu hivi na kuvisoma kwa kuanzia, mapema iwezekanavyo THE CASHFLOW QUADRANT, THE BUSINESS SCHOOL & THE BUSINESS OF THE 21ST CENTURY vyote vikiwa vimeandikwa na Robert T. Kiyosaki. Vinapatikana kwenye maduka yafuatayo: Scholastic Bookshop (Mlimani City & Posta), Dar es Salaam Printers, Saramanda, n.k. Pia, kwa wauza vitabu stand ya mabasi ubungo vinapatikana.

Ninasema kwa kuanzia, kwa maana kwamba kuna vitabu vingi vizuri (sio vya Robert Kiyosaki peke yake) lakini vitabu hivi vitakusaidia kukupa mwanga zaidi juu ya Biashara na Ujasiriamali katika karne hii ya 21, hasa kwa watu ambao tunakumbwa na changamoto za Usimamizi na Mitaji ya mawazo ya Biashara zetu bila kusahau Ofisi/Eneo (premisis) la kufanyia biashara na Stadi /Mbinu za Biashara. Zaidi, vitakupa muongozo mzuri namna unavyoweza kuutumia muda wako wa ziada (part time) kujenga TIMU ya watu watakaokuwa wanakufanyia kazi (SYSTEM/ NETWORK) kama ambavyo Bakheresa, Mengi, Manji, Mkono, n.k walivyo na wanavyoendelea kufanya.

Kwa mawasiliano zaidi, piga 0713 366 473 au 0767 277 223.

KILA LA KHERI WAKUU.
 
Kubota pole na mikaa, hawa kienyeji wako pure wanachukua muda gani hadi kuuzwa au kutaga. Hawa hybrid miezi sita kutaga ila majogoo wanaendelea kukua. Na wanakoma kutaga umri gani?
 
Hapo kwenye vifo vya vifaranga ndipo napahitaji kwani nazalisha vifaranga 20 nabakia na viwili mwisho wa siku

 

Je unawapatiaje joto? Inabidi uweke taa za umeme ama vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…