Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ndugu yangu Kubota hii mbinu ya kulowesha chakula niliwahi itumia baada ya muda kuku walipata mafua.nilipoenda kwa daktari akanielekeza kuacha kuwapa chakula Chenye unyevu na pumba zao akanielekeza nizikaushie kwenye kivuli.vp wewe haikukupa tabu?

Mama Timmy hilo tatizo ninaimani linaweza kutokea, ingawa sikuwahi kufikwa na tatizo hilo. Sikuwa nakilowanisha sana chakula ni kiasi tu cha kufanya chakula kisiwe katika hali ya unga unga ambao kuku walikuwa wakiurusha nje kirahisi pia ilikuwa inawafanya wakati mwingine wachague chenga tu hasa wanapokuwa wameshiba. Naafikiana nawe kwamba kwa afya njema ya kuku kwa ujumla inashauriwa kuepuka vitu vyenye maji maji.
 
Mkuu Kubota bado tuko pamoja kwenye hili darasa.Kwajinsi navyosoma uzoefu wako hapa kuna wakati najihisi kabisa kama nafahamu mazingira yako na jinsi unavyojitoa katika ufugaji.Kiukweli kuku wetu wa asili tulizoea kuwafuga hasa kama kitoweo ukuaji wake ni mdogo, ingawa akipunguziwa shughuli ile ya kutafuta chakula mwenyewe anaweza akaongezeka kasi ya kukua kidogo lakini sio sawa na wa kisasa.Kuku wa asili inamuhitaji miezi 5 hadi 6 hadi aanze kutaga ambayo ni sawa na kuku wa mayai lakini tofauti inakuja kwenye idadi ya mayai kwa mwaka anyoweza kutaga.Kutokana na kutorishishwa na ukuaji wa kukua wa asili nadhani ndio maana watu wakaamua kuanza kufuga kuku chotara ambao kwa kweli ukuaji wao unarihisha na hata ukiwafuga unafurahia kuwaona na uzito wa kutosha.Katika hali ya kawaida kabisa ukimwambia mtu ambaye hajawahi kufuga kuwa unafuga kuku wa kienyeji moja kwa moja anachulia ni kitu rahisi sana ni kiasi cha kufungua banda asubuhi na kufunga jioni lakini ukija kumpa hii shule na uliyopitia atakuwa umemfungua akili na kuona sio shughuli rahisi hivyo.Mimi naelewa ulikopitia kwa sababu mimi pia nina uzoefu wa ufugaji na ni hobby yangu kubwa tu.Kwa sasa ngoja niishie hapa tukisubiria nondo zako mkuu.

Ulichosema mkuu Dafo ni kweli na ni hakika kabisa. Mimi ni shabiki mkubwa wa msemo usemao ukitaka kujua utamu wa ngoma ingia uicheze. Mambo mengi si rahisi kama yanavyoonekana kwa nje.
 
Ahsante sana kwa darasa zuri. Mimi sijaanza ufugaji lkn najifunza sana katika hii thread na ipo siku nitaanza kazi hii.

Asante mkuu endelea kufuatilia thread hii na zingine nyingi za ufugaji wa kuku hawa hapa JF.
 
Mama Timmy hilo tatizo ninaimani linaweza kutokea, ingawa sikuwahi kufikwa na tatizo hilo. Sikuwa nakilowanisha sana chakula ni kiasi tu cha kufanya chakula kisiwe katika hali ya unga unga ambao kuku walikuwa wakiurusha nje kirahisi pia ilikuwa inawafanya wakati mwingine wachague chenga tu hasa wanapokuwa wameshiba. Naafikiana nawe kwamba kwa afya njema ya kuku kwa ujumla inashauriwa kuepuka vitu vyenye maji maji.
Nashukuru kwa darasa ndugu yangu.barikiwa
 
Ahsante Mkuu Dafo , sina uhakika na chanjo niliyowapa kama ina fanya kazi, niliinunua na duka liko karibu na ninapoishi niliitumia maramoja tu nikatupa iliyobaki kwa kuwa waliniaambia ikiishiwa ubaridi inaishiwa nguvu.
kama itawezekana wakati tunamsubiri Kubota unaweza kutuelezea magonjwa ya kuku na dalili zake hasa vifaranga. magonjwa yananichanganya kati ya mdondo na huu wa kuvaa makoti Yellow diarrhea or fowl typhoid kama @Mama Joe
alivyodokeza. @Mama timmy inaelekea tiba mbadala unauzoefu nazo thanks. Ngoja tusubiri na mbinu za kubota naamini tutafanikiwa. thanks all.

Asante Mkuu Guta kwa kunitia hamasa kwa jinsi unavyoifuatilia stori. Maana unaposimulia kitu halafu unaemsimulia anasinzia sinzia wala hakusikilizi au anaangalia angalia saa yake mkononi ni balaa utajisikia vibaya! Masimulizi ya magonjwa yanakuja muda mfupi bahati nzuri wadau michango yao imeshaongelea kwa uzuri sana eneo hilo la magonjwa ambayo ndiyo masumbufu sana. Nitakuja na mimi na version yangu ingawa mchele ni ule ule tofauti ni mapishi tu!
 
Kuna maandiko mengi JF ya ufugaji Kuku wa Kienyeji! Nawasilisha kwenu wadau wa JF mbinu ambazo kwa mikono yangu nimezitumia kutatua changamoto za kuku wa kienyeji! Nimeandika kuwalenga wajasiliamali ambao hawana nguvu kifedha kujenga mabanda kisasa, mashine kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa wala kujenga wigo (fence) n,k. Naomba mzijue mbinu hizi nisije kufa nazo, huu ni mchango wangu kwenu watanzania wenzangu wale ambao mtakuwa hamjawahi kuzisikia mbinu hizi. Mbinu hizi baadhi nilisoma vitabuni nikazijaribu na kuziboresha kwa mazingira yangu duni! Mbinu zingine niliziona kwa wakulima duni kama mimi nikazitumia na kuleta mafanikio makubwa, mbinu zingine nilizigundua mwenyewe na nikafanikiwa sana. Hizi mbinu hazijafanyiwa utafiti rasmi lakini nimeweza kufanikiwa kuwa na kundi kubwa la kuku kwa haraka sana kupitia ujanja huu!!

Mdau wa JF nakualika utembelee uzi huu mara kwa mara kila upatapo fursa ili uweze kufuatilia simulizi yangu maana itakwenda kwa vipande vipande. Mnakaribishwa kuchangia uzoefu wenu ili tuboreke zaidi.

Mbinu hizi zitagusia zaidi: Utotoreshaji vifaranga vingi kwa mara moja bila kutumia mashine! Ukuzaji wa vifaranga vingi kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi, ulinzi wa kuku dhidi ya wanyama maadui, kudhibiti kuku wasizurule, magonjwa niliyofanikiwa kuyadhibiti, ujenzi wa vibanda wenye kukidhi mahitaji mbali mbali. Ni utaalamu nilioupata kwa gharama kubwa na mahangaiko ya muda mrefu, nauleta kwenu ili sote tuendelee kukua pamoja kiujasilia mali.

Stay tuned and keep on visiting this thread!!

Kubota kweli nimejifunza mengi sana kupitia huu uzi, Hata mimi vifaranga vilikuwa vinakufa sana nikivitenga na mama zao hivyo nikaamua niwe nachagua wachache wavilee sasa nimejifunza mbinu mpya. Lakini bado nina tatizo moja kubwa kuna ugonjwa unanisumbua sana na sijapata ufumbuzi bado kuku wanaadhirika machoni na kunakua na lea kama ya mafuta yaliyoganda ndani ya macho, ikiitoa inatoka, kuku anapoteza uwezo wa kuona macho yanabadilika rangi na anadhoofu kwa kuwa hali vizuri, mwisho anakufa. Kuana mtaalam moja huku kijijini kwetu aliniambia kuwa ni chronic respiratory diseases lakini alishindwa kunipa suluhisho la aina ya dawa ninayoweza kuwapa. Naombeni mchango wenu.
 
Kuna maandiko mengi JF ya ufugaji Kuku wa Kienyeji! Nawasilisha kwenu wadau wa JF mbinu ambazo kwa mikono yangu nimezitumia kutatua changamoto za kuku wa kienyeji! Nimeandika kuwalenga wajasiliamali ambao hawana nguvu kifedha kujenga mabanda kisasa, mashine kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa wala kujenga wigo (fence) n,k. Naomba mzijue mbinu hizi nisije kufa nazo, huu ni mchango wangu kwenu watanzania wenzangu wale ambao mtakuwa hamjawahi kuzisikia mbinu hizi. Mbinu hizi baadhi nilisoma vitabuni nikazijaribu na kuziboresha kwa mazingira yangu duni! Mbinu zingine niliziona kwa wakulima duni kama mimi nikazitumia na kuleta mafanikio makubwa, mbinu zingine nilizigundua mwenyewe na nikafanikiwa sana. Hizi mbinu hazijafanyiwa utafiti rasmi lakini nimeweza kufanikiwa kuwa na kundi kubwa la kuku kwa haraka sana kupitia ujanja huu!!

Mdau wa JF nakualika utembelee uzi huu mara kwa mara kila upatapo fursa ili uweze kufuatilia simulizi yangu maana itakwenda kwa vipande vipande. Mnakaribishwa kuchangia uzoefu wenu ili tuboreke zaidi.

Mbinu hizi zitagusia zaidi: Utotoreshaji vifaranga vingi kwa mara moja bila kutumia mashine! Ukuzaji wa vifaranga vingi kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi, ulinzi wa kuku dhidi ya wanyama maadui, kudhibiti kuku wasizurule, magonjwa niliyofanikiwa kuyadhibiti, ujenzi wa vibanda wenye kukidhi mahitaji mbali mbali. Ni utaalamu nilioupata kwa gharama kubwa na mahangaiko ya muda mrefu, nauleta kwenu ili sote tuendelee kukua pamoja kiujasilia mali.

Stay tuned and keep on visiting this thread!!

Nimeipenda hii, na kila mtu humu JF akitoa utaalamu wake kwetu nazani itafikia hatua tutakuwa hatupigi tena kelele kuhusu mamabo ya siasa maana kila mtu atakuwa busy na mihangaiko yake na aikfika JF anaangalia FORUM ya ujasiriamali na kuendelea na mambo yake. hongera mkuu Kubota
 
1) Nawashukuru Controlers wa JF kwa kufanya Update mliyoifanya kama inavyoonekana.
2) Nashukuru wadau kwa kunitia moyo kupitia comments zenu.
3)Mama Timmy mpendwa na Mkuu LiverpoolFC bado tuko wote, niliporudi toka kwenye mkaa wangu jana nilikuta watu wangu hamjapita kusoma, na mimi ninasubiri hadi msome kwanza ndiyo niendelee, twende hivyo hivyo taratibu jamani.

Right now ninaandika kasheshe za magonjwa, subirini kidogo namalizia, na tanuli langu jipya la mkaa ndiyo ninaliwasha usiku wa leo sasa huwa hatulalagi siku hiyo, likifunguka haupo asubuhi unakuta majivu tu. Kwa hiyo labda nitawasilisha Ijumaa au Jumamosi. Msichoke jamani hapa JF ni kama nyumbani tunakimbilia wapi? Ila tuendelee kujadiliana na kubadilishana uzoefu.
 
Nimeipenda hii, na kila mtu humu JF akitoa utaalamu wake kwetu nazani itafikia hatua tutakuwa hatupigi tena kelele kuhusu mamabo ya siasa maana kila mtu atakuwa busy na mihangaiko yake na aikfika JF anaangalia FORUM ya ujasiriamali na kuendelea na mambo yake. hongera mkuu Kubota

Mimi binafsi nimepata maujanja mengi sana hapa JF na imekuwa chanzo cha kubadili maisha yangu and my life will never be the same again! Acha tu niyapange vizuri mahesabu from matanuru yangu ya mkaa, na mimi lazima nitaichangia JF kuishukuru! JF ni kila kitu walahi!

Wakuu, Habari ya Utafutaji?

Pamoja na michango mizuri ya Wanajamvi, nami napenda kuchangia kama ufuatavyo:

Karibu kila mtu huwa anataka kuwa tajiri. Tatizo, wengi wetu hatupo tayari kulipa gharama (we are not ready to leave the comfort zone).

Kuna aina kadhaa za umasikini, mojawapo ni umasikini wa fikra/ mawazo. Tukiuondoa kwanza umasikini huu wa mawazo, ni rahisi kuondokana na umasikini wa kipato. Hakuna njia ya mkato zaidi ya kupenda kujisomea/ kusikiliza vitabu / machapisho au cd mbalimbali zinazungumzia maisha ya watu waliofanikiwa au kanuni za mafanikio. Hakuna mbadala.

Ndugu Wanajamvi, tafuteni vitabu hivi na kuvisoma kwa kuanzia, mapema iwezekanavyo THE CASHFLOW QUADRANT, THE BUSINESS SCHOOL & THE BUSINESS OF THE 21ST CENTURY vyote vikiwa vimeandikwa na Robert T. Kiyosaki. Vinapatikana kwenye maduka yafuatayo: Scholastic Bookshop (Mlimani City & Posta), Dar es Salaam Printers, Saramanda, n.k. Pia, kwa wauza vitabu stand ya mabasi ubungo vinapatikana.

Ninasema kwa kuanzia, kwa maana kwamba kuna vitabu vingi vizuri (sio vya Robert Kiyosaki peke yake) lakini vitabu hivi vitakusaidia kukupa mwanga zaidi juu ya Biashara na Ujasiriamali katika karne hii ya 21, hasa kwa watu ambao tunakumbwa na changamoto za Usimamizi na Mitaji ya mawazo ya Biashara zetu bila kusahau Ofisi/Eneo (premisis) la kufanyia biashara na Stadi /Mbinu za Biashara. Zaidi, vitakupa muongozo mzuri namna unavyoweza kuutumia muda wako wa ziada (part time) kujenga TIMU ya watu watakaokuwa wanakufanyia kazi (SYSTEM/ NETWORK) kama ambavyo Bakheresa, Mengi, Manji, Mkono, n.k walivyo na wanavyoendelea kufanya.

Kwa mawasiliano zaidi, piga 0713 366 473 au 0767 277 223.

KILA LA KHERI WAKUU.
 
Kubota pole na mikaa, hawa kienyeji wako pure wanachukua muda gani hadi kuuzwa au kutaga. Hawa hybrid miezi sita kutaga ila majogoo wanaendelea kukua. Na wanakoma kutaga umri gani?
 
Hapo kwenye vifo vya vifaranga ndipo napahitaji kwani nazalisha vifaranga 20 nabakia na viwili mwisho wa siku

Wana JF natumaini hamjambo, ni siku nyingine naomba niendelee na simulizi ya mihangaiko yangu ya ufugaji wa Kuku wa Kienyeji!

Naomba nisisitize kutokana na nilichoshuhudia ni kuwa wafugaji wengi huishia kubaki na idadi ndogo ya kuku, hii hasa kutokana na utotoaji duni au vifo vingi sana vya vifaranga. Mbinu ya kuwatenganisha vifaranga na mama zao na kuwakuza peke yao ikifanywa kwa uangalifu hupanua kundi la kuku kwa haraka sana. Kuna utenganishaji ambao hufanyika mara tu vifaranga wanapototolewa aina hii huwezesha kuku kuwa na awamu nyingi za utagaji na uatamiaji kufikia hadi awamu 6 kwa mwaka. Kwa wale wenye mashine za kutotolesha vifaranga ambako kuku hawaachwi kuatamia kabisa, kuku hao huweza kutaga mayai mengi zaidi kwa mwaka kulingana na uwezo wa aina ya kuku.

Mimi sikuwa na mashine ya kutotolesha na wala sikuweza kuwatenganisha vifaranga mara baada ya kutotolewa kwa kuwa sikuwa na miundo mbinu yenye kuwezesha kufanya hivyo. Niliwategemea kuku hao hao kuatamia na kukuza vifaranga. Isipokuwa sasa tofauti na kawaida, mimi nilipunguza idadi ya kuku wa kuatamia kwa kuwapa mayai mengi kuku wachache wayaatamie ili wengine badala ya kuatamia mayai machache wakaendelee kutaga, pia baada ya hawa kuku wachache kutotolesha, vifaranga vyao nilivikabidhi kwa kuku wachache zaidi kama nilivyosimulia jana, ili na hawa nao warudi kundini kutaga! Kuwa na kuku wengi wanaotaga kulisaidia kupata lishe na kuuza mayai ambapo nilikuwa napata pesa ya kununulia chakula na dawa za kulea vifaranga na kuku wote.

Baada ya kumudu kuweza kutotolesha vifaranga kwa wingi liliibuka tatizo la vifo vya vifaranga kiasi ambacho kilianza kunikatisha tamaa kabisa! Ilinichukua muda sana nikijiuliza kwa nini? Hadi kufikia napata ufumbuzi nilikuwa nimeshatupa vifaranga wengi sana, nitalielezea hili vizuri wakati wake ukifika hapo baadae.
 
Ni kweli usemavyo.kutibiwa ni lazima kuku akipata maradhi.ila Kama ukiwa na mazoea ya kutumia Haya majani Kama lishe inasaidia sana kuku kutokuonewa na magonjwa hovyo hovyo.mimi nafuga wa kienyeji kabisa na ninawatoa kwa mama Yao mara wanapoanguliwa na kukauka nawafuga Kama broiler kwa wiki Sita tu.baada ya hapo naendelea nao Kama kawaida ya kienyeji.

Je unawapatiaje joto? Inabidi uweke taa za umeme ama vipi?
 
Back
Top Bottom