habari za Easter wadau, tumerudi tena sasa huko wengine tulikuwa hakuna network. Hongera LiverpoolFC kwa kuongeza vinyoya, kweli umejitahidi sana kaza buti, mimi wangu wanaendelea vizuri.
Kuhusu soko Kubota, mimi sikuwa na wa kuuza labda wadau wengine waje watatuelezea. Kila la heri.
Karibu sana JF, Mkuu Mbugazetu! Hapa ndiyo Forum ya ujasiriamali na hii umeingia ni thread ya ufugaji wa kuku wa kienyeji. Karibu sana mgeni wetu!Maisha ni jinsi unavyoyatengeneza kama wazazi wako walikupeleka shule na ukakubali kusoma,elimu uliyo ipata ukaitumia kwenye maisha ya kila siku,hakika lazima ufanikiwe.
Mkuu Kubota unaendelea kukusikilizia kwenye darasa lako!Karibu sana JF, Mkuu Mbugazetu! Hapa ndiyo Forum ya ujasiriamali na hii umeingia ni thread ya ufugaji wa kuku wa kienyeji. Karibu sana mgeni wetu!!
mkuu Kubota tunaendelea kukusikilizia kwenye darasa lako!
Mkuu muda si ni kama wa kuku siku 21? haiana tofauti na kuku, Mkuu China kampuni ziko nyingi mno zinazo tenegneza Incubators na bei zao ziko Chini kabisa ingawa kuna zingine ni ghali, Ila ya Mayi 1500 mpaka kuifikisha Babdari ya Dar ni kama Milioni Moja na Lakini Mbili tatu, Ya mayai Buku ni kama laki 9 hivi,
Kashasepa,ngoja niende zangu MMU.
Karibu sana mkuu na hongera kwa kuwa na mawazo ya kijasiriamali...Ndugu wanajf mimi ni mgeni humu ndan lakin nimeona mwanga tulivu kwani nafuga kuku wa kienyej kupitia uzi huu nimejifunza jins ya kuboresha mradi wangu,soon ntakuwa na mashine ya kutotoleshea vifaranga,naomba ushaur zaid ili nijikwamue kimaisha..thanx an God bless u all!
Poa Mkuu betlehem, darasa litaendelea usikae mbali. Nilipause kidogo maana unajua wachangiaji ndiyo wanaoamsha masuala ya kujadili na wachangiaji wangu nadhani hizi mvua zimewakeep bize kulima, hawaingii jukwaani. Mimi hizi mvua kwenye matanuru yangu ya mkaa mbona ni baraka, bwana miti anavyoogopa mvua, tunajimegea tu miti. Halafu na kamshahara kake bado hajakamaliza hadi aishiwe atakuta nimeshapakuwa huyooo mjini.
Ndugu wanajf mimi ni mgeni humu ndan lakin nimeona mwanga tulivu kwani nafuga kuku wa kienyej kupitia uzi huu nimejifunza jins ya kuboresha mradi wangu,soon ntakuwa na mashine ya kutotoleshea vifaranga,naomba ushaur zaid ili nijikwamue kimaisha..thanx an God bless u all!
Mkuu Kubota katika pita pita zangu nimekutana na hii kitu au maarifa kutoka kwa moja ya wafugaji wanaofuga kuku wa kienyeji kibiashara..
Wanadai ukitaka kuku atage na kutotoa vifaranga wengi na wakue na afya nzuri na kwa speed nzuri (good growth rate) inabidi uhakikishe kuku wenye uhusiano wa damu hawapandani. Yaani kama ni jogoo basi lisiwe na undugu wowote na mitetea, kama ni baba asiwapande watoto wake, majogoo nayo yasiwapande mama zao, lakini pia kaka na dada wasipandane...
Wanadai ukifanikiwa kwa hilo utaangua vifaranga wengi kwa muatamio mmoja na vifaranga vitakua kwa speed kali mno na havidhuriwi sana na magonjwa...Sijui kama mlikua mnaijua hii kitu...
Kitu ambacho nimekua nikifuatilia sijapata jibu ni suala la vyakula gani umlishe kuku wa kienyeji ili atage mayai kwa wingi, maana katika kuku wa kisasa hii kitu ipo. Watengenezaji wa vyakula vya kuku huchanganya baadhi ya vyakula vinavyomp kuku stimu za kutaga (anakua na stimu za kudondosha mayai kama mtu aliye na tumbo la kuhara anavyokuwa na stimu za kudodondosha zigo lake kwa choo)..
Nikifanikiwa kupata hili nitamwaga jamvini hapa ila kama kuna wakuu wengine wana ideas wanaweza kutumwagia hapa...
Mkuu ina maana bei za incubator ndio zimeshuka hivi aisee??? Maana juzi kati niliona ya mayai kama 500 hivi ilikua zaidii ya Million 4...Au umekosea ku-type mkuu??
Kama bei ni hii basi na mie nikaagize fasta maana kutotoa kwa kutegemea kuku wenyewe ni mateso sana aisee....[/QUOTE
Mkuu Asigwa, usishangae, Chasha hajakosea kutype !!! Ukibahatika kuona bei ya vitu vya China kwenye mtandao, utashangaa sana na unaweza kulia na wahindi wanaoagiza vitu huko na kutubamiza mibei ya kutisha kwenye maduka yao ya uhindini. Ukiingia kwenye mtandao ukaangalia bei za mashine mbali mbali na vifaa vya kilimo hata mashine za kukamulia alizeti huwezi kuamini bei zilivyo!! Kwa mfano kuna powertiller (horse power 15) inajembe la kuchavanga kwenye mpunga, ina trailer ya tani 1, ina mashine ya kupandia, ina jembe la kulimia plow inauzwa USD 2000. Ukibadili USD kwenda T sh ni kama shillingi 3,300,000/= ukijumlisha na gharama za kukomboa bandarini hata zikifika millioni 5 bado ni bei poa sana ukilinganisha na bei za uhindini ambazo si chini ya 9 millioni.
Kwa hili Chasha anamaanisha alichokiandika, na mwenyewe ataongezea. Ingia ucheze uone utamu wa ngoma mkuu Asigwa.
| Jane wang |